Nchi 10 nje ya Afrika wanakopatikana waafrika wengi zaidi duniani.

ZaqEddy

Member
Jun 21, 2016
78
61
Kwa mujibu wa nadharia ya “Nje ya Afrika”, watu wamesambaa kutoka barani Africa kwenda kokote kuujaza ulimwengu. Waafrika hawa wa sasa wamewafuata wazee wao wa kale sehemu za mbali – lakini kuna baadhi ya maeneo ambayo yaliyoko nje ya bara la Afrika ambako waafrika wameweka makazi na kukulia huko.
africa+usiku.jpg


Sababu za waafrika hao kufika na kuweka makazi katika nchi hizo zinatofautiana sana, zikiwemo sababu za makazi wakati wa utumwa na uhamiaji. Orodha hii ni ya nchi 10 dunia nzima ambazo zina idadi kubwa wa watu weusi wengi mbali na bara la Afrika. Hii ni kwa mujibu wa mtandano wa Howzit MSN.
Brazil Nchi ya Brazil inaongoza kwa kuwa na watu weusi zaidi duniani kwa nchi ambazo haziko bara la Afrika. Kuanzia karne ya 16 hadi kufikia miaka ya 1860, nchi ya Brazil ilikuwa ndiyo msafirishaji mkubwa wa watumwa ulimwenguni. Walakini, Brazil pia ni miongoni mwa nchi inayopigiwa mfano kwa kuwa na uwiano wa kuwa na ongezeko la watu mchanganyiko ulimwenguni.
brazil.jpg


Vipimo vya DNA kuhusu makundi ya ukuaji wa watu nchini Brazil katika miaka ya hivi karibuni, inaonesha kuwa, watu wanaweza kuwakilisha uwiano wao katika namna ambayo haiakisi asili yao.

United States Nchi ya Marekani, ni nchi ya pili kwa kuwa na idadi kubwa ya watu weusi duniani ikiwa na watu 12 million ambao wanatambulika kuwa wana asili ya Africa. Waafrika nchini Marekani wanafanya kuwa na idadi kubwa ya watu nchini humo.
USA.jpg

Waafrika wengi nchini Marekani wamekwenda kipindi cha biashara ya utumwa, walakini, kwa miaka ya sasa kumekuwa na ongezeko kubwa na wahamiaji kutoka Afrika kuelekea nchini Marekani ambapo 57% ya wahamiaji nchini Marekani wamehamia katika kipindi cha kuanzia mwaka 1990 hadi 2000. Raia wengi wa Marekani wamekuwa wakijaribu kutaka kujua hasa vizazi vyao vimetokea wapi. Mwanamama Oprah Winfrey tayari amepata kujua wapi kizazi chake kimetokea ambapo inadaiwa kuwa kimetokea nchini Liberia.

Colombia Jamii ya watu wa bchi ya Colombia hutofautiana kimakundi na imechanganyika, ikiwa na 14% ya mchanganyiko wa watu wenye asili ya Afrika na Ulaya, 3% imefanywa na mchanganyiko wa watu wa jadi ya Africa na Amerindia, na 4% inatokana na watu wa jadi ya Africa moja kwa moja.
colombia.jpg


Wahamiaji wengi kutoka bara la Africa kwenda nchini Colombia wamefika nchini humo kutokana na biashara ya watumwa katika karne ya 16 na 19 na wameweka makazi katika pwani za Caribbean na pacific. Haiti 85% ya watu wananchi wa Haiti wana asili ya Afrika Magharibi wakati 25% inayobakia inatambika kuwa ni mchanganyiko wa asili. Kufuatia mapinduzi ya watumwa, yaliyochagizwa na mapinduzi ya Ufaransa, nchi ya Haiti ilikuwa ni nchi ya kwanza kuwa Jamhuri ya watu weusi duniani.
haiti.jpg

Mapema mwaka jana, nchi ya Haiti ilitangaza kuwa itaomba uanachama katika Umoja wa Africa, ingawa nchi hiyo haiku katika bara la Africa. Jamhuri ya Dominica Watu wa jamhuri ya Dominica ni mchanganyiko (kufikia 73%) wakati 11% ya watu hao inatambulika kuwa ni watu weusi. Stadi zinaonesha kuwa hadi kufikia 85% ta watu nchini humo ni uzazi wa Africa.
dominican+republic.jpg

Jamhuri ya Dominica ina historia ya makundi ama tofauti za makundi ya rangi, na kabila hasa wakati wa kipindi cha Trujillo ambapo kina maana ya kuwa watu hupangwa kulingana na utambulisho wa makundi yao. France Ni kinyume cha sheria kukusanya takwimu ya rangi/kabila na dini nchini Ufaransa, ingawa imekisiwa kuwa idadi ya watu kutoka bara la Afrika na Caribbean nchini Ufaransa inafikia watu kati ya 1 - 1.5 million. Makisio mengine huiweka namba hiuo juu zaidi.
france.jpg

Watu weusi wanne kati ya watano nchini Ufaransa wanatoka katika jadi ya Africa. Wahamiaji wa Africa nchini Ufaransa wanatoka katika nchi za Algeria, Morocco, Tunisia, Cameroon, Ivory Coast, Mali na Senegal. Jamaica 92% ya watu nchi Jamaica wanatoka barani Africa. Watumwa 750 000 walipelekwa nchini Jamaica kutoka nchi zijulikanazo sasa kama Ghana na Nigeria kati ya 1655 na 1807. Hata pale biashara ya utumwa ilpokomeshwa bado wafanyakazi kutoka sehemu mbalimbali za ulimwengu huu walimiminika nchini Jamaica.
jamaica.jpg

Hali uhamiaji ingalipo nchi Jamaica, ikiwa na idadi kubwa ya waJamaica waliotawanyika katika nchi za Marekani, Uingereza na Australia. Uingereza Katika miaka ya nyuma, watu weusi walianza kuhamia nchi Uingereza mwishoni kabisa mwa karne ya 16. Mapema karne ya 17 watumwa kutoka barani Africa ambao walikuwa nchini Hispania walianza kumiminika na kuingia nchini Uingereza.
uk.jpg

Idadi ya wakaazi weusi nchini Uingereza iliongezeka wakati wa kipindi cha biashara ya watumwa. Idadi kamili ya sasa ya raia wa Uingereza wenye jadi ya Africa na Caribbean inafikia watu 1.5 million. Cuba Takwimu kuhusu asilimia ya watu wenye jadi ya Africa wanaoishi nchini Cuba ina kinzana sana, stadi zingine hudai kuwa, watu hao ni 33% wakati wengine wakisema inakaribia 62%. Lakini watu wanaopatikana katika kisiwa hicho inajulikana wazi kuwa ni mchanganyiko.
cuba.jpg

Kuna wahamiaji hasa kutoka nchini Angola na mataifa mengine ya Africa. Inaarifiwa kuwa, ukabila na urangi ni haramu nchini Cuba. Italy Hadi mwaka 2010 nchi ya Italia inakadiriwa kuwa na wahamiaji 1 million kutoka barani Africa. Wahamiaji wengi wa kiafrika nchini humo wanatokea katika nchi zilizopo Kaskazini mwa Africa kama vile Morocco, Tunisia, Misri na Algeria.
italy.jpg

Pia wapo wahamiaji kutoka nchi za Afrika magharibi kama vile Senegal, Nigeria na Ghana.
 
Back
Top Bottom