Nchi hii inataka Rais dikteta na mtenda haki

koryo

JF-Expert Member
Jun 21, 2010
639
278
Jana nimesikia hotuba ya Rais Magufuli Rais wa awamu ya tano na ninampongeza sana kwa hotuba nzuri iliyojaa UKWELI MTUPU.

Nchi hii ilipofikia inataka Rais DIKTETA NA MTENDA HAKI kama Rais Magufuli.

Nchi hii iipofikia iikuwa kama shamba la bibi ambapo kila mtu analichezea kama anavyotaka.

Inakuwaje mtu anapata mshahara wa Tshs.35,000,000 na mwingine anapata Tshs.310,000 kwa mwezi wakati mahitaji yao ni sawasawa.

Mhe.Magufuli alikuwa tu muungwana lakini matatizo haya yameletwa na Serikali ya awamu ya nne.

Wanatakiwa WAWAJIBISHWE.
 
HAKI wewe unaitafsiri vipi, lakini pia UDIKTETA kwako una maana gani?
Unasema tunahitaji Rais DIKTETA pia wakati huo huo MTENDA HAKI.
Sifahamu kama kuna kiongozi duniani aliyenyooshewa mkono kwa UDIKTETA na wakati huo huo alisifiwa kwa kutoa HAKI kwa wananchi wake.
 
Rais kazi anayo tena kubwa ya kuweka system ifanye kazi nchi nzima kama yeye anavyotaka na sii huu utawala wa hadi yeye awe eneo husika ndiyo kazi ama majipu yatumbuliwe hii nchi iko na mikoa mingi mno...Akitumbua majibu Dar nani atatumbua majipu yaliyopo Moshi kule holili na akienda Holili Moshi kutumbua nani atakuwa Tabora kutumbua...Atachokea njian asipo-implement system iwe inafanya kazi nchi nzima..
 
Back
Top Bottom