Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Kwahiyo tulianza uchambuzi wa kina kwelikweli, mmepitia kwenye mlolongo mingi kweli kweli, vyombo mbalimbali vimehusika,
Lengo lilikuwa moja tu; natak kujenga Tanzania ya aina gani? na Je, nichague watu wa aina gani watakaoifikisha hiyo Tanzania ninayoitaka, na ndiyo maana process (mchakato) ilikuwa ndefu."
Maneno hayo aliyazungumza Mhe. John Pombe Magufuli, Rais wa Tanzania, aliyazungumza kwenye hafla ya kuwaapisha wakurugenzi wapya aliowateua yeye mwenyewe.
Watanzania tunajifunza kwamba, mchakato wote huo na milolongo yote hiyo waliyoipitia hata kupatikana hao wa kurugenzi, ni kubaini yupi ni chama gani, yupi ni CHADEMA, yupi ni CUF, yupi ni ACT au NCCR-Mageuzi, maana imeonekana wazi kabisa kuwa uteuzi huo ulizingatia zaidi itikadi ya chama cha siasa, yaani sifa ya kwanza ni kuwa mwanachama wa chama cha mapinduzi CCM, haijalishi uzoefu wa kazi au elimu mtu aliyonayo.
Bado imewasikitisha watanzania wengi juu ya aliyekuwa mwanachama wa CCM na baadaye kuhamia ACT, Hidaya Usanga, alipoteuliwa kuwa mkurugenzi mtendaji wilaya ya mji wa Tarime, na baada tu ya kubainika kuwa ni mwanachama wa chama cha ACT, uteuzi wake ukatenguliwa mara moja.
Kwa mujibu wa TAARIFA YA ULIMWENGU JUU YA HAKI ZA BINADAMU, Kifungu cha 21. Inatamkwa kwamba:
1. Kila mmoja anayo haki ya kushiriki katika Serikali ya nchi yake yeye mwenyewe binafsi au kwa njia ya mjumbe aliemchagua kwa hiari yake.
2. Kila mmoja anayo haki sawa ya kufanya kazi katika Serikali; matakwa hayo huonyeshwa katika uchaguzi halisi unaofanywa muda baada ya muda ambao kila mtu hupiga kura na ambao hufanywa kwa kura ya siri na kila mtu kwa hiari yake.
3. Matakwa ya watu ndiyo yatakuwa msingi wa utawala wa serikali; hali hii itajidhihirisha kwenye chaguzi za haki kwa watu wote na ambazo zinafanyika kwa siri au namna nyingine ambayo itahakikisha uchagazi kuwa huru.
Unaposema kusimamia sheria, ni sheria zipi unazozisimamia? Unasema unamtanguliza Mungu, mbona kwa haya unatanguliza Itikadi ya chama cha siasa?
Pia, unasema Tanzania unayoitaka, Je; ndiyo Tanzania wanayoitaka watanzania wote? labda hukufahamu hili awali, naomba kukufahamisha: CHADEMA/UKAWA tunaposema People's Power, yaani Nguvu ya Umma, tunamaanisha kuwa Umma wa watanzania ndiyo wenye mamlaka, Umma ndiyo unaoamua nchi iweje, iongozwe namna gani, na masuala yote yahusuyo nchi, na sio mtu mmoja aamue. (Rejea Kifungu cha 21 kifungu kidogo cha 3 cha Taarifa ya Ulimwengu ya Haki za Binadamu hapo juu.)
Nchi haiwezi kupiga hatua kama ubaguzi wa kiitikadi unaonekana wazi kutokea mamlaka ya juu ya nchi, nchi hii ni ya Watanzania wote, hakuna mtu wala kikundi cha watu, wenye hati miliki ya nchi hii.