Nchi iko katika maombolezo, huku soka, harusi, sherehe na burudani zinaendelea, sasa kwanini kumpokea Lissu ndio iwe tatizo?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,013
144,371
Na sio hayo tu, hata upigaji wa kura za maoni kweny vyama vya siasa unaendelea. Sasa kwanini watu kwenda kumpokea mgeni/kiongozi wao ndio iwe tatizo?

Ni wapi CHADEMA wamesema wataandamana?

Kukutana airport huku kila mtu akitokea nyumbani Kwake, ndio kuandamana au ndio kufanya mkusanyiko usio halalai?

Kama ni hivyo, wanaokusanyika katika sehemu zingine kama viwanjani, kwenye makongamano au mikutano,nao wanavunja sheria?

Hivi nchi hii imeundwa leo au jana kiasi kwamba bado hatuzijui vizuri sheria za nchi na katiba ya nchi hii mpya?

Kwa maneno mengine,tunaishi katika nchi mpya ikiwa na watu wapya katika uongozi wa taaaisi mbalimbali za nchi na ndio maana tunaonekana kukosea/kujichanganya?
 
Ni maombolezo FAKE Mkuu. Nakumbuka Maombolezo ya Mwalimu starehe zote Nchini zilifungwa. Kwanini maombolezo haya ni tofauti? KULIKONI?

Je, Mkapa kwa kumpinga yesu wa lugola kuongeza muda baada ya miaka 10 na kuitaka Tume Huru ya Uchaguzi alionekana ni pingamizi la maccm hivyo kupewa sumu kama Mangula aliyekataa Membe kufukuzwa chamani?
 
Mkuu mambo mazito hayo kumbe kapewa sumu?
 
Ni maombolezo FAKE Mkuu. Nakumbuka Maombolezo ya Mwalimu starehe zote Nchini zilifungwa. Kwanini maombolezo haya ni tofauti? KULIKONI?

Je, Mkapa kwa kumpinga yesu wa lugola kuongeza muda baada ya miaka 10 na kuitaka Tume Huru ya Uchaguzi alionekana ni pingamizi la maccm hivyo kupewa sumu kama Mangula aliyekataa Membe kufukuzwa chamani?
Alafu kifo kilivyotangazwa usiku ule,nawaza tu.

Anyway,labda walikuwa wanafuatulia hali yake kwa karibu.

Na mpaka kufikia leo hii,hivi wamesema kafariki kwa ugonjwa gaini?
 
Hakika ninyi si chama cha siasa ila chama cha shari mithili ya uhuni.

Mikusanyiko uliyoitaja ni tofauti sana na mlichopanga na kutegemea kutokana na ujio wa Lissu. Kauli na maandalizi yanaashiria uvunjifu wa amani wa amani.

Mjitafakari la hamtaeleweka iwapoJeshi la Polisi litalazimika kutumia nguvu kuzuia uvunjifu wa amani
 
Nimesikiliza vituo vya redio na baadhi ya TV, naona muziki ni kama kawaida. Nyimbo za maomboleza hakuna kabisa. Hiyo kuzuia Tundu Lisu kupokelewa na watu ni wivu tu wa kisiasa. Wanajua fika Lissu atavuta umati wa watu, na kuanza kupandisha hamasa ya watu.
 
Hakika ninyi si chama cha siasa ila chama cha shari mithili ya uhuni.

Mikusanyiko uliyoitaja ni tofauti sana na mlichopanga na kutegemea kutokana na ujio wa Lissu. Kauli na maandalizi yanaashiria uvunjifu wa amani wa amani.

Mjitafakari la hamtaeleweka iwapoJeshi la Polisi litalazimika kutumia nguvu kuzuia uvunjifu wa amani
Sometimes ni bora kukaa kinyaaa!
 
Hamna kuandamana wala kukusanyika hasa eapoti. Imeshasemwa hivyo, mtaandamana humu jf panatosha!
Ole wenu sasa..
 
Hakika ninyi si chama cha siasa ila chama cha shari mithili ya uhuni.

Mikusanyiko uliyoitaja ni tofauti sana na mlichopanga na kutegemea kutokana na ujio wa Lissu. Kauli na maandalizi yanaashiria uvunjifu wa amani wa amani.

Mjitafakari la hamtaeleweka iwapoJeshi la Polisi litalazimika kutumia nguvu kuzuia uvunjifu wa amani

Hiyo ni hali ya kawaida sana, chama kikizeeka hukosa mvuto, na hutumia mabavu ya vyombo vya dola kuendelea kukubalika. Na wanapoona chama chochote kinakubalika hukifanyia mizengwe ili kisiendelee kuvuta wananchi. Haya yanayofanyika dhidi ya cdm kwa kutumia vyombo vya dola sio mageni, bali ni kwakuwa chama kikongwe hakina jinsi zaidi ya kujilinda kwa kutegemea vyombo vya dola.
 
Sometimes ni bora kukaa kinyaaa!
Siwezi kukaa kimya ninaposoma upuuzi. Ujio wa Lissu wewe na familia yako unaokuongezea nini? Ujio wa Lissu kuhamsisha watu wasio na hatia ikatoea vurugu wakaumizwa, wewe mhamasiahaji unafaidika nini? Kifo cha Akwilina hakijawapa funzo? Siasa za kitoto hizo.
 
Back
Top Bottom