Nchi hii tunahitaji mabadiliko makubwa kwenye mfumo wa utoaji haki. Mwananchi anaweza kupelekwa mahabusu wakati wowote Mamlaka ikitaka

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,489
40,999
Nchi hii tunahitaji mabadiliko makubwa kwenye mfumo wa utoaji haki. Mwananchi anaweza kupelekwa mahabusu wakati wowote, wenye mamlaka wakitaka, bila ya kujali una kosa au huna kosa.

Niliwahi kuhudhuria kikao kimoja kilichokuwa kikiendeshwa na Mkuu wa Wilaya. Wakati akitoa maagizo yaliyoonekana wananchi hawakuyapenda, wananchi wakaanza kuguna, na kijana mmoja akanyosha mkono, kutaka kuuliza swali.

Mkuu wa Wilaya hakufurahi, akaanza kufoka, 'mimi siyo mtu wa kunyoshewa mkono wakati nahutubia. Wewe unajifanya mjanja sana eeh? Pale ofisini pangu nina marehemu wengi ambao waliowaua hawajulikani. Nikikupa wewe marehemu mmoja, hakika nakuambia, hutoki ndani kabla ya miaka mitatu. DC siyo mtu wa kuchezewachezewa kama unavyofikiria. Ninyi vijana ni wajinga. Nikitaka unaozea jela wewe". Baadhi ya wananchi wakaanza kucheka. Hakikuwa kichekesho. Lakini kauli ile ilipeleka ujumbe mzito, kuwa kutokana na mfumo wetu mbovu wa sheria, mwananchi unaweza kupelekwa mahabusu bila ya kuwa na kosa lolote.

Nakumbuka kisa kingine, wakati wa kampeni za uchaguzi, mwananchi mmoja alikataa tangazo la kampeni la marehemu kuwekwa kwenye nyumba yake. Jioni alikamatwa, akaswekwa mahabusu. Siku ya tatu alipelekwa mahakamani kwa kosa la ujambaz wa kutumia silaha.

Mwananchi wa Tanzania, haki yake ipo kwa kudra za watawala na Polisi. Leo hii, Polisi asiye na maadili, unaweza kushindwa kuelewana naye kwa mambo ya kawaida, na kesho ukaja kuchukuliwa mzobemzobe kupelekwa mahabusu, usijue ni kwa kosa gani, siku inayofuata ukapelekwa mahakamani, ukashangazwa na msululu wa mashtaka. Unaweza kuja kutoka baadaye, lakini baada ya kuteseka mahabusu.

Kama tunataka wananchi tuishi kwa uhuru, na haki zetu kulindwa, mfumo wetu wa utoaji haki ni lazima ubadilike. Tumeona jinsi awamu ya 5 ilivyotumia vibaya kasoro za mfumo wetu wa utoaji haki, katika kufanya uonevu wa hali ya juu kwa watu wasio na hatia. Tusikubali haya yaendelee.
 
We Nassari hamia CCM vinginevyo tutakupa kesi ya uhujumu uchumi. Kwani unapata shida gani kuunga juhudi na UDAS utapewa? Akisikika mtendaji mmoja wa DPP ya mwenda zake.
 
Aisee ndiyo maana tunataka kaiiba mpya itakayolinda haki za watu, kuondoa vyeo feki kama ukuu wa wilaya na kupunguza madaraka ya rais na pia kuzipa nguvu taasisi zaidi kuliko kulimbikiza madaraka katika baadhi ya vyeo
Katiba mpya itatoa wigo na mipaka ya madaraka lakini pia checks and balancing. Isije ikawa mhuni mmoja tu kisa anata demu wako anakupa kesi ya ugaidi.j
 
Mimi napata shida Sana kuwaelewa Hawa viongozi wetu.Hivi kiongozi mkubwa let say DC ,unashindwa kuwa na hekima na busara za kutambua hiki sahihi kuongea hiki si sahihi kweli?

Unawabwatukia binaadamu wenzio Kama wewe ni immortality you never die.Watawala wenye hekima kibongobongo wanaojielewa ni tunu Sana na nadra kuwapata.wengi wanamihemko ya ufahari na kuwatunishia misuri wananchi wanaoongozwa.

Uongozi pia ni kalama kweli ,pia ni spirit ambayo mtu lazima uji sacrifice kwa ajili ya kuwapa huduma Bora unaowaongoza.sasa tz mwananchi anamuogopa kiongozi ,Sasa izo kero zake atamwambia Nani?
 
Hamnazo hakua mtu
JamiiForums-490856356.jpg
 
Mimi napata shida Sana kuwaelewa Hawa viongozi wetu.Hivi kiongozi mkubwa let say DC ,unashindwa kuwa na hekima na busara za kutambua hiki sahihi kuongea hiki si sahihi kweli?

Unawabwatukia binaadamu wenzio Kama wewe ni immortality you never die.Watawala wenye hekima kibongobongo wanaojielewa ni tunu Sana na nadra kuwapata.wengi wanamihemko ya ufahari na kuwatunishia misuri wananchi wanaoongozwa.

Uongozi pia ni kalama kweli ,pia ni spirit ambayo mtu lazima uji sacrifice kwa ajili ya kuwapa huduma Bora unaowaongoza.sasa tz mwananchi anamuogopa kiongozi ,Sasa izo kero zake atamwambia Nani?
Mtu akipewa uDC anajiona mwenye akili kuliko wote ndani ya wilaya.
 
Bila kunyang'anya nguvu za kuamrisha polisi walizo nazo wanasiasa watu wengi wataendelea kuteswa na "politically motivated prosecutions"
 
Back
Top Bottom