Goliath mfalamagoha
JF-Expert Member
- Aug 3, 2012
- 602
- 2,505
Serikali iache dharau na dhihaka kwa Watanzania, Usanii uishie 2016, huku 2017 tunataka kazi sio siasa za umeme na kumkwamisha rais wetu kipenzi Dokita John Pombe Magufuli tuliyemchagua wenyewe.
Waziri Muhongo anatufanya Watanzania ni wajinga kiasi hiki?? Ewura na TANESCO ni taasisi zilizochini yake, chochote hakiwezi kufanywa bila kupita kwake... Maombi ya Tanesco kupandisha gharama za umeme sio ya jana wala juzi, ni nusu mwaka sasa maombi yalikuwa mezani yakifanyiwa mchakato, Wamekubaliana wamepandisha, kisha asubuhi anaibuka kwenye vyombo vya habari kujikanusha...
Mwaka 2017 uwe mwaka wa mabadiliko na kufanya kazi sio siasa za majitaka na kutafuta huruma ya umma huku mkiliumiza na kutweza taifa. Ni muhongo huyu huyu mwenye historia mbaya ya ESCROW na akalidanganya bunge uso kwa macho, kisha akajiuzuru na kurejea kwa mlango wa mwingine, leo tena anatudanganya Watanzania kwamba amezuia ongezeko la bei ya umeme ilihali kimantiki yeye mwenyewe ndiye alipandisha...
Ole wenu muishio kwa hiyana ya ujinga wetu...