Nchi gani kiongozi anatembea na msafara wenye kubeba maspika yenye nyimbo za kumsifia?

instagram

JF-Expert Member
May 27, 2014
2,091
4,715
Kwa kiongozi kufanya msafara na maspika yenye nyimbo zinazobeba maudhui ya sera za chama ni jambo la kawaida hasa hasa kwenye kampeni za uchaguzi au uzinduzi au hafla za kichama.

Ila kwa kiongozi kusafiri au kufanya ziara za kitaifa na magari yaliyobeba maspika yanayopiga nyimbo za kukusifia wewe binafsi na siyo chama chako wala maudhui ya chama si jambo la kawaida.

Je, ni kiashiria gani kwa kiongozi wa kitaifa kufanya ziara za kikazi kitaifa akiwa na magari yenye maspika yanayopiga nyimbo za kumsifia yeye binafsi na siyo chama chake?
 
Ulitaka wakusifie wewe? Vile vile fahamu hizo nyimbo kwa mfano zinawasifia viongozi wote kuanzia rais, makamu, waziri mkuu na wananchi wa Tanzania. Shida ni nini Rais Magufuli anawanyima usingizi, na bado mtakoma tu!
 
Ndio ulivyopangiwa kuandika leo?
weka clip hapa inayoonuesha nyimbo za kumsifia zaidi Rais ziarani.

tunachokiona ni kwamba spika zile zinatumika kwa kufanikisha hotuba za rais anaposimama kuongea na wananchi hata kama hakuna jukwaa rasmi lililoandaliwa rasmi.

na hii ni mwiba kwenu msiomtakia mema rais,maana kaja na staili yake ya uongozi na ya kuwafikia wapiga kura wake bila kusubiri kupangiwa na wale wapigaji,kama tulivyozowea huko nyuma awamu zilizopita.

mahali pekee tunaposikia rais akiimbiwa ni pale anapokuwa na hafla au ufunguzi wa miradi ya maendeleo kote nchini

na hii ni protocol ya kawaida ya ushereshaji.

Nyinyi team MACHUNGU mmejaa sumu hasa hao wanaowatumia baada ya kukosa mlichokuwa mkitarajia yaani kunyanganywa tonge mdomoni.

hasira full time,hata macho uamejaa hasira tupu.

Ni wazi kwamba wapinzani mmeishiwa sera.
Magufulification imewashika nyumbu wote na sasa mnashiriki ziara zake kila kona.
na hii inadhihirisha lwamba mnaunga juhudi,kwa staili yenu.

shame on you idiots at all the time.kwa kushindwa kuyaona mabadiliko makubwa yanauotokea nchini huku mkijdai kuomba demokrasia wakati nyinyi ikiwashinda kwenye vyama vyenu.

Tuko na JPM mpaka 2025
 
Mkuu hayo maspika mimi naobaga yanarahisisha mazungumzo kati ya Rais na halaiki yake hasa wale kinamama wenye matatizo...sijawahi kuona hizo spika zikifunguliwa manyimbo na watu wakaanza kuserebuka kama tulivyozoea kuona kwenye kampeni kwa jinsi ulivyojaribu kutuambia hapa.
 
Back
Top Bottom