Nchi haina Kiongozi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nchi haina Kiongozi?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Zamazamani, Apr 21, 2009.

 1. Z

  Zamazamani JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2009
  Joined: Jun 13, 2008
  Messages: 1,624
  Likes Received: 339
  Trophy Points: 180
  Ndugu zanguni kuna mambo mengi kuhusu uwekezaji katika nchi hii yananitatiza sana an kunikatisha tamaa kabisa .Hapo nyuma nilikuwa nasikia tu stories kuwa wawekezaji (hasa wale ukweli) wengi wao wanakuwa very dissapointed na utaratibu uliopo hapa nchini......siyo rahisi kabisa kwa mtu aweze kuwekeza hapa.,mara nyingi mwisho wanaamua kuondoka....sasa nimeyashuhudia mwenyewe....Kuna jamaa zangu ambao wapo very serious wamekuja kuwekeza hapa nchini.....lakini nimezunguka nao sehemu zote husika bila ya mafanikio...ni kwamba hakuna mtu wa kutoa maamuzi yeyote huko serikalini....kwa mfano hawa jamaa zangu walikuwa interested na kutoa msaada (siyo mkopo) wa kujenga soko la kisasa la samaki pale bagamoyo...jamaa wame spend two months bila responses yeyote toka wizara husika...na wala TIC (extremely hopeless) hawaonekani kustuka ingawa information zote wanazo.....ishu nyingine iliyoshindikana ni nyanja ya kilimo cha kisasa....jamaa walijipanga kuja kutoa misaada mikuwa sana ya pembejeo za kilimo ili kusaidia hasa wakulima wadogowadogo...lakini Tumekwama kabisa siyo wizara husika wala TIC ambao wameweza kutusaidia...sasa mimi najiuliza hawa viongozi wetu wakuu wanavyopiga kelele juu ya kuwahimiza wawekezaji kuja hapa ina maana haya hawayajui?????...kuna kitu hapa sielewi kabisa..inanitia uchungu sababu nimejaribu kuwabembeleza wavute subira lakini nimechemsha ...kweli nchi yetu ni ya kipumbavu namna hii????!!!!!SASA TUNAFANYAJE since things are not moving at all????
   
 2. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Si juzi tu JK alikuwa Saudia 'kuiuza nchi'?
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Sijaelewa hasa wanawekeza au wanasaidia.Kama ni kusaidia watafute NGOs ( hasa za kimataifa zenye kushughulika na kilimo au uvuvi na kwa pamoja wakishirikiana na local NGOs wanaweza kuingia pasipoingilika.Unless ukute nao hawana haja ya kweli ya kusaidia - ukute ni wawekezaji wenye kutaka faida na imeshahisiwa kuwa wana ajenda ya siri ndiyo maana hakuna uamuzi unatolewa so far!
   
 4. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #4
  Apr 21, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  JK aliahidi kuanzisha INVESTORS COMPLAINTS BUREAU under state house supervision...

  sasa sijui mkulu kila kitu anaongea tuu ili mradi au?? hii labda ingewasaidia wenye malalamiko kusikikaa zaidi..
   
 5. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #5
  Apr 21, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  miujiza miujiza miujiza
  tanzania ni miujiza kantri
   
 6. D

  Dandaj Member

  #6
  Apr 21, 2009
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nafikiri hao jamaa hawakupasa kulalamika kama mtu wanayetaka kumsaidia hataki. Na hao waliokataa kupokea hiyo misaada wanajua madhala ya misaada ndio maana hawajaikimbilia.
   
 7. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #7
  Apr 21, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  kwa hiyo misaada ya wasaudia haina madhara ndo wanaikimbilia????
   
 8. Z

  Zamazamani JF-Expert Member

  #8
  Apr 21, 2009
  Joined: Jun 13, 2008
  Messages: 1,624
  Likes Received: 339
  Trophy Points: 180
  pamoja na hayo yote...nafikiri kuna tatizo kubwa kwenye kutoa maamuzi ,hususan kwenye serikali hii.....kama hawataki misaada...si waseme tu black and white.....mi ninachokiona ni kwamba kila mtu anamtegeshea mwenzie....hakuna wa kumfunga paka kengele....labda mtu akija na ajenda ya kusaidia kampeni kama Saudia itakuwa kidogo rahisi.......
   
 9. Mpendanchi-2

  Mpendanchi-2 JF-Expert Member

  #9
  Apr 21, 2009
  Joined: Apr 4, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Sometimes tunaweza kuwa tuna toa lawama kwa serikali bila kujua undani, the so called wawekezaji wapo wa aina nyingi sana, wapo mataperi wanaotafuta project na kwenda kuuza, wapo wanaotafuta gear ya kuingia na kupata ardhi n.k . Hivyo vyombo vya serikali wakati mwingine vinakuwa vimeyagundua hayo ndiyo maana wanazungushwa.
   
 10. H

  Haika JF-Expert Member

  #10
  Apr 21, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  je wewe unajua utaratibu wa wawekezaji hapa tanzania?
  je wao wanaujua?
  je wanae local shareholder?
  wameconsult investor mwingine ambaye ameshaanza operations wajue alivyofanya?

  Waambie watoe matongotongo huku sio porini
   
 11. S

  Shelute Mamu Member

  #11
  Apr 22, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa Serikali iliyo makini inakuwa wazi kumweleza mtu nini kinachotakiwa (Masharti ya muwekezaji) jawabu siyo kumzungusha mtu kama taratibu ziko wazi. Kwa nini azungushwe huo si uungwana hata kidogo na kunaonyesha kutujiamiani!!!!

  Baba wa Taifa ndiyo maana anakumbukwa maana yeye alikuwa muwazi kama ndiyo ni ndiyo na hapana ni hapana BASI haina mjadala na mtu anaelewa. Tabia hii ya kuzungusha watu ndiyo inaathiri hata watu waliostaafu, malamiko ya walioonewa kazini, malipo wa EAC n.k.
   
 12. Z

  Zamazamani JF-Expert Member

  #12
  Apr 22, 2009
  Joined: Jun 13, 2008
  Messages: 1,624
  Likes Received: 339
  Trophy Points: 180
  Shelute Mamu
  Nakupa 5!!!! kama nchi ina serikali na ina taasisi zinazoshughulika na mambo ya uwekezaji na vitu kama hivyo.....kwa nini wasitoe mwongozo badala ya kuanza kukimbia kimbia kama watoto????watu kama TIC wanafanya kitu gani???Hawa wapuuzi walitakiwa kuwa na info zote za uwekezaji at one stop point....lakini nenda pale uulize hata kipaumbele cha nchi hii ktk uwekezaji...utazungushwa mpaka ujute kuwafahamu!!!
  Hawa jamaa zangu siyo matapeli..sababu tuna projects nyingine ambazo ni productive kule Ghana.......ni stori ndefu anyway...
  Mnachekesha sana yaani nchi hii iwe na uadilifu wa kuangalia eti kama project ina madhara???labda hatupo pamoja ..mnaota...
  Kuhusu taratibu za kufungua kampuni ,local shareholders nk kila kitu tunakifahamu ....ILA MOST OF THESE PLACES WANATAKA RUSHWA...NA JAMAA WAMEGOMA KUTOA RUSHWA NDIPO MATATIZO YALIPOANZIA!!!!
   
 13. Z

  Zamazamani JF-Expert Member

  #13
  Apr 22, 2009
  Joined: Jun 13, 2008
  Messages: 1,624
  Likes Received: 339
  Trophy Points: 180
  Sasa huu ndio upumbavu, ujinga na upuuzi.......kwanza hawa jamaa nawajua vizuri ni more than just wawekezaji....we have other projects in other countries....
  Halafu kama nchi ina miongozo kwanini wasituelekeze nini cha kufanya au kama hawaitaji misaada/uwekezaji kama huu??? kwani ni lazima kuwekeza ktk nchi hii???? Hawa jamaa nimekuwa nikiwa convince kwa muda mrefu waje hapa kuwekeza ili ndugu zetu wapate ajira nk.....lakini imekuwa night mare...kuna harufu ya rushwa kila sehemu...hawa jamaa wamegoma kutoa hiyo rushwa!!!ndio tatizo
   
 14. Z

  Zamazamani JF-Expert Member

  #14
  Apr 22, 2009
  Joined: Jun 13, 2008
  Messages: 1,624
  Likes Received: 339
  Trophy Points: 180
  Huu ndiyo upumbavu wenyewe..........ndio maana kuna vyombo husika ....au kazi yao ni kukata viuno tuu na kula hela ya walipa kodi???? kazi ya chombo kama TIC nk ni nini??
  Kwa nini umtafute investor aliyetangulia??ishu za local share holder nk na taratibu zote tunazijua na wanatukwamisha vilevile!!!!
   
 15. Z

  Zamazamani JF-Expert Member

  #15
  Apr 22, 2009
  Joined: Jun 13, 2008
  Messages: 1,624
  Likes Received: 339
  Trophy Points: 180
  Huu ndiyo upumbavu wenyewe..........ndio maana kuna vyombo husika ....au kazi yao ni kukata viuno tuu na kula hela ya walipa kodi???? kazi ya chombo kama TIC nk ni nini??
  Kwa nini umtafute investor aliyetangulia??ishu za local share holder nk na taratibu zote tunazijua na wanatukwamisha vilevile!!!!
  wewe ndiyo utoe tongotongo kwanza........
   
 16. N

  Nsaji Mpoki JF-Expert Member

  #16
  May 1, 2009
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 396
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mie narudi kwenye mada inayosema 'Nchi haina viongozi''. Naiona ni mada nzuri yenye mwelekeo wa kujenga taifa letu. kutokana na hilo mie nitaendeleza mjadala wa namna tunavyoshindwa kutumia fedha za ndani katika kuwezesha ukuaji wa uchumi. Katika hili nitarudi tena kwenye fikra za Pinda za kutaka kuiwezesha tanzania kuwa ghala la chakula na kuwa na uwezo mkubwa wa kiuchumi. Hta jana ijumaa wakati akiulizwa maswali na wabunge alirejea hili. Wana JF. Kwa wiki mbili zilizopita nilibahatika kushuhudia uwasilishaji wa bajeti za Mikoa na halmashauri za wilaya. Nimepitia baadhi hakuna kitu. kwanza ile ceiling yenyewe waliyopewa haiwezi kabisa kufanya lolote. Bado asilimia 80 ya bajeti yote ya nchi imeachwa wizarani kwa ajili ya mikutano, warsha na kongamano. Kingine nilichokiona ni upotevu mkubwa wa pesa za serikali. Niwape mfano halisi.Mkoa mmoja tu. Sitaki kuutaja ulikuja na watu 100 ina wamekaa DSM kwa siku 20 ikiwa na maana kuwa kila mmoja lilipwa Tshs 80,000 kwa siku. Nikapiga hesabu kwa wastaniu wa namba hiyo hiyo ya watu kwa mikoa 21 ukichanganya gharama mza mafuta(wastani wa gari nne kila naneKila Mkoa), posho, fedha za dharura na stationery/printing unapata jumla ya Tshs. 34,069,140,000/= kwa kazi ambayo kama ungekuwa na mawasiliano mazuri ya mtandao kusingekuwa na gharama ya kiasi hiki. Bilioni 34 ni fedha nyingi. Wenzangu mtanambia unaweza kujenga zahanati ngapi. Kilichonishtua zaidi ni ile siku ambapo mabomu yalilipuka mbagala. Vijana wa HAZINA wakaitangazia mikoa na halmashauri kuwa Bbudget codes zimebadiilka hivyo wanatakiwa kuanza kuandaa upaya bajeti zao. Walilijua hili mapema lakini hawakusema. Hali hii imesababisha watumishi walioishi DSM kwa siku 20 sasa waongeze siku nyingine. Sijui itakuwa hadi lini na nani atalipia gharama hizo za watu kukaa DSM kwa uzembe wa HAZINA. Kingine nilichojifunza ni kuwa wakati huu wa bajeti baadhi ya makamishna wa HAZINA hugeuka miungu. MARAS na MA DED hupiga magoti kuomba omba fedha as if fedha wanazoomba ni zao kwao Binafsi. Yupo Kamishna mmoja kutoka mkoa aliotoka mwalimu ambaye ametengeneza altare na kila Afisa Mhasibu humpigia magoti kuomba fedha. Hii ni aibu kubwa kwa nchi yetu.Ni aibu kwa Waziri Mkuu kwasababu aliahidi kusimamia na kuhakikisha Bajeti ya Mwaka huu inaandaliwa ili kuimarisha sekta muhimu kama kilimo. Ameshindwa. Mikoa na Halmashauri ndio zinamaliza kuwasilisha bajeti zao. Wataalamu waliotumwa toka TAMISEMI kumsaidia ni kama hawajui lolote. Wameingia pale hawana wanachojua wakabaki kusuburi lunch boxes. Utastaajabu. Wakati mikoa inawasilisha bajeti zao ungetegemea wachangie au wahoji lolote lakini wapi. Baadhi wakawa wanatwanga usingizi na wengine utafikiri hawapo. Aibu tupu. Ninadhani kati ya mawaziri wakuu tuliokuwa nao. Huu ni mtazamo wangu. Pinda atahesabiwa kuwa Waziri Mkuu dhaifu na Mswahili kuliko wote waliowahi kuongoza Tanzania. Anasema hafuatilii.
   
 17. T

  TheSun New Member

  #17
  May 3, 2009
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanza inasikitisha kuona kwamba taratibu husika zilikuwa hazifuatwi katika swala zima la kile kinachooenekana kama nia njema ya watu hawa. Kwanza swala la msaada si swala la mwanzo la TIC (since its not an investment), ni swala linaloangukia katika taasisi za utoaji huduma kwa jamii zisizo za kiserikali. Hivyo kama lengo ilikuwa ni kutoa msaada, wahuskika au wale ambao mlikuwa mkishiriki kuhakikisha kwamba lengo la watu hawa linakamilika m(wa)ngefuata hatua za mwanzo za kujua ni huduma gani tayari ipo katika eneo hili la Bagamoyo, pili ni matatizo na faida gani ambazo hii hudumu inayo katika kukidhi matakwa ya watoaji na wahitaji huduma yake, through feasibility study, ainisha maeneo unayoyaona kwamba yanahitaji msaada ambao utatatua na kuendeleza mradi huo ikiwa ni pamoja na kuainisha maeneo yanayonitaji kufanyiwa kazi na kutoa matokea yaliyokusudiwa katika kipindi cha muda mfupi na muda mrefu. Baada ya kuwa na hii ripoti wasilisha kwa taasisi husika kile ulichokiona kinahitaji msaada na malengo yako, basing on your area of interest wao watakueleza nini wanachokijua kuhusu mradi huo na kukuelekeza nini cha kufanyika kama nikukupa orodha ya taasisi husika ambazo tayari ziko kwenye mradi huo, walicho/wanachokifanya, matatizo yao n.k. ili uweze kuona kama unaweza kuwatumia katika kutekeleza malengo ya msaada wako huo au ni taratibu gani unahitaji kufuata kuanzisha mradi wako binafsi kwa kusudio hilo hilo la kutoa msaada...hapa ndio usajili wa mradi wako utahitaji kupitia TIC au kufuata maelekezo yao kwa kuzingatia taratibu na sheria za nchi zilizopo katika swala hili. Serikali ya Japan ilifuata taratibu hizi kwa soko la feri.....sasa sijui hawa ndugu walikuwa serious kiasi gani lakini hujaeleza kwa kina ni taratibu gani zilifuatwa kabla ya kuilaumu serikali.....

  "Failure can be divided into those who thought and never did and into those who did and never thought."
   
  Last edited: May 3, 2009
 18. S

  Simoni Member

  #18
  May 3, 2009
  Joined: Oct 10, 2008
  Messages: 67
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na mpendanchi2
   
Loading...