Hivi karibuni kulikuwa na matangazo ya wizi wa pesa kupitia wanafunzi hewa wa vyuo vikuu. yaonekana hilo ni tone ktk tabia mbaya iliyoko vyuoni.
Maelezo yafuatayo, yametolewa kwenye mtandao wa chuo kikuu cha kilimo, SUA. Bahati mbaya kabisa wahusika ni wakuu wenyewe, sijui nani anapewa jukumu la kulinda mali ya umma chuoni.
Soma na kama kuna vyombo vinavyohusika fuatilieni ili nchi iende inavyotakiwa.
------------------------------------------------
Wale munaofuatilia yanayotokea hapa chuoni, munafahamu sekeseke linalotokea kwa sasa hadi watu wamepigiwa simu za vitisho ili waache kulizungumzia tatizo hilo. Kwa ujumla ni wizi mkubwa wa pesa za mradi wa NORAD uliokuwa kwenye ujenzi wa jengo la kitivo cha sayansi kule Mazimbu.
Takribani bilioni 1 imeliwa na watawala wetu. Jengo hili limekuwa likijengwa kwa miaka zaidi ya mitatu sasa. Ni jengo dogo lililopangwa liwe la gorofa tatu. Baada ya kupatikana pesa, likapunguzwa kuwa ni la gorofa mbili na mwishoni sasa limekuwa ni jengo la gorofa moja, lakini gharama yake imebaki kuwa ni ile ile!
Ni muendelezo wa miradi ya wizi pamoja na ile ya ujenzi wa kumbi mbili za mihadhara iliyochota zaidi ya bilioni 1.3, maktaba ya mazimbu iliyobomoka tangu siku ya kwanza, maabara ya zoolojia inayovuja hadi leo bila kutumika, chanzo pekee cha maji kilichotumia mabilioni wakati hadi leo watu wanakunywa tope, huku kukiwa na tenda feki za madawa kila mwaka, pia jengo la kilimo biashara ambalo leo hii limechakaa hata kabla ya miaka 4!
Pesa kama hizo kwa vyuo vingine linajengwa jengo kubwa na la maana sana.
Wakati Naibu katibu mkuu alipotembelea chuo hiki cha SUA, mwezi wa nne alielezwa ujenzi huo ulikuwa unaendelea vizuri na kufikia mwezi wa 6 jengo lingekamilika.
Leo hii Disemba jengo bado halijamalizika na pesa hazitoshi kwa kusingizia mabadiliko ya ujenzi ambayo hata hayastahili kutumia milioni 100, sasa chuo kinatafuta mabilioni kwa kisingizio kwamba ni kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa jengo hili. Huu ndio mgogoro tulionao sasa hivi hapa chuoni tunaomba wote wanaousikia, waelewe.
Yaonekana nguvu ya Mh. Magufuli haijasikika vizuri hapa chuoni maana kwa taarifa tulizonazo toka ndani ya idara ya uhasibu SUA, pesa za jengo hili, viongozi wetu wamezigawana na zimeliwa kwa pamoja. Bila aibu naomba niwataje kama nilivyosimuliwa kwamba wafuatao ndiyo wamegawana pesa hizo.
Ikiwezekana wajitokeze kueleza sababu ya kuleta vitisho kwa wale wanaouliza upotevu huo wa pesa:
1. Mkuu wa chuo (VC) Prof. Monela amebeba sehemu ya pesa hizo, mlinzi mkuu wa mali ya chuo asiyefanya kazi yake
2. Naibu makamu mkuu wa chuo taaluma (DVC acad), Prof Gillah kila dili kwake ni safi tu
3. Msarifu (Barsar), ndg. Raphael na staf yake hadi kwa cashier wetu hawa ni walinzi wasiotaka kulinda pesa
4. Ofisi ya ugavi ilipewa mgao wa jumla Yaani Zumo na watu wake ambao ni wazoefu ktk dili
5. Afisa mipango, Masawe na watu wake ambao ni wazoefu kwa dili kama hizi
6. Ukaguzi wa mahesabu kwa akina Mulyomi pamoja na watu wake walipitisha kuwa ni malipo halali
7. Kurugenzi ya utafiti, pale Muhikambele alipewa na watu wake na hata messenger alipata.
8. Mkuu wa kitivo cha sayansi. Prof. Mwangingo ambaye amejitafuna mwenyewe jengo lake
Kuna watu wengine wawili ambao wanaonekana kufahamu dili hili na wanafahamu jinsi gani pesa hizo zimeliwa.
Tuna wasiwasi kwamba hata wao walipewa mgao. Hao ni:
1. Prof. Ishengoma
2. Prof. Kulwijila
Wawili hawa ni wahusika ktk mradi huo na hakika wanastahili kufahamu pesa ilivyochotwa.
Ndugu zangu hawa ndiyo viongozi wa chuo chetu cha SUA tunaodhani wanaendeleza chuo. Tunapohangaika kuongeza mapato ya chuo tuelewe viongozi wanaongeza wizi pia.
Sasa hivi juhudi zinazofanywa ni kuzuia mambo haya yasiende nje ya chuo na bahati mbaya wanatumia vitisho vya simu na kuna sehemu wamesikika wakitafuta pesa za kuhonga wale wanaodhani wanaweza kulitoa nje ya chuo.
Sisi wanajumuiya ya chuo tunasemaje? Waalimu tunasukumwa kufundisha kwa nguvu bila hata motisha wakati wenzetu wakichota pesa na kujenga mahoteli yasiyolingana na kipato chao. Ombi langu kwa watu hawa, warudishe pesa za jengo hili kwa gharama yoyote ile hata kama ni kuuza hoteli wanazojenga.
Habari hizi tunazifikisha TAKURU tukiomba watusaidie kueleza jinsi gani pesa imepotea kwa kisingizio kwamba zilirudishwa kwa wafadhili. Maana jengo la gorofa moja haliwezi kuwa na thamani ya bilioni 3. Hatutakubali kuwalea wezi. Bahati mbaya kabisa hata wastaafu tunaohitaji uzoefu wao mzuri kumbe wao wamezoea mengine kabisaa!
Haya ni maelezo ya wazi kwenu wahusika. Jitokezeni mueleze kwa nini jengo halijaisha na kwa nini gorofa moja itumie zaidi ya bilioni mbili kwa kisingizio cha maabara.
Magereza watajenga nyumba kibao za kuishi kwa bilioni 10 tu za Mh. Rais!