Nchi iliyo serious na Uchumi haiwezi kuokoa vitega uchumi kwa njia za kizamani

Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
21,414
37,618
Sekta ya Utalii ni miongoni mwa mito inayolisha Taifa letu kiuchumi. Miongoni mwa vivutio vikubwa vya Utalii ni Mlima Kilimanjaro.
Leo ni zaidi ya siku 5 chanzo hiki kikubwa cha mapato ya nchi yetu kinateketea kwa moto na kupoteza uasili wake.

Njia za kupandia mlima zinaharibika, mahema ya kupumzikia watalii yanateketezwa kwa moto na hivyo kuzua hofu kwa Watalii walio na ratiba ya kupanda mlima.

Cha kushangaza moto huo mkubwa unadhibitiwa kwa kutumia matawi ya miti. Hivi tuko makini kweli kuacha Mlima Kilimanjaro uteketee kwa moto huku Serikali ikiwaachia askari wa TANAPA watumie njia za kizamani za kuzima moto?

Kwanza wao wenyewe wanaathirika na hali ya hewa hivyo kuwa vigumu kupanda mlima unaoungua. Ukiongeza na hewa ya Ukaa inayoongezeka kwa kuungua majani, miti na misitu, hewa ya Oksijeni inapungua sana na hivyo kufanya ufanisi mdogo wa wazimaji hawa kuisha kabisa kwani wanabaki kupigania roho zao kwa kutafutiza hewa haba iliyobaki.

Hivi hatuoni aibu kumwonyesha mhifadhi kila siku kwenye TV akihangaika na vijana wake kuzima moto kwa matawi ya miti?
Tumegeuka Taifa ya Makomediani.
 
Back
Top Bottom