Nchi haina wazee wanaoshauri?

MFIZIGO

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
374
232
Nasema tena nchi hii kuna uwezekano mkubwa haina wazee au ambao waliopo hawaelewi majukumu yao. Katika nchi au eneo lenye wazee mambo huwa hayaaribiki, hata yakiharibika huwa ni kwa muda tu.

Sasa ona hapa kwetu wazee wao wameamua kuwa kimya, nao wamekuwa waoga kama sisi vijana ambao hatujui lolote, wao ndiyo waliokuwa wakemeaji wa mambo haya yanayokwenda mrama sasa.

Au huenda wazee hawajapendezwa na suala la huyu mkuu wa kaya mpya? Kwa hiyo wanaona bora aharibu tu. Kweli katika nchi yenye wazee, uvunjwaji wa katiba unakaliwa kimya kiasi hiki?

Kweli katika nchi yenye wazee, watu wa nchi hiyo wanaishi huku hawaijui kesho yao? Kweli katika nchi yenye wazee, kila mtu ni mchochezi madamu tu unamkosoa 'sizonje'? Ona sasa wazee! Wawekezaji wanakimbia kwa sababu ya misimamo ya hovyo ya 'Sizonje' na hili nalo mmelikalia kimya?

Mnasubiri mpaka atangaze kukiuza chama chenu ndiyo muibuke mlipo na misuli yenu viunoni? Sisi vijana tunashindwa kumshauri kwa kuwa 'hatujui kitu', nyinyi mnajua kwa kuwa mlishapita huko aliko Sizonje.

Tusaidieni kuinusuru.
 
1. Yule mzee mwenye kidoti kidevuni mlimchapa makofi
2. Yule aliyewahi kuwa katibu wa chama chenu na mkuu wa mkoa wa Dar, mwanae mmemnyima uwaziri mkuu
3. Yule mzee wa msoga, mlimsimanga sana kipindi cha uongozi wake, hivyo anataka muisome, kwanza yeye mwenyewe anamuogopa Sizonje
4. Wazee wote wa Zanzibar wapo bize kuijenga nchi yao changa, kwani yanayoendelea huku wao hayawahusu hata robo chembe.
5. Mzee 'ruksa' kama lilivyo jina lake maana yake kesharuhusu haya kutokea.
6. Mzee 'asiye na dini' kwa sasa yupo huku kwetu na ana hamu kweli Sizonje akosee
 
Desmond Tutu wa kibongo wote majoga.... wakati wameisha zeeka lakini hawapo tayari kusema ili kunyoosha mambo mpaka wanatia hasira... ubinafsi umewajaa ......
 
Has many advisors but when they meet him....is him who advise them....
 
Back
Top Bottom