Nchemba acharuka bungeni. Ataka kujua ripoti ya mnyika leo bungeni

wakuziba

Senior Member
Jun 24, 2012
123
43
Asubuhi hii saa 4 na dkk 10, mh Nchemba ameomba muongozo wa naibu spika kuhusu maelezo ya uthibitisho wa yeye kuhusika na EPA. amezungumza huku akionesha hisia kali sana.

Kasema kuwa wakati wa kashfa ya EPA alikua hajaanza kufanya kazi B.O.T. kasema wapiga kura wake na familia yake imeguswa sana na tuhuma hizi. Ameomba kujua maendeleo ya suala hilo kutoka kwa naibu spika. Tundu Lissu amejaribu kusema kuwa muongozo wa Nchemba siyo sahihi lkn naibu spika akamuelimisha Lissu kuwa muongoozo haujawekewa ukomo.

ndugai ameomba wabunge wawe makini na kauli zao. "mbunge huwezi kusema kuwa una ushahidi wa jambo fulani kisha ukiombwa ushahidi unapeleka habari za mtaani na ushahidi wa magazeti".

"Mnyika alidai kuwa mh nchemba alihusika na EPA. Mnyika ameleta ushahidi ambao ni maelezo mafupi. suala hili nalipeleka kwenye kamati ya maadili ya bunge, watapitia ushahidi wa Mnyika kisha wote wataitwa kuhojiwa na kamati. matokeo ya kamati tutafahamishwa" alisema ndugai

kwa jinsi lissu alivyokua anababaika, inaelekea MNYIKA SUALA HILI LIMEMKALIA VIBAYA! yetu masikio. Tunasubiri taarifa ya kamati.

UCHAMBUZI WANGU
Ni dhahiri kuwa CCM wameshapitia ripoti ya Mnyika na kuiona haina mashiko. kama ingekua na mashiko, Nchemba angezuiwa toka jana na CCM kuzungumzia suala hilo. Vile Nchemba ameliibua tena leo hii, inaonesha ametumwa na chama chake. Ama kweli Nchemba amshika Mnyika pabaya! Mdomo jamani mdomo! mdomo jamani mdomo
 
Mbona mengine wanayo tuhumiwa hawakazanii ushahidi?
Huyu Mchemba ni misifa sana.

Aishie huko hawezi kushindana na Jembe Mnyika katika hoja
 
Dah!ila kitendo cha Nchemba kujioneshea kidole kichwani kama ishara ya kusema ana akili sana...ivi Nchemba anaamini ana akili kuliko watu wote??ameniboa kwa ishara kila akijiangalia akiona kamera inammulika anaonyesha ishara kuwa "Nina akili sana" ....mshamba sana uyu jamaa
 
I am just curious to know the outcome of this saga!! kama kweli wako serious na miongozo, wauweke hadharani ushahidi wa Lema dhidi ya waziri mkuu kusema uongo. Otherwise, tutarudi kule kule tunakowaweka magamba wote!
 
Nchemba bado ana-behave kama mwanafunzi wa sekondari. Utoto mtupu.
Haya report zote sasa ziwekwe mezani kuanzia ile ya Lema, Zitto na wengine. Fair game!
 
Dah!ila kitendo cha Nchemba kujioneshea kidole kichwani kama ishara ya kusema ana akili sana...ivi Nchemba anaamini ana akili kuliko watu wote??ameniboa kwa ishara kila akijiangalia akiona kamera inammulika anaonyesha ishara kuwa "Nina akili sana" ....mshamba sana uyu jamaa
Inasemekana jamaa alinyonya hadi miaka 5
 
Lazima kanuni na utaratibu huu ufuatwe FIRST COMES FIRST SERVED

Kabla ya USHAHIDI wa Mnyika lazima shahidi zilizotangulia tufahamishwe matokeo yake. Ndugai TENDA HAKI. Tunataka Matokeo ya SHAHIDI zifuatazo kwanza
1. Lema v. Pinda (kusema uongo)
2. Magdallena Sakaya v. DCs kuchukua Hongo
3. Zitto v. Baraza la mawaziri kurubuniwa
4. Mnyika v Nchemba kuhusika EPA.

Najua Ndugai huwa unapitia JF
 
Lets Assume kuwa hiyo kamati ya nidhamu ikamtia hatiani Mnyika what will be the worse Scenario? CCM udhibitisho huo wa mnyika utafuta madhambi yenu yote?
 
Mkuu u mean FIFO aijazingatiwa hapa?
 
Dah!ila kitendo cha Nchemba kujioneshea kidole kichwani kama ishara ya kusema ana akili sana...ivi Nchemba anaamini ana akili kuliko watu wote??ameniboa kwa ishara kila akijiangalia akiona kamera inammulika anaonyesha ishara kuwa "Nina akili sana" ....mshamba sana uyu jamaa

Nilikuwa na muheshimu sana Ndugai lakini kumbe na yeye ni dhaifu
 
Inaweza kuwa ngumu kwa Mnyika kuthibitisha uhusika wa Nchemba lakini sitategemea kuona Ushahidi ukisomwa mbele ya wabunge. Haya yanawezekana;

a) Kwa kutoridhisha kuwa Nchemba amehusika, Mnyika atakuwa amesema uongo na atakuwa suspended. Hatakiwi mjengoni!
b) Jambo hili kuachwa bila adhabu yoyote kwa Mnyika lakini ikasemwa kuwa ushahidi ni dhaifu. Hofu itakuja kwa wabunge wa Chadema kudai maelezo ya Lema na Zitto yatolewe na adhabu kwa wahusika itolewe kwa kipimo sawa na atachopewa Mnyika.

Kwa mbali naona jambo hili litapita tu kama yalivopita EPA, Richmond, Dowans na washirika wake!! Kumbukeni EPA ni moja ya sehemu ambapo CCM hataki kurudi! Na namna ya kutorudi ni kumaliza mambo kimya kimya. Naichukulia hii kama "case closed". Nitashangaa nikisikia hata hiyo taarifa ya Kamati ya Nidhamu, achilia mbali adhabu kwa Mnyika.
 
Wakati mwingine mtaniona mbaya kwa kusema ukweli,ripoti ngapi za ushahidi wa wabunge wa CDM hausomwi wala kujadiliwa na kupewa majibu? uzembe ni wa wabunge wetu wa CDM pia! kwanini hawashinikizi ushahidi wao kufanyiwa kazi kama anavyokomaa Nchemba? Nafikiri spirit ya wabunge wa CDM imeshuka sana,hawawajibiki kama mwanzo walivyoingia bungeni.wanatakiwa wawe aggressive wasisikilize propaganda za CCM kuwapoza!
 
wakuziba
Wait a minute, unaposema lissu anababaika unamaanisha nini? Lissu amesema kuwa Mnyika tayari amepeleka maelezo (ushahidi) ofisi ya bunge..

Sambamba na hilo Lissu alilenga kumkumbusha Nchemba kuwa kanuni ya 68 aliyoitumia inapaswa kutumika kuomba kuomba mwongozo kwa jambo linalozungumzwa na sio lililokwisha zungumzwa.

Wakati ukitafakari hayo ukumbuke naibu spika yuko pale kwenye kiti kutetea upande upi.
 
Last edited by a moderator:
524018_199190553541959_1808874647_n.jpg
 
Lets Assume kuwa hiyo kamati ya nidhamu ikamtia hatiani Mnyika what will be the worse Scenario? CCM udhibitisho huo wa mnyika utafuta madhambi yenu yote?

tumia akil yko vizuri unapoandika. mtu kusema uongo bungeni, kama ni muadilifu anafaa kujiuzulu. pale hatupeleki watoto ambao hata hawajui familia inaendeshwa vipi. kupayuka na kubwabwaja si mahala pake bungeni. ataendelea kuwa mbunge lkn wanaomuamin watapungua! hadhi yake itashuka. vile na wewe bado unalishwa hujui majukumu ni nini huwezi kuelewa maana ya hadhi katika jamii.
 
Mahakama ya bunge!!! Mhhhh!!!
ONLY THE FIT OF THE FITEST WILL SURVIVE.
 
tumia akil yko vizuri unapoandika. mtu kusema uongo bungeni, kama ni muadilifu anafaa kujiuzulu. pale hatupeleki watoto ambao hata hawajui familia inaendeshwa vipi. kupayuka na kubwabwaja si mahala pake bungeni. ataendelea kuwa mbunge lkn wanaomuamin watapungua! hadhi yake itashuka. vile na wewe bado unalishwa hujui majukumu ni nini huwezi kuelewa maana ya hadhi katika jamii.

  1. Red umetumia yako wakati unaandika?
  2. Green auna ukweli au ushaidi wa kimantiki.
  3. Blue Usimtukane usiyemjua yaweza kuwa ni mmoja kati ya wanaosababisha wewe kupata mahitaji yako ya msingi
 
Inaweza kuwa ngumu kwa Mnyika kuthibitisha uhusika wa Nchemba lakini sitategemea kuona Ushahidi ukisomwa mbele ya wabunge. Haya yanawezekana;

a) Kwa kutoridhisha kuwa Nchemba amehusika, Mnyika atakuwa amesema uongo na atakuwa suspended. Hatakiwi mjengoni!
b) Jambo hili kuachwa bila adhabu yoyote kwa Mnyika lakini ikasemwa kuwa ushahidi ni dhaifu. Hofu itakuja kwa wabunge wa Chadema kudai maelezo ya Lema na Zitto yatolewe na adhabu kwa wahusika itolewe kwa kipimo sawa na atachopewa Mnyika.

Kwa mbali naona jambo hili litapita tu kama yalivopita EPA, Richmond, Dowans na washirika wake!! Kumbukeni EPA ni moja ya sehemu ambapo CCM hataki kurudi! Na namna ya kutorudi ni kumaliza mambo kimya kimya. Naichukulia hii kama "case closed". Nitashangaa nikisikia hata hiyo taarifa ya Kamati ya Nidhamu, achilia mbali adhabu kwa Mnyika.

kweli mkuu magamba hawataki kuumbuka zaidi na hiyo kesi wataipotezea kimya kimya.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom