Nchi ilikuwa imeoza yote, tumuombee Magufuli na Majaliwa waendelee kutumbua Majipu uchungu

K 4 LIFE

JF-Expert Member
Jul 21, 2015
2,567
416
nachoweza kusema ni kwamba magufuli kaipokea nchi ikiwa imejaa majipu mwili mzima, tunachotakiwa ni kumuombea kwa mungu yeye magu na majaliwa waendelee kutumbua majipu uchungu mpaka yaishe, ila ulinzi wa moja ni muhimu kwani wanagusa maslahi ya mafisadi hatari.
 
Jip main wanalikwepa,,,tusingefika hapo unafikir nani aliachia mianya yote hii kama c yy wa white house
 
Itafutwe namna ya kuiajibisha Serikali ya awamu ya nne kwa uchafu na aibu walioiletea nchi hii.
 
nachoweza kusema ni kwamba magufuli kaipokea nchi ikiwa imejaa majipu mwili mzima, tunachotakiwa ni kumuombea kwa mungu yeye magu na majaliwa waendelee kutumbua majipu uchungu mpaka yaishe, ila ulinzi wa moja ni muhimu kwani wanagusa maslahi ya mafisadi hatari.

Ujumbe mzuri sana.
Ni wajibu wa kila mtanzania kumtakia kheri Magufuli maana kazi anayofanya ni kubwa na hatari.
Kumbuka JPM aliwahi sema alipoingia alikuta hali mbaya sana kiasi kwamba hata mishahara hailipiki
 
Hapa umenena pwenti kubwa sana

Kila mtu alikuwa afisa usalama,
Lugha ya unanijua Mimi ni nani ilitawala kila kona
Ukiiba au ukimtapeli mtu ndo unaonekana shujaa
Wizi kila kona
Mpaka hali ya hewa kwa ujumla ilikuwa mbaya joto kupitiliza
 
Itawajibishwaje serikali ya awamu ya nne wakati aliyekuwa amilijeshi mkuu amesha teuliwa kuwa mkuu wa chuo UDSM!
 
Tanzania haijawai kuwa na awamu ya nne

Umeongea au umeandika kwa hasira au pengine kwa kutia chumvi mno. Awamu ya nne ilikuwepo, lakini ni kweli awamu hii itakumbukwa kwa mengi huku mabaya yakichukua nafasi kubwa.

MAZURI:

Uhuru mkubwa wa kutoa mawazo
Uhuru wa kusafiri
Kupanuka kwa mawasiliano ndani ya jamii na hata nje ya jamii (nchi)
Kusambaa kwa bidhaa nyingi

MABAYA:
Kuongezeka kwa pengo kati ya matajiri na maskini

Wenye fedha kushika madaraka ya kiuchumi, kisiasa na kijamii

Kushamiri kwa wizi, ufisadi wa mali za umma

Kushamiri kwa rushwa kila katika kila sekta na hasa kwenye vyombo vya dola na vya maamuzi

Kushindwa kwa mfumo wa uongozi na utawala kufanya kazi

kushuka kwa nidhamu ya wafanyakazi katika sekta za umma

Upendeleo katika kutoa vyeo kwenye sekta za umma -wakuu wa mashirika, wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa na hata mawaziri- entrenchment of patrimonialism, clientelistic and patronage tendencies into our society.

Kushamiri kwa majungu katika maeneo yote ya kazi huku majungu na fitina ikiwa ni sifa za mtu kupata madaraka

Kushamiri kwa utengano wa watu kwa kuzingati maeneo hali iliyojitokeza hata katika upigaji wa kura - Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro kujitokeza kuwa ni Pemba ya Tanzania bara katika masuala ya kisiasa.

Kushamiri kwa ujanja ujanja katika uendeshaji wa maisha- Baadhi ya watu kuishi bila kufanya kazi-madalali, matapeli, madawa ya kulevya n.k.

Kushamiri kwa biashara ya madawa ya kulevya

Kushuka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania
 
Sasa hapo uongozi ulikuwa wapi na madudu yote hayo
 
Tanzania haijawai kuwa na awamu ya nne
Kwa kweli lazima tujipe pongezi watanzania, kwa kiasi fulani tuliishi kwa amani wakati nchi iko ktk autopilot. Miaka takriban 10, tatizo la mkwere ni ushosti na uanadiplomasia uliopitiliza!
 
Hahahahahahahaa 10years auto pilot
 
alisema anataka kutengeneza tanzania ya matajiri kwani mmesahau tena hayo sio majipu ni hali ya kawaida
 
KWELI Nchi Imeoza, Kuanzia Mifumo, Viongozi, Watendaji, Chama Kinachotawala Na Watunga Sera Wake!!! KWANI Miaka 39 Yote Si Hao Hao CCM, Ndio Wanaounda SERIKALI INAYOONGOZA Hiyo Nchi Ambayo Unasema /Mnasema Imeoza!!! JE, Walishindwa Vp KUONDOA Huo UOZO Walionao!!!??
 
Back
Top Bottom