Nchi fulani inaweza kuichezeana nchi nyingine michezo michafu kuvuruga amani

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,939
Wadau habari jana nilitafakari sana sana nikafikia tamati ya mawazo yangu kwamba katika diplomasia fulani kiongozi anaweza kung'amua mapema michezo michafu ya nchi husika hivyo akashauriwa akaachana na mahusiano kitendawili yasiofaa.

Hivyo kiongozi aakacha kuihusudu nchi ya Bosnia hezegovina, inawezakana nchi ya Bosnia inaagenda yake ya siri kwa kuwa kiongozi wake ametokea kwenye jamii ya intellijensia, lakini kiongozi wa Chechnia hana hata uelewa wa masuala ya kiintelijensia ya kimataifa lakini kiongozi, Alexandre ivanovich aliigundua mapema kwa kupokea ushauri kutoka kwa Mkurugenzi mkuu wake wa usalama bwana Victor Vyerichev kwa kuambiwa punguza mahusiano na Bosnia kwa kuwa kuna dalili zote kwamba kuna kikundi cha kuua watu ndani ya nchi ya Bosnia kinavuka mipaka na kufanya mauaji kwa nchi ya Chechnia ili kuichafua nchi ya Chechnia kuiporomosha kiuchumi,kisiasa na kiuslama,kisa tu imetulia kwa miongo,na inaonekana nchi ya Chechnia iliwahi kuishauri Bosnia iache kuingilia na kuibiia cremia mafuta yake.

Mkurugenzi wa usalama wa Chechnia bwana Victor Vyerichev akatoa angalizo kali kwa kiongozi huyo na kumwambia hatakua tayari kuiona Chechnia inaangamia, kuja kustuka ilikua ndoto na kuamua kuamka asubuhi kusali na kupasha mwili joto.
 
Wachache watakuelewa

Why wachache? Kila mtu anaelewa isipokuwa watu hawatatoa comments kwa sababu hadi sasa hawajaelewa katika hiyo ndoto, bwana Victor Vyerichevr alieelwaje, alichukua hatua zipi baada ya kusikia akiambiwa ajiongeze. Lakini zaidi, ndoto haikusema alikuwa addicted kwenye huo uhusiano kwa kiasi gani. Ndoto haikusema uhusiano huo aliuthamini kwa sababu alijua kuna mwelekeo mwema, au aliushikilia kwa sababu hakuwa na confidence hivyo kutafuta rafiki wa kumwongoza namna ya kutawala.

Lakini baada ya hayo, hujasema kama alikubalia ama kukataa ushauri na nini ilikkuwa hatima ya hao waliomshauri. Hivyo, wanaogopa hatima yao mkuu!.
 
Hivi Victor Vyerichev alimkemea kiongozi wa Bosnia au bosi wake, kama hadi Victor amkemee kiongozi wa Bosnia huku boss wake yuko kimya inawezekana Alexandre ivanovich na kiongozi wa Bosnia dili lao moja, au Alexander alikuwa sio mzaliwa wa Chechnya.
 
Ama Alexander aliwekwa Chechnya na Vyerichev kufanya kazi zake ndo sababu alikosa nguvu kuachana urafiki na rais wa Bosnia. Kama angelala tena akaota tungeelewa urafiki wao uliishaje kati ya hao viongozi wa hizo nchi mbili.
 
Kabisa inawezekana ni mipango ikiwa kama kisasi kwa hiyo nchi juu jambo ya fulani lililowaumiza huko nyuma. Labda kuzuia wizi wao wa rasilimali za nchi nyingine jirani
 
Hata ukielewa jitaidi Ku comment kwa mafumbo maake hali ya hewa imebadilika hawachelewi kukuteka hawa kundi sumbufu la wasiojulikana.

Kundi korofi sana hili....anyway-mr Slim anamwendesha mkuu kwa kila kitu
 
Mkuu tumekuelewa ila inategemeana na tabia ya mkuu wa nchi na tabia ya mkuu wa usalama wa Taifa,kuna yale makundi ya tabia za watu akina sanguine nk mi sio mtaalamu sana,endapo mkuu wa nchi yupo ktk kundi la tabia sawa na mkuu wa usalama wa taifa tusitegemee badiliko,tusubiri anguko maana kila mmojawapo atajiona bora na hashauriki hvy mbwai na iwe mbwai ,Mungu anahitajika sana atuonee huruma ktk hili.
 
Comrade Igwe..hakika wasema na lisemwalo lipo kama halipo laja...Mstaafu wa nchi ya Bosnia Herzegovina kwenye kikao cha ukanda wa nchi zenye maji mengi na maziwa makuu miaka ile akatoa ushauri wa amani kwa kiongozi mkuuu wa nchi ya Chechnia akae na wenzake kuondoa mtafaruku wa yanayotokea ukanda wa maziwa makuu na asali,jambo likawa jambo akajiapiza kuwa wewe mkuuu wa Bosnia Herzegovina hufahamu unalonena hakika nitakusubiri muda muafaka utanitambua.Je tunakumbukumbu!
 
Hata ukielewa jitaidi Ku comment kwa mafumbo maake hali ya hewa imebadilika hawachelewi kukuteka hawa kundi sumbufu la wasiojulikana.

Kundi korofi sana hili....anyway-mr Slim anamwendesha mkuu kwa kila kitu
Hao hawana uwezo wa kuteka watu humu wameshashindwa, ingekuwa FB hapo sawa, humu Hadi ujianike mwenyewe.
 
Hata ukielewa jitaidi Ku comment kwa mafumbo maake hali ya hewa imebadilika hawachelewi kukuteka hawa kundi sumbufu la wasiojulikana.

Kundi korofi sana hili....anyway-mr Slim anamwendesha mkuu kwa kila kitu
Dah
 
Hivi Victor Vyerichev alimkemea kiongozi wa Bosnia au bosi wake, kama hadi Victor amkemee kiongozi wa Bosnia huku boss wake yuko kimya inawezekana Alexandre ivanovich na kiongozi wa Bosnia dili lao moja, au Alexander alikuwa sio mzaliwa wa Chechnya.

Ni mzaliwa wa Bosnia Herzegovina
 
Why wachache? Kila mtu anaelewa isipokuwa watu hawatatoa comments kwa sababu hadi sasa hawajaelewa katika hiyo ndoto, bwana Victor Vyerichevr alieelwaje, alichukua hatua zipi baada ya kusikia akiambiwa ajiongeze. Lakini zaidi, ndoto haikusema alikuwa addicted kwenye huo uhusiano kwa kiasi gani. Ndoto haikusema uhusiano huo aliuthamini kwa sababu alijua kuna mwelekeo mwema, au aliushikilia kwa sababu hakuwa na confidence hivyo kutafuta rafiki wa kumwongoza namna ya kutawala.

Lakini baada ya hayo, hujasema kama alikubalia ama kukataa ushauri na nini ilikkuwa hatima ya hao waliomshauri. Hivyo, wanaogopa hatima yao mkuu!.

Victor Vyericherv aliamua kuingia kazini rasmi kwa manufaa ya Chechnya
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom