Nchemba acharuka bungeni. Ataka kujua ripoti ya mnyika leo bungeni

Kuna tetesi kuwa Dola ya Mabwepande imewapiga stop hawa jamaa kuendesha midahalo. Mwenye data zaidi atujuze

IMG_2378-1024x683.jpg
 
ushahidi wa wizi unakoma miaka mingapi baada ya wizi kufanyika?
sheria inasema anayekutwa na mali ya wizi au aliyeshiriki kutukia mali ya wizi naye ni mwizi na si lazima awepo kwenye eneo la tukio.
wizi wa epa ulivyofanyika hela zake zilisaidia uchaguzi wa ccm na yeye mwigulu alip[okuja kuwa mweka hazina wa ccmaidha aliandika ripoti na kuweka sawa mahesabu pamoja na kulipwa posho sasa ni ushahidi gani wanautaka?
 
Ni jambo ambalo nina uhakika nalo kwanini niliache linyamaziwe kimya. Tuhuma nzito kama hiyo nikiinyamazia nitakuwa wa ajabu sana wakati imetokea nikiwa sio mwajiriwa BOT. KAMA KUNA ZILIZO ACHWA NI HIZO NA SIO MWENDELEZO. KAMA ALITELEZA ASEME KAMA NI UELEWA ASEME LAKINI MIMI NA EPA TUKO MBALI KAMA MBINGU NA NCHI.
 
Ushahidi wa Mnyika usomwe hadharani tupime sisi kama mwigulu alihusika au la!
 
Having gone thru' all comments,I agree with mtoa hoja ya kuwa Mnyika this time ameshikwa pabaya hata sisi wa CDM wenzake tunaliona hilo na ndo maana tunakazana kukumbushia vitu ambavyo vilishapita katika ile hali ya kujipoza na hili ambalo dhahiri limeanza kutuendea kombo,habari za ushahidi wa Lema sijui nani zinatoka wapi katika kipindi hiki....tukubali/tukatae wabunge wengi wa CDM utoto unawasumbua na kuropokaropoka bila mpangilio maalum na kwenyewe ni tatizo kubwa sana.
 
Ni jambo ambalo nina uhakika nalo kwanini niliache linyamaziwe kimya. Tuhuma nzito kama hiyo nikiinyamazia nitakuwa wa ajabu sana wakati imetokea nikiwa sio mwajiriwa BOT. KAMA KUNA ZILIZO ACHWA NI HIZO NA SIO MWENDELEZO. KAMA ALITELEZA ASEME KAMA NI UELEWA ASEME LAKINI MIMI NA EPA TUKO MBALI KAMA MBINGU NA NCHI.

Asante Kaka kwa kuwafafnunulia kuwa tuhuma zako si mwendelezo wa shahidi za kina Lema na nani sijui wanaozipigia debe hapa.
 
Suala la Lema wala msilizungumzie maana lilishatolewa majibu na Spika kuwa, Mbunge anapopoteza Ubunge wake hata kesi zake zinapotea nae. So Ishu ya Lema na Pinda is no longer valid.
 
Ni jambo ambalo nina uhakika nalo kwanini niliache linyamaziwe kimya. Tuhuma nzito kama hiyo nikiinyamazia nitakuwa wa ajabu sana wakati imetokea nikiwa sio mwajiriwa BOT. KAMA KUNA ZILIZO ACHWA NI HIZO NA SIO MWENDELEZO. KAMA ALITELEZA ASEME KAMA NI UELEWA ASEME LAKINI MIMI NA EPA TUKO MBALI KAMA MBINGU NA NCHI.
Is this your 1st post? Au kuna mtu kajisajili kwa jina lako. Nakumbuka kusoma michango yako humu kabla ya huu wa leo. Hapo kwenye red, kushindwa kwa wenyeviti kusimamia mijadala kulichangia kumfikisha Mnyika kutoa kauli ile. Sijui mtu kama Mabumba mlimpa uenyekiti kwa kutumia vigezo gani.
 
Asubuhi hii saa 4 na dkk 10, mh nchemba ameomba muongozo wa naibu spika kuhusu maelezo ya uthibitisho wa yeye kuhusika na EPA. amezungumza huku akionesha hisia kali sana. kasema kuwa wakati wa kashfa ya EPA alikua hajaanza kufanya kazi B.O.T. kasema wapiga kura wake na familia yake imeguswa sana na tuhuma hizi. ameomba kujua maendeleo ya suala hilo kutoka kwa naibu spika. tundu lissu amejaribu kusema kuwa muongozo wa nchemba siyo sahihi lkn naibu spika akamuelimisha lissu kuwa muongoozo haujawekewa ukomo.

ndugai ameomba wabunge wawe makini na kauli zao. "mbunge huwezi kusema kuwa una ushahidi wa jambo fulani kisha ukiombwa ushahidi unapeleka habari za mtaani na ushahidi wa magazeti".

"mnyika alidai kuwa mh nchemba alihusika na EPA. mnyika ameleta ushahidi ambao ni maelezo mafupi. suala hili nalipeleka kwenye kamati ya maadili ya bunge, watapitia ushahidi wa mnyika kisha wote wataitwa kuhojiwa na kamati. matokeo ya kamati tutafahamishwa" alisema ndugai

kwa jinsi lissu alivyokua anababaika, inaelekea MNYIKA SUALA HILI LIMEMKALIA VIBAYA! yetu masikio. tunasubiri taarifa ya kamati.

UCHAMBUZI WANGU
ni dhahiri kuwa ccm wameshapitia ripoti ya mnyika na kuiona haina mashiko. kama ingekua na mashiko, nchemba angezuiwa toka jana na ccm kuzungumzia suala hilo. vile nchemba ameliibua tena leo hii, inaonesha ametumwa na chama chake. ama kweli nchemba amshika mnyika pabaya! mdomo jamani mdomo! mdomo jamani mdomo

Hakuna lolote huyo nchemba anazuga tu hakuna aliyeumia katika jimbo lake wala nini. asitake kusingizia eti wapiga kura wake wameumia, wapiga kura wepi? hao anaochukua wake zao?(refer Igunga case) hana lolote kama ana umia aje kusema humu jamvini tufumue yote yake. anababaika tu kukimbia kivuli chake ( dogo do not be haunted by the same shadow of yourself)
 
Kwa mtazamo wangu hapa ni MNYIKA AISHIKA PABAYA SERIKALI kwa maana fupi tu ni serikali na Nchemba kama wanabisha/anabisha hakuusika na kashfa ya EPA basi sisi kama wananchi tunahitaji kujua fedha zile ziliibwa na nani? zilipelekwa wapi na kwa matumizi gani? na kama zilirudishwa hao waliorudisha ni akina nani? na walichukuliwa hatua gani kwa wizi huo? pia na baada ya kurudishwa zilitumika wapi na zilirudishwa katika akaunti gani? kwa hili Nchemba anapokanusha basi awe na majibu mbadala ni akina nani waliiba kwa sababu alipoingia pale BOT alikuta ripoti na wakati fedha zinarudishwa alikuwepo, hii isiwe janja ya kuchezea akili zetu watanzania.

Sishangai ksbb nimeshawahi kuona pia mfano katika maswali ya True/False swali linalohitaji jibu la True mtu akaandika False.....ndo upeo wake ulipoishia,sasa afanyeje...ndo sawasawa na wewe.
 
Lazima kanuni na utaratibu huu ufuatwe FIRST COMES FIRST SERVED

Kabla ya USHAHIDI wa Mnyika lazima shahidi zilizotangulia tufahamishwe matokeo yake. Ndugai TENDA HAKI. Tunataka Matokeo ya SHAHIDI zifuatazo kwanza
1. Lema v. Pinda (kusema uongo)
2. Magdallena Sakaya v. DCs kuchukua Hongo
3. Zitto v. Baraza la mawaziri kurubuniwa
4. Mnyika v Nchemba kuhusika EPA.

Najua Ndugai huwa unapitia JF

mkuu umesHu ule wa kiwia kupigwa na wanachama wa chama cha.................
 
Pengine hutokea kuwa wameshikwa pabaya! Tatizo la Wabunge wenu wanapenda kubeba habari za kusikia na kuzitamka hadharani. Mbona wakati wa Slaa alikuwa muangalifu wa anachosema?
Tatizo la wabunge vijana wanacheza karata bila kuangalia mbele wakati wenzao wanatafuta weak-point ya kummaliza yoyote
Nasema bado hata Slaa habari za Kontena la kura zilizopigwa tayari huko Mbeya aliletewa na IGP alipoenda hakukuta chochote wakati huo Slaa yuko Igunga sasa bado kuna ukweli hapo au ni kutibuliana mwenzako asitawale
Hii thread ya Mwigulu ipo hapa toka jana na tukawatahadharisha wachangiaji msiwagombanishe wabunge kwani nao ni maMember humu ndani. Leo Ndugai karudia kusema Bungeni kuwa mitandao inahusika kusambaza habari za Mwigulu na EPA bora tuiachie Kamati itaamua km ni adhabu tusilalamike humu JF huenda ikawa ndio chanzo
 
1. Kanuniya 5 (1) ambayo inasema kuwa “katikakutekeleza majukumu yake yaliyotajwa katika ibara ya ya 84 ya Katiba , Spikaataongozwa na kanuni hizi ……….”

2. Kanuniya 63 (2) “ Mbunge yeyote anapokuwa akisema Bungeni hatachukuliwa kuwa anasemauongo iwapo anafanya rejea ya habari kuhusu jambo Fulani lililotangazwa aulililoandikwa na vyombo vya habari”

3. Kanuniya Adhabu : hii ni kanuni ya 73 (3) “Endapo mbunge yeyote atatakiwakuthibitisha ukweli wa jambo au suala alilolisema Bungeni na hadi kufikiamwisho wa muda aliopewa amekataa au ameshindwa kutoa uthibitisho huo,Spikaanaweza kumsimamisha Mbunge huyo kuhudhuria vikao vya Bunge visivyozidi vitano”

4. Kanuniya kupelekwa kamati ya haki, maadili na madaraka ya bunge ni 74(1) “Spikaanaweza kutaja jina la Mbunge kwamba amedharau mamlaka ya Spika na kasha kupelekajina hilo kwenye kamati ya Haki,Maadili na Madaraka ya Bunge…..”
 
Asubuhi hii saa 4 na dkk 10, mh nchemba ameomba muongozo wa naibu spika kuhusu maelezo ya uthibitisho wa yeye kuhusika na EPA. amezungumza huku akionesha hisia kali sana. kasema kuwa wakati wa kashfa ya EPA alikua hajaanza kufanya kazi B.O.T. kasema wapiga kura wake na familia yake imeguswa sana na tuhuma hizi. ameomba kujua maendeleo ya suala hilo kutoka kwa naibu spika. tundu lissu amejaribu kusema kuwa muongozo wa nchemba siyo sahihi lkn naibu spika akamuelimisha lissu kuwa muongoozo haujawekewa ukomo.

ndugai ameomba wabunge wawe makini na kauli zao. "mbunge huwezi kusema kuwa una ushahidi wa jambo fulani kisha ukiombwa ushahidi unapeleka habari za mtaani na ushahidi wa magazeti".

"mnyika alidai kuwa mh nchemba alihusika na EPA. mnyika ameleta ushahidi ambao ni maelezo mafupi. suala hili nalipeleka kwenye kamati ya maadili ya bunge, watapitia ushahidi wa mnyika kisha wote wataitwa kuhojiwa na kamati. matokeo ya kamati tutafahamishwa" alisema ndugai

kwa jinsi lissu alivyokua anababaika, inaelekea MNYIKA SUALA HILI LIMEMKALIA VIBAYA! yetu masikio. tunasubiri taarifa ya kamati.

UCHAMBUZI WANGU
ni dhahiri kuwa ccm wameshapitia ripoti ya mnyika na kuiona haina mashiko. kama ingekua na mashiko, nchemba angezuiwa toka jana na ccm kuzungumzia suala hilo. vile nchemba ameliibua tena leo hii, inaonesha ametumwa na chama chake. ama kweli nchemba amshika mnyika pabaya! mdomo jamani mdomo! mdomo jamani mdomo

TUTAONA MWISHO WAKE.:A S-baby:
 
Nimejaribu kuonyesha ukiukwaji mkubwa wa kanuni kama ulivyofanywa leo na Ndugai , hakika Bunge likiendeshwa kwa mtindo huo linaelekea kuzimu kabisa.
 
ninaboreka sana na uendeshaji wa bunge la sasa... halina mvuto kabisa manake wakati wowote unakuwa unategemea upendeleo... hadi naona ishakuwa kama kawaida... bunge lilikuwa lile la Sita bana.... hili ni upuuzi mtupu.. huyo sijui ndugai kakaa kizaramo sana (mtanisamehe ndugu zangu wazaramo sio lengo langu ni maudhi tu ya hapa na pale!) Akiongea mbunge wa upinzani tusi.... wa ccm sawa... inaboa.... naomba huyo ndugai atambue kwamba anaboa... tena kwa sasa anamzadi hata bi kiroboto.
 
Nchemba hajatulia....Anapenda sn misifa!

na wapenda sifa huwa ni malimbukeni au hivyo wanavyojivunia navyo ni vya kubahatisha ndio maana wanataka ulimwengu ujue kama ni vya kawaida ungewakuta wapo poa tu
huyu limbukeni,mshari,mpenda uswahili wa kupashana bila adabu wala busara hana jipya
watu kama hawa ukiwa hutaki kupoteza muda ni wa kupuuza ama kuwaumbua misifa yote huisha
 
Back
Top Bottom