Nchemba tena - bungeni; adai kutishiwa kuuwawa na wabunge wa CHADEMA

Mwigulu vipi! murder zote hupelekwa Mahakamani, iweje uombe utaratibu Bungeni ili kujadili vurugu za Iramba na kupelekea mauaji ya mfuasi wa ccm, mbona hukuomba utaratibu kwa kutekwa Dr.wetu Ulimboka? Acha Bunge liokoe muda na fedha ya walipa kodi,Wahi kwenye sheria.
 
Waendelee tu kucomedica huko bungeni.. 2015 yaja, wananchi tutafanya maamuzi sahihi

Huyo mwigulu hata mtoto ndondocha ana nafuu.. msameheni bure
 
ccm watu makini either hawapewi nafasi au hamna, lakini sitaki kuamini kuwa hamna nawafahamu wengi makini!

watu makini wa ccm unafiki unawafanya wasiwe makini na ukiwa mnafiki si makini tena unakuwa umepoteza sifa, mkama katibu wao ni makini sana ona alivyofunikwa na unafaki sasa anaonekana kituko, kwa ujumla ukiendelea kuwa ndani ya ccm umakini haupo tena!
 
Taarifa za magazeti zinasema CCM ndio walishikwa na hasira na kuanza kurusha mawe. Ukirushiwa mawe ufanye nini? Jini kwa jino!
 
Wewe unayejiita Mch. hata sikuelewi,wewe kama ni mkwel kwa unayozungumza unaushahidi na hayo malipo ya mtaa wa ufipa? muogope Mungu,kuwa mpambe lakn ujue Mungu anahesabu kila mawazo,maneno na matendo yako!upambe wako usikufanye kuwa muongo ili unogeshe stori na kutetea vitu usivovijua.

Mkuu wengine ni kuwasamehe bure tu.hapo kuna cha uchungaji kweli la bda ni uchungaji wa mshahara.kwanza mchungaji hatakiwi kuwa shabiki wa chama chochote.kazi ya mchungaji ni kumwomba mungu atuchagulie kiongozi bora kutoka chama chochote kwa sababu watu wote ni wake.ukiona mtu anajiita mchungaji halafu anaonyesha ushabiki wa wazi na uwongo kama huu muwekee kiulizo.ndiyo yaleyale ya kina kakobe mungu amemteua mrema kuwa rais mpaka leo hakuna cha urais.wachungaji mjihadhali na uwongo.msidhani kuwa mmesimama kumbe mlishaanguka zamaniiiiiiii.
 
Mbona hakuomba mwongozo kwa mauaji yaliyofanywa na wana ccm kule Arumeru mashariki,Igunga. Kama ana huruma aombe mwongo pia kwa mateso hata mauaji ya nayoendelea kufanywa na chama ambacho yeye ni mweka hazina.Hazina inayohifadhi mabilion ya fedha za EPA kupitia kagoda, hakika fedha hizo zingeokoa maisha ya watoto,akina mama na wagonjwa wengine kwani huduma za afya zingeboreshwa.Mwigulu UPO? OMBA MWONGOZO HUO PIA
 
na ndugu katika bwana wanalipwa hawa pale mtaa wa ufipa ndio maana wao wako masaa 24 humu ndani kwa kazi hizo za kukashifu kutukana na kutetea hata uozo ambao hauteteki na kushabikia kila uongo wanaouanzisha

mnalipwa eeeh!
Endeleeni kujidanganya si mlisema jf ni ya chadema na ninyi mkaanjisha yenu vp wateja hawapo!
Mwaka huu mnakazi sana!
 
Anatafuta kura.

Kwanini hakwenda kulala msibani na asubiri mpaka wazike ndo aje bungeni?
Au kuna baridi sana kipindi hichi?

Yani katika watu walioongea jambo la kufikirika wewe umesema issue ya maana sana ,hivi kweli marehemu kama angekuwa ni mtu wa muhimu kwa mchemba si angekuwa msibani sasa hivi.tena leo bungeni amesema marehemu ni msadizi wake wa karibu.
 
hakuna namba za wabunge wa chadema,kila mtu ana namba yake na lazima itoe jina lake kwa hiyo bila hata kufika polisi spika angeutangazia uma sms alizopewa jina ni la nani na zinasemaje?
na polisi kuanzia hapo wangekuwa na kazi rahisi.
 
mbona wapo wachungaji ambao ni wabunge wa vyama.na kama kakobe alisema mrema ni raisi wa wa tz na kura zikachakachuliwa wewe unajuaje yaliyokuwa yanaendelea kwenye chumba cha kuhesabia kura ? hata wewe jadili mada usijadili watu.
 
Ataka shuhuli za bunge zihairishwe wajadili mauaji yaliyotokea singinda kama jambo la dharura kwa taifa, adai kutishiwa kifo na wabunge wa chadema kwa njia ya sms.
My take: Kweli si si em wamefilisika kisiasa mpaka wanafikia hatua ya kutumia mauaji kama mtaji wao wakisiasa, nahuyu mchemba nawasiwasi na uwezo wake wakufikiri nakupambanua mambo, yaani mgomo wa madactari, namengine mengi yanayo sababishwa na serikali ya CCM hayaoni kuwa na msingi , hili la shabiki wa sisiem aliyepita kwenye mkutano wa CDM tena kuna uwezekano ni wao walimtuma na kupandikiza watu watakao mpiga ili CDM ionekane haifai..sisi wananchi tunaimani na CDM kama mtetezi wa haki zetu wanyonge, pia mkombozi wa rasilimali zetu kutoka mikononi kwa wanyonyaji.

mkuu spika alikubali huo muongozo? maana niko huku mpulungu zambia sina access na runinga.
 
Akiomba muongozo wa spiker Mwigula Mchemba amesema ametishiwa kuuwawa na baadhi ya wabunge wa Chadema kwa kumtumia sms akilinganisha na tukio la kuuwawa kwa kijana wa uvccm iramba.

Hii inaonyesha mwigulu alivo mpumbavu na mjinga tena sana! Kwani kwa kuwa alitishiwa maisha kwa njia ya simu na namba za watuhumiwa anazo na swala lipo polisi amelileta bungeni ili nini?? kwani lilitokea ndani ya bunge? maana hiyo ni jinani iliyotendeka nje ya bunge sasa kulileta bungeni ni kutokujua kanuni na sheria ndio maana nilianza kwa kumtukana maana alipoteza bila sababu muda wa bunge!kujipatia umaarufu wa kijinga! Pili serikali pamoja na vyombo vya dola wanakaa kimya hawachukua hatua zozote dhidi ya kauli na vitendo vya uchochezi kutoka ndani ya ccm hasa kwa makada kama huyu mjinga na Nape nae amekuwa akisema chadema magaidi hachukuliwi hatua huko ni sawa na kukalia bomu kusubiri lilipuke any moment! Lissu alitahadharisha wananchi watachoka na kuanza kuchukua njia za kimapinduzi zilizochukuliwa duniani kote ndicho sasa hivi kinaanza! Machafuko hayaanzi kama vita huanza kwa mtu mmoja wawili kuuawa au kujeruhiwa then kulipa visasi hapo ndio vita kamili inaanza CCM na vyombo vya dola watch out, historia itawahukumu! Lissu alisema kuwa wajukuu wake wakimuuliza atasema "tulisema lakini tulizidiwa nguvu"
 
Hawa mwisho wataomaba mwongozo hata wanapotaka kwenda kujisaidia - mbaffff!
 
Kutokana na tukio lililotokea kwenye jimbo la Iramba Kwa Mwingulu Nchemba kwa mkutano wa CHADEMA kuvamiwa na kikundi cha kihuni cha Mbunge wa Iramba Mwigulu Nchemba na kufanya vurugu zilizopelekea kujeruhiwa kwa watu na hatimaye kuuwawa kwa mfuasi wa CCM, inatoa fundisho kuwa CCM imeamua kutuchokoza na imetangaza vita na CHADEMA! Sasa LIWALO NA LIWE hatutakubali kuonewa wala kunyanyaswa na kikindi cha wahuni! Hizi siasa za Mwigulu ni za kihuni, hatuwezi kuzivumilia! Vyombo vya dola kama police pia vinahusika kwenye hili tukio na sasa wameitengeneza Story eti Viongozi wa CHADEMA ndo walianzisha vurugu kwa kumtukana Mwigulu na wananchi wakakasirika ndo vurugu zikatokea, kamando hivyo hizo mbona hakuna kiongozi wa chama aliyejeruhiwa? Na mbona mkutano uliendelea baada ya vurugu kwa Amani? Kuanzia sasa mikutano yetu tutailinda! LIWALO NA! LIWE,


Huu ulioandika sasa ndio tunaouita ***** na usio na tija bali umepoteza muda wako bure. Kuua muuwe CDM , Mwigulu anahusikaje hapo ? Nyie ni wauaji na sheria ichukue mkondo wake
 
Mi napendekeza zikusanywe hoja zote alizozisema Nchemba toka aingie bungeni halafu mwaka 2015 tuzipeleke kwa wana Iramba kama reference ya kumpigia chini kwa kuwa kazidisha mizaha kuliko kuwatetea wananchi wake wa Iramba
 
hakuna namba za wabunge wa chadema,kila mtu ana namba yake na lazima itoe jina lake kwa hiyo bila hata kufika polisi spika angeutangazia uma sms alizopewa jina ni la nani na zinasemaje?
na polisi kuanzia hapo wangekuwa na kazi rahisi.

Subirini mnyolewe, mnyoaji Mwigulu ameisha wafikia , na ananyoa nywele za aina zote mwilini

 
Mi napendekeza zikusanywe hoja zote alizozisema Nchemba toka aingie bungeni halafu mwaka 2015 tuzipeleke kwa wana Iramba kama reference ya kumpigia chini kwa kuwa kazidisha mizaha kuliko kuwatetea wananchi wake wa Iramba

Mnaua msaidizi wake halafu mnasemaje nyie wauaji ? kusanyeni hizo hoja, na wana iramba jana hizo hoja zetu walizikataa hasira zake mkaamua kuua cdm

 
Mbona hakuomba mwongozo kwa mauaji yaliyofanywa na wana ccm kule Arumeru mashariki,Igunga. Kama ana huruma aombe mwongo pia kwa mateso hata mauaji ya nayoendelea kufanywa na chama ambacho yeye ni mweka hazina.Hazina inayohifadhi mabilion ya fedha za EPA kupitia kagoda, hakika fedha hizo zingeokoa maisha ya watoto,akina mama na wagonjwa wengine kwani huduma za afya zingeboreshwa.Mwigulu UPO? OMBA MWONGOZO HUO PIA

Leteni santuri Mpya, santuri za EPA, nk tumeisha zichoka kutoka midomoni mwenu

 
Back
Top Bottom