Nchi imegubikwa na mashaka CCM wamechakachua maboksi ya kura........... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nchi imegubikwa na mashaka CCM wamechakachua maboksi ya kura...........

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Nov 1, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Nov 1, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,852
  Trophy Points: 280
  Jumla ya mawaziri 14 hivi hadi sasa yasadikiwa wamepoteza viti vyao lakini kila mahali wakubwa hao wanakataa matokeo na kutaka kura zihesabiwe upya!!!!!!!!!!!!!!......

  Katika sheria ya uchaguzi ni kwa amri ya mahakama tu ndiyo unaweza kupita kibali cha kurudia kuzihesabu kura tena lakini viongozi wa CCM serikalini wanatumia madaraka yao kushinikiza wasimamizi wa majimbo ya chaguzi ambao ni wadogo wao kiajira kurudia kuzihesabu kura kinyume na sheria.............

  Swali la kujiuliza hivi ni kwa nini CCM wanaamini mwaka huu kura zimekosewa kuhesabiwa na kwa nini hawasubiri matokeo yatangazwe kama sehemu nyingine ambazo wamefanya vizuri?

  Yaelekea NEC inapoona CCM imeshindwa ipo tayari kurudia kuhesabu kura ili kuyachakachua matokeo ya ridhaa ya wananchi na hili huenda likaielekeza nchi kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe........Ni lazima wasiwasi uwepo wa usalama wa maboksi vinginevyo CCM wasingeshupalia kura zihesabiwe tena yaani hata mawakala wao waliowaweka wenyewe hata hawaamini tena...........

  Wapo wanaona ya kuwa kama majemedari wa JK wataonekana wameanguka itakuwa vigumu kwa serikali ya CCM kumtangaza Jk kibabe kuwa ameshinda na hivyo ni lazima watumie nguvu ya dola kuhakikisha ya kuwa majemedari wake ambao ni mawaziri wanakubalika na jamii jambo ambalo siyo kweli hata kidogo ...........

  Kukosekana kwa NEC kuwa na waajiriwa wa kudumu kumechangia katika serikali ya CCM kuvuruga riidhaa ya wananchi kwa kuwatumia watendaji wa serikali za mitaa hususani Ma-DED.....katika kuchakachua ridhaa ya wapigakura
   
 2. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #2
  Nov 1, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  walisema watakubali matokeo mbona sasa hawakubali, wakubali kama kuna mushkeli waende mahakamani basi hamna jinsi
   
 3. Nenga

  Nenga Member

  #3
  Nov 1, 2010
  Joined: Sep 3, 2007
  Messages: 75
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 15
  Si ndio muda wa kuongeza kura za kuchakachua hapo.
   
 4. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #4
  Nov 1, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Shime Watanzania tukataeni kurudia kuhesabu kura. Kama hawaridhiki na matokeo wajiandae kwenda Mahakamani.
  Hivi ingelikuwa ni WAPINZANI WANADAI KURUDIA KUHESABU KURA wangekubali??????????????????

  Kwanini CCM wanacheza na HAKI ZA WATANZANIA.
   
 5. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #5
  Nov 1, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Matokeo wanayaona machungu wakati sisi ndio tumepiga kura
   
 6. g

  gidytitus JF-Expert Member

  #6
  Nov 1, 2010
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 332
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Hivi kwel JK Nyerere angekuwepo aya yote yange2kuta? Huu ndo wakat wa kumkumbka Ding yetu! Hi ndo shda ya nyumba kuongozwa na mtoto wa kimada! Watanzania shime wakat ndo huu wa kujtoa kwa ajil ya watoto we2! Wala tusjarb kuweka iman ye2 kwa NEC kua ipo kwa maslah ya umma, TUSAHAU KABISA kua Tz bila kuchukua hatua ya kuondoa hawa mafsad moja bada ya mwngne raslmal ze2 ztaibiwa na kukobwa zote, mi naona wale walokuwa wakiamin kua viungo vya albino vyaweza kuwatajirsha mi nawashaur sasa waanze kutafuta hao mafsad kwan hao ndo wamekalia nyota zao, wakiwamalza hao nadhan maisha yao yatakuwa raha mstarehe. TANZANIA BILA CCM IMEWEZEKANA SASA!
   
Loading...