Nchi hii haina upinzani wa kweli

The golden

JF-Expert Member
Sep 11, 2018
1,381
2,553
Leo nimeamua tujadili hili swala.

Kuna watu , akiwemo Pasko Mayala wanapenda kusema , hapa kwetu hakuna upinzani wa kweli. Wapinzani hawana hoja kabisa.

Naomba kuuliza maswali yafuatayo ili nielewe vizuri.

1. Upinzani wa kweli ni upi? naomba features za upinzani wa kweli. Ikiwezekana toa mifano nchi zenye upinzani wa kweli na namna wanavyofanya siasa zao.

2. Wanasema upinzani hauna hoja za maana. Hoja za maana ni zipi? ,toa mifano kwenye maelezo yako.

3. wanaosema kuwa hapa kwetu hakuna upinzani wa kweli, kwa nini wao wasiwe wapinzani halafu waufanye huo upinzani wa kweli?

Karibuni kwa mjadala.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Upinzani uliopo uliasisiwa kwa huruma ya Mwalimu Nyerere na si kwamba kuna watu jasiri waliupigania.....ndio maana unaitwa Upinzani " Kanyaboya"
 
Unasema? ,hebu fafanua.

Sent using Jamii Forums mobile app

Hata katika mchakato wa kuanzisha mfumo wa vyama vingi, wananchi walio wengi walichagua kuendelea na chama kimoja.... Nyerere kwa shinikizo la mabeberu alilazimisha ili kukidhi masharti ya misaada.

Hivyo uliundwa upinzani uchwara ili tu kuwazuga mabeberu, tazama waasisi wa upinzani utagundua wote walio hai leo wana vinasaba vya chama tawala... changanya na zako mbayuwayu.
 
Du! ,Watanzania wengi ndio maana kunafeli mitihani , yaani hili ndilo jibu la maswali ya hapo juu. Hebu soma tena uelewe hayo maswali.
Hata katika mchakato wa kuanzisha mfumo wa vyama vingi, wananchi walio wengi walichagua kuendelea na chama kimoja.... Nyerere kwa shinikizo la mabeberu alilazimisha ili kukidhi masharti ya misaada.

Hivyo uliundwa upinzani uchwara ili tu kuwazuga mabeberu, tazama waasisi wa upinzani utagundua wote walio hai leo wana vinasaba vya chama tawala... changanya na zako mbayuwayu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu , naomba unipe elimu ya kutosha upinzani wa kweli ni upi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Upinzani wa kweli ni ule unaopiganiwa kutokea chini na watu wenye ujasiri wa kile kinachopiganiwa.

Tanzania ilikuwa na wapinzani wa kweli kutokea miaka ya Uhuru kama akina Rip Mapalala, Kasanga Tumbo nk so ili kuwadhibiti ndio ukaasisiwa huu upinzani mamboleo wa akina Mtei, Marando nk

Unajua Nyerere alibarikiwa kuwa na akili sana!
 
Du!
Upinzani wa kweli ni ule unaopiganiwa kutokea chini na watu wenye ujasiri wa kile kinachopiganiwa.

Tanzania ilikuwa na wapinzani wa kweli kutokea miaka ya Uhuru kama akina Rip Mapalala, Kasanga Tumbo nk so ili kuwadhibiti ndio ukaasisiwa huu upinzani mamboleo wa akina Mtei, Marando nk

Unajua Nyerere alibarikuwa kuwa na akili sana!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli mpaka sasa upinzani bado. Mpaka kije kizazi chenye maono mapya ya kisiasa na kiuchumi:
Hatuna upinzani wa kweli?
I. Mpinzani wa kweli Hana Bei. Atafia itikadi za chama na Wananchi wake. Hapa wapinzani wetu wamefeli sana
II. Huu utitili wa vyama vya upinzani vinaua nguvu ya upinzani.
III. Mpinzani wa kweli sio hama hama. Naona wapinzani pia wanapokeana, hatari sana
IV. Hatuna Sera ya kitaifa inayo ongoza upinzani, Chadema wanataka federation wengine wanataka republic, hii pia si njema
V. Wapinzani hawana umoja. Wengine wamefanikiwa kufika hapo walipo kwa kusaliti wenzao katika upinzani.
Kwa ujumla bado sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
I
Leo nimeamua tujadili hili swala.

Kuna watu , akiwemo Pasko Mayala wanapenda kusema , hapa kwetu hakuna upinzani wa kweli. Wapinzani hawana hoja kabisa.

Naomba kuuliza maswali yafuatayo ili nielewe vizuri.

1. Upinzani wa kweli ni upi? naomba features za upinzani wa kweli. Ikiwezekana toa mifano nchi zenye upinzani wa kweli na namna wanavyofanya siasa zao.

2. Wanasema upinzani hauna hoja za maana. Hoja za maana ni zipi? ,toa mifano kwenye maelezo yako.

3. wanaosema kuwa hapa kwetu hakuna upinzani wa kweli, kwa nini wao wasiwe wapinzani halafu waufanye huo upinzani wa kweli?

Karibuni kwa mjadala.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata Nccr Mageuzi chama cha udugu na uzalendo?
 
Hawa kupinga kila kitu wanajua ndo upinzani....Hawajifunzi hata kwa wapinzani wa kipindi hiki,Dems,wanavyoendesha mambo yao.
 
siasa hatuijui kuanzia wananchi mpaka hao wanasiasa wenyewe.
hata mpinzani hajui upinzani wake unasimamia nini.
ukiwa mpinzani alafu ukajitoa wazi kushiriki shughuli yeyote ya maendeleo iliyo asisiwa na chama kinachotawala unaitwa msaliti pia hivyo hivyo chama tawa ku suport jambo ama ushauri uliotolewa na upinzani ni kosa kubwa ndani chama.

moja kati ya mambo meengi ya kuweka sawa hili jambo ni elimu ya siasa.
lkn pia uchaguzi wowote ule ni lazima mshindi apatikane kwa asilimia na sio idadi ya kura.

Upinzani wa kweli upo,utaendelea kuwepo.
1.CUF ya Maalim Seif alivyoweza kumdhibiti Commando Amour.kwa kumshinda bila kificho katika uchaguzi mkuu japo CCM ilinyakuwa madaraka kwa nguvu.
2.Mchungaji Mtikila alivyoiburuza serikali kwenye mahakama na kuishinda mara nyingi kwenye maswala ya katiba.
3.Profesa Mbilinyi alivyotema uwaziri wa fedha baada ya vyama vya upinzani kugunduwa na kuanika madudu katika vibali vya kuangiza mafuta ya kula.
4.Waziri Iddi Simba Alivyofukuzwa uwaziri wa Viwanda baada ya vyama vya upinzani kugundua kashfa katika uagizaji wa sukari.
5.EPA
6.ESCROW
Tuseme tu katika upinzani kuna misuguano kama huko CCM.
Jenerali Ulimwengu aliposema katika hatua ya kujenga demokrasia tumerudi nyuma miaka 50,wa kulaumiwa sio upinzani bali Magufuli anaezika upinzani bila aibu wala sababu.
 
Back
Top Bottom