Nchi gani ya Afrika iliyoongozwa/tawaliwa na Rais mmoja tu kwa miaka mingi na ikapata maendeleo?

lukoma

JF-Expert Member
Jul 1, 2013
2,995
2,245
Iko mifano mingi Afrika ya nchi ambazo marais wake wameongoza au tawala kwa muda mrefu (miaka mingi) lakini hakuna chochote cha maana walichofanya. Kutaja kwa uchache, Uganda na Congo!!!

Itambulike iwe Rais mwenyewe, wasaidizi wake, washauri wake au mwananchi wa kawaida kufikiria tu rais aongezewe muda ni ubinafsi ambao matokeo yake ni udikiteta!

Kikwanzo kikubwa sana cha maendeleo Afrika ni ubinafsi (udikiteta) sio mabeberu. Hivi nchi yenye raia zaidi ya 50 m unawezaje kufikiri wewe ni bora zaidi kuliko wengine wote. Wazo kama hilo ni ubinafsi ambao huzaa udikiteta.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.
 
Libya ilikuwa na maendeleo chini ya Gadaffi

Sent using Jamii Forums mobile app
Maendeleo katika mtazamo upi? wa madaraja na barabara? sawa, ya kijamii je? yalikanyagiwa chini. Mwanadamu amezaliwa kuwa huru na si hivyo tu bali mahitaji ya binadamu yanabadilika kila uchao. Akisharidhika na jambo moja huwa anataka lingine. Kwenye management tunasema a satisfied need is not a motivator. People cannot be motivated by a single motivating factor. There is always hierarchy of need.
Kwa hiyo kusema kwamba umenunua ndege na umejenga madaraja ndo watu watakuwa motivated forever ni kujidanganya.
 
Wapo walioleta sawa maendeleo lakini kwa kubinya haki na uhuru na maendeleo ya nchi izo uishia kuwa historia maana wengi wao uondoka kwa nguvu ya wananchi. kiongozi makini ni yule anayetoka madarakani haraka kabla ajachokwa kama alivyofanya Nyerere.
 
Libya ilikuwa na maendeleo chini ya Gadaffi

Sent using Jamii Forums mobile app
Maendeleo lzm yawe endelevu,libya ni mfano mzuri wa kujenga nchi juu ya mgongo wa mtu mmoja badala ya taasisi,hata Nyerere alifikiri kudumu kwenye uongozi kutamhakikishia kuisogeza nchi kimaendeleo lkn badala ya kusonga mbele alishuhudia mporomoko wa uchumi akamua kusimama pembeni ni kwa sababu Nyerere alikuwa na hekima lkn hao akina museveni ni watu wa kawaida sana wanaongozwa na woga na ubinafsi tu hawafai kuwa tolea mfano.
 
Back
Top Bottom