hazard Don
JF-Expert Member
- Oct 9, 2017
- 1,165
- 947
Sio kweli.Haya mnayo yaona leo ni matokeo ya mtu mmoja Mbowe ya kumleta Lowasa Ukawa,hili lilikuwa bonge la kosa ambalo kwa mtu makini kabisa kwa kosa lile alitakiwa ajihudhuru, ila Mbowe anadunda, untouchable, ukimkosoa humu watu wanakushambulia.
Nilikiwa mwanasiasa kindakindaki wa CHADEMA chuo kuanzia 2009,ila baada ya Lowasa kuingia nilikaa pembeni,nikabezwa,nikapondwa baada ya UKAWA kupata viti vyingi bungeni,ila baada ya wabunge kuanza kurudi CCM ,kuna watu niliwaambia 2020 hali itakuwa mbaya sana na leo tuna yaona.
CHADEMA mlivyo mleta Lowasa UKAWA na kujiamini kwamba mpo imara,kumbe mliacha nyumba yenu mliyokuwa mnaijenga kidogo kidogo kwenye mwamba na kwenda kujenga kwenye mchanga kisa tu kuna urahisi.Sasa angalieni leo mnayo yapata ni haki yenu hamjaibiwa hata kura moja.
CHADEMA mkitaka kusimama tena mnabidi muanze upya mfumue chama chote na mkijenge CHAMA kupitia vijana wenu na watu wenu mlio waandaa nyinyi na si kunyakua wanasiasa kutoka CCM na mnatakiwa kiwaamini watu wenu.