Nchi haiendeshwi na mitandao ya kijamii!!-Salva Rweyemamu

Ni kweli. Nchi ikianza kuendeshwa kwa kupitia mitandao ya kijamii ni hatari sana.

So Salva was right on point.
Mkuu Mitandao ya Jamii inawakilisha SAUTI za Wanajamii, Wanasiasa na wafaidika wa keki ya Taifa siku zote hali ngumu ya maisha kwao ni hadithi, Mfumuko wa bei hauwezi kumkuta JK ,Salva and the like.Hali ya maisha ni ngumu sana jamani.Huko vijijini moto unawaka acheni tu.
 
Hivi kweli nchi au organisations yoyote inaweza kuishi bila kupata na kutoa habari?Inawezekana jamaa huyu ni juha la habari.
 
Nchi iko shwari wakati maisha yanazidi kuw amagumu
Mfumoko wa bei ni tatizo la dunia kwani jamaa amekuwa gavana wa benki kuu anatupa taarifa hizo
Imani kwa rais amefanya research wapi kutupa data kuwa imani kwa rais wa nchi inazidi kupanda
maisha ya mtanzania yanazidi kuboreka kwa kipi kwa kutojua kesho anakula nini ndo maisha yanaboreka
Ahhh majibu mepesi kwa maswali magumu

Safi sana mkuu kwa kuyaona hayo.Salva anaganga njaa ikulu hana lolote.
 
Hivi serikali ikichukua cues zake toka humu JF wewe utaiona hiyo ni serikali ya maana kweli?

Ndo yale yale ya Captain kushupaliwa kuchukua hatua kwa ushahidi wa kwenye mtandao (Jason borne's conspiracy theory) uliopelekwa na six.
 
Salva atasemaje wananchi imani kwa Rais wao inazidi kupanda wakati ulinzi wa huyo mkweree ndio unazidi kuimalishwa kwa woga gani kama wananchi wake wanampenda? Wangekuwa wanampenda wasingempopoa na mawe wala kumpa maneno ya kumkashifu mitandaoni!! Rais anaependwa haogopi kuonana na wananchi, lakini huyu mkweree hana hata ratiba ya kuonana na wanachama wake kama ilivyokuwa enzi za Mwinyi ambapo wanachama walikuwa wanaonana nae pale ofisi ndogo ya chama Lumumba au hata Dodoma!!

Ndivyo MAGAMBA wanavyojipa matumaini kuwa wanapendwa. YAANI NATAMANI HII MIAKA IISHE UPESI. Na jinsi maisha yalivyokuwa magumu sidhani kama nitafikia 2015.

hana Jipya la kueleza watu, hivi huyo Rweye kama alijua kuwa hawezi kujibu maswali, alifuata nini Studio. Kwa nini asingelimtuma Shamba Boy wa Ukulu huenda angelijibu vizuri.

MAISHA BOMU KWAKILA MTANZANIA

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
NICAMPOON

8.JPG
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Wacha waendelee kujifariji kupitia vi-media vya wazee wa kujipendekeza...... Revolution is on Progress!!!!!!
 
Wajameni hivi umri wa kustaafu ni miaka mingapi kwa watumishi wa Serikali??

Mzee kama huyu bado yupo ofisini, na ndio maana hata akili nayo imelala. Kisha tunalalamika kuwa tanzania ajira ni ngumu kumbe kuna watu wanaopaswa kustaafu bado wapo kazini. Vijana wenye akili zinazochemka wanakosa ajira.

Au mnataka hadi tuandamane ndipo mtatoka maofisini mtupishe vijana. Na ndio maana nchi inakwenda vibaya kwa sababu ya wazee wanaongangania ofisi.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
nilichigundua ni kuwa Kibonde alimuuliza Rweyemamu maswali mazuri na yenye mustabali wa taifa ila huyu rweye akatoa majibu marahisi sana. hili ni janga la kitaifa kama hamjui
Kifupi walikutana waigizaji wawili wa Zecomedy original.
 
Salva anasifia suti ya mfalme ilivyo nzuri wakati kila mtu anaona mfalme yuko uchi.

Hizi njaa tabu sana.

Salva uzalendo ulimwisha kipindi alipoteuliwa kuwa mwandishi wa habari wa Rais... Otherwise,zamani alikuwa timamu sana... Calibre ya kina Jenerali alikuwa... Tulikuwa tunakunywa naye chai(breakfast?) Chef's Pride..

Ah.. Basi bana..
 
Mkuu Mitandao ya Jamii inawakilisha SAUTI za Wanajamii, Wanasiasa na wafaidika wa keki ya Taifa siku zote hali ngumu ya maisha kwao ni hadithi, Mfumuko wa bei hauwezi kumkuta JK ,Salva and the like.Hali ya maisha ni ngumu sana jamani.Huko vijijini moto unawaka acheni tu.

Kwa hiyo unaona ni sawa kabisa kwa serikali kuchukua cues zake toka humu na kwenda kuzifanyia kazi kesho yake?
 
Crystal clear! nchi haiwezi kamwe kuongozwa na mitandao na magazeti.

Nchi haiongozwi na mitandao ya kijamii na magazeti! Kwa nini wakubwa kila kukicha wanawaita waandishi wa habari (wengi ni wa magazeti)? Kwa nini yeye Salva aliajiriwa Ikulu? Ni mjuzi wa sera? Au mtabiri wa nyota?

Kwenye hoja ya mitandao ya kijamii, wanaoandika kwenye hiyo mitandao ni misukule? Na wanancho andika kina mantiki? Yeye binafsi (Salva) anatumia mitandao ya kijamiii kutoa habari au hatumii? Kule michuzi blog anapeleka press release zake kila siku kwa nini? Huko sio kuendesha nchi kwa kutumia mitandao ya kijamii kama unatoa taarifa kupitia kwenye hiyo mitandao? Boss wake mwenyewe yuko kwenye facebook na twitter? why?

Salva akitambua kuwa hiki ni kizazi cha dotcom atafanya kazi vizuri lakini akiegemea zama za ki-RTD RTD atakwaruzika!
 
wasemaji wote wawe wa wizara au idara au ikulu huwa ni waongo kutetea unga wao
huyu bwana alikuwa number moja kukosoa CCM nk alipopewa kacheo kafunika kila kitu maisha ya kinafiki kama haya hayana maana
Mtume Petro alimkata mtu sikio kumtetea Yesu,atuambie kama yuko tayari kukatwa sikio kwa ajili ya kutetea uwongo wa aina hii
nchi iko salama wapi watu wanaishi kwa tabu au kwa vile anatembela VX anasahau watu wanaishi kwa dhiki kwa sababu ya uovu na uongo anaoutetea. Ole wao wanafiki,waongo, maana dhiki yao kuu imeshaandaliwa,
 
Mitandao imeandika kuhusu kuvunjwa na kubadilisha baraza la mawaziri, tunamtaka Salva baada ya miezi 2 aje atu-prove wrong
 
msemaji wa ikulu,ktk kipindi cha jahazi,amesema nchi iko shwari kabisa,na imani ya wananchi kwa rais wao inazidi kukua kila cku!!tatizo la mfumuko wa bei sio tatizo la serikali ni tatizo la dunia nzima!na wale wanaopiga kelele kila siku juu ya mabdadiliko ya baraza la mawaziri sio kazi yao,na pindi rais atakapoona inafaa kufanya hivyo atafanya hivyo.Na magazeti yaache kutabili mambo kwani hata kwenye makubaliano yaliofikiwa kwenye mgogoro wa madaktari,ni baina ya serikali na ma dr,wala sio na magazeti.Na maisha ya mtanzania yanaboreka kila uchao!!kweli mwenye shibe hamjui mwenye njaa jamani.
Mbona Jk anaongea kupitia face book?Je huo si mtandao?
 
Ilikuwaje Mkama akatuhumu Jf
 
Hivi serikali ikichukua cues zake toka humu JF wewe utaiona hiyo ni serikali ya maana kweli?

Mkuu mie sioni ubaya wowote kama zitasaidia kuleta maendeleo, kupambana bila woga na mafisadi na hata kuwafilisi mali walizozipata kifisadi, kuhakikisha rasilimali za nchi zinawanufaisha Watanzania wote badala ya wageni na mafisadi n.k.
 
Mimi napenda serikali inayofuata utawala wa kisheria na inayoendeshwa kwa mujibu wa katiba. Serikali yoyote ile inayoendeshwa kwa kufuata yale yajadiliwayo mitandaoni na watu wasiojulikana ni hatari sana.

Kwa hiyo bado naiunga mkono kabisa hoja ya Salva ila haina maana naiunga mkono CCM. Nataka tu yeyote atakayekuwa madarakani basi aongoze kwa mujibu wa sheria/ katiba.
 
Back
Top Bottom