ntogwisangu
JF-Expert Member
- Nov 25, 2011
- 524
- 164
Ingawaje siungi mkono kuvuliwa uanachama kwa baadhi ya wanachama na viongozi wa chama cha NCCR,lakini nimefurahishwa na ule uthubutu wa kuchukua maamuzi magumu ambayo ndugu zangu wa CCM wamekua wagumu kuyachukua.
Kuchuka maamuzi magumu kunaleta nidhamu katika kazi.Watendaji wa serikali pamoja na vyama vyote vya siasa,kama kila mmoja angekua anatimiza wajibu wake,na wale wenye mamlaka wakawawajibisha wanaoenda kinyume na taratibu,nina uhakika kuwa Tanzania ya leo ingekua ni ile nchi ya asali na maziwa tunayoitamani.
Naomba tuichukulie NCCR kama mfano na tuanze kubadilika tuchukue maamuzi magumu katika kuwajibishana.
maamuzi haya ccm wanayochombeza katika vyama vya upinzani wanapaswa kuyafanya wao katika kusukuma mbele gurudumu la taifa!!otherwisw watanzania wote tuna laana!!!