NCCR yameiva: Kafulila kuvuliwa uanachama Jumamosi!

zetu.bora mtu awe kama shibuda tujuwe moja kuliko unafki wa kishe..... Wanajidai wanaharakati kumbe wezi tu.
 
Kama tunadai Katiba Mpya ni lazima tudai Katiba Mpya ndani ya Vyama vyetu vya upinzani ambapo viongozi wete hawako tayari kukosolewa!! Ni dhahiri kwamba , JEMUS MBATI NI CCM na sasa anatekeleza Kazi ya CCM kuwaondoa Wapinzani Bungeni!!!


Hata kama JEMUS MBATIA atahonga Wajumbe Wa Halmashauri Kuu yote ,Kwa Lengo la Kumuondoa Kafulila hawezi kumuhonga MUNGU ambaye yupo Mbioni KUIONDOA CCM Madarakani ambaye ni mungu wa JEMUS MBATIA.

Hakuna Shaka kuwa Wananchi tunataka Wapinzani imara Bungeni wenye mtazamo wa kuhoji maswala ya Wizi wa CCM na viongozi walioko Serikalini!!
Hata hivyo suala linalo endelea katika Vyama vya Upinzani kwa sasa ni migogoro ambayo inafanya wezi wa rasilimali wafurahie.

Mtazamo wangu kwa hili ni Kwamba mtu PASIPO HAKI HAPANA AMANI na Jemus Mbatia Hawezi kutafuta amani Kwa Kumuondoa kafulila bali ajitazame kama tuhuma anazosema Kafulila ni za kweli bila kujali kibarua cha CCM. Leo Utamuondoa Kafulila Kesho utaondolewa wewe kwani ni vigumu sana kumutetea Mharifu!!!

Umenena vema mkuu.
 
Kafulila akalia kuti kavu NCCR Send to a friend
Wednesday, 14 December 2011 21:21
0digg

kafulilachangia.jpg
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi),David Kafulila

Fidelis Butahe na Aidan Mhando
MBUNGE wa Jimbo la Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila, ambaye Desemba 8 mwaka huu alienguliwa katika nafasi ya ukatibu mwenezi, huenda akavuliwa uanachama. Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa mbali na kuvuliwa wadhifa huo, mbunge huyo, sasa anakabiliwa na hatua nyingine ngumu zaidi kisiasa, baada ya uongozi wa chama hicho kutaka kumvua uanachama.

Kwa mujibu wa habari hizo, hatua hiyo imepangwa kufikiwa Jumamasi hii, wakati Halmashauri Kuu ya chama hicho itakapoketi kwa dharura jijini Dar es Salaam kujadili mambo mbalimbali ikiwamo, suala la Kafulila. Katibu mkuu wa NCCR Mageuzi Samwel Ruhuza alithibitisha jana maandalizi ya kikao hicho cha dharura lakini, akasema agenda zake hazijapangwa.

"Ni kweli Halmashauri kuu imeitishwa kwa dharura Jumamosi hii jijini Dar es Salaam na baadhi ya wajumbe wameanza kufika," alisema Ruhuza na kuongeza: “Mkutano utafanyika keshokutwa (Jumamosi) lakini bado hatujapanga eneo tutakapofanyia. Tukipanga tutawajulisha waandishi wa habari,” alisema Ruhuza. Alipoulizwa iwapo moja ya ajenda za mkutano huo ni kumjadili Kafulila, katibu mkuu huyo alisema kwamba hawezi kulizungumzia suala hilo sasa hadi muda mwafaka utakapowadia. Chanzo cha habari ndani ya chama hicho kimeeleza kuwa kanuni za nidhamu na usuluhishi za NCCR ukurasa wa 49, jedwali la saba kipengele cha kwanza na cha pili, zinaonyesha kuwa Kafulila anaweza kutimuliwa uanachama na huo baada ya kuondolewa uongozi.

Kwa mujibu wa chanzo hicho "Mtu yoyote anayetoa siri za chama nje ya vikao kama ni mara ya kwanza atapewa karipio kali au kuvuliwa uongozi na endapo akirudia mara ya pili, anavuliwa uanachama." Vyanzo zaidi vilidokeza kwamba ni kosa kwa mwanachama kumtuhumu kiongozi au mwanachama mwenzake kupitia vyombo vya habari (nje ya vikao vya chama) na kwamba, kufanya hivyo ni sawa na kukihujumu chama.
“Kafulila alitakiwa kupingana na Mbatia (Mwenyekiti) ndani ya vikao vya chama na siyo katika vyombo vya habari na sio yeye tu, wale wote waliohusika kufanya jambo hilo nao watahusishwa”, kilisema chanzo hicho na kuongeza: “Suala hili karibu litafikia tamati na kumaliza mvutano ndani ya chama; Kafulila kavunja kanuni nyingi za chama sijui itakuwaje ngoja tusubiri uamuzi.”

Kauli ya Ruhuza Awali, akizungumza na gazeti hili Ruhuza alisema hawezi kuzungumza mambo ya ndani ya chama kwa kuwa kwa kufanya hivyo naye atakuwa amevunja kanuni na taratibu za chama. “Ninachoweza kuhoji ni kitendo cha Kafulila kuzungumza na vyombo vya habari juu ya barua niliyompa, kulikuwa na ulazima gani wa kuzungumza habari hizo?,” alihoji Ruhuza.

Alisema barua hiyo alimuandikia tangu Desemba 8 mwaka huu, lakini iweje taarifa za yeye (Kafulila) kuvuliwa uongozi zianze kuibuka baada ya kukabidhiwa barua hiyo. “Nashindwa kuelewa amezipeleka katika vyombo vya habari kwa mtizamo gani, mimi ningeweza kuwaita waandishi na kuwaeleza suala hilo lakini niliona halina maana yoyote,” alisema Ruhuza. Ruhuza alisema kutokana na madaraka aliyopewa kikatiba, anaweza kuteua wajumbe wa Sekretarieti au kuwaengua bila kushauriana na mtu yoyote.
“Nina mpango wa kuiboresha hii idara (Uenezi) ili kuipa makali, atakapoteuliwa mtu mwingine wa kuziba nafasi hiyo vyombo vya habari vitaelezwa,” alisema Ruhuza Alipoulizwa kuhusu hatma ya Kafulila, alisema suala hilo hawezi kulizungumza bali linaweza kujadiliwa katika vikao vya ndani vya chama. Mbatia Akizungumza na Mwananchi Mbatia alisema hawezi kuzungumza masuala ya utendaji wa chama katika vyombo vya habari na kutaka atafutwe Katibu Mkuu, ili alizungumzie suala hilo.

“Mambo ya chama siyazungumzi katika vyombo vya habari nayazungumza katika vikao vya chama na nikifanya hivyo, nitakuwa nimekwenda nje ya kanuni na taratibu za chama,” alisisitiza Mbatia. Kauli ya Kafulila Kwa upande wake Kafulila alisema anachofahamu ni kwamba, mkutano wa Nec utakutana Februari 3, mwaka 2012 na katika mkutano huo, Mbatia ndiye atatakiwa kutoa maelezo ya ajenda iliyoibuliwa katika mkutano wa Nec uliofanyika Novemba 5 mwaka huu kama ni mpinzani ama kibaraka wa CCM.

“Wajumbe wa Nec walionyesha kutokuwa na imani na Mbatia tangu mkutano wa Nec wa mwezi uliopita, na walimtaka awasilishe utetezi wake kwa Katibu Mkuu , utetezi ambao utajadiliwa katika kikao cha mwakani,” alisema Kafulila. Alipoulizwa kuhusu kuzungumza mambo ya ndani ya chama katika vyombo vya habari Kafulila alihoji, “Mambo gani hayo ninayozungumza na vyombo vya habari? Chama ni vikao kaka, wewe muulize Ruhuza kama Mbatia ameshawasilisha utetezi wake”.

Kutokana na hali hiyo huenda mkutano huo ukaibua sura mpya ndani ya chama hicho kutokana na kwamba kuna baadhi ya wajumbe walionyesha kutokuwa na imani na Mbatia tangu katika mkutano wa NEC ulimalizika hivi karibuni.
Katika hatua nyingine Ruhuza amesema hali ya siasa ndani ya chama hicho sasa ni shwari na kwamba kitaendelea kuwashughulikia wanachama wake wanaoonekana kuwa ni kikwazo kwa kutengeneza makundi yenye lengo la kukibomoa. Alisema kuenguliwa kwa Mbunge huyo ni adhabu tosha na kwamba chama hicho kitaendelea kufanya mabadiliko makubwa ya uongozi.

Alisema chama cha NCCR ni chama kikongwe hapa nchini na kwamba wanataka kukijenga ili kiwe imara ndio mana wameamua kufanya mabadiliko ya uongozi ndani ya chama na kwamba kwa kuanzia wameanza katika nafasi ya Katibu Uwenezi kwa kumuondoa katika nafasi hiyo. “Chama chetu hakiwezi kuyumbishwa na watu wachache na kwamba tumeamua kufanya mabadiliko ambayo sasa tunatengua baadhi ya vitengo ndani ya chama na kuweka uongozi mpya ambao utawezesha kuinua chama,” alisema Ruhuza.

Aidha Ruhuza alifafanua kwamba kutokana na kazi ya ukatibu Uwenezi ndani ya chama kuhitaji muda mwingi kutekeleza majukumu yake ya kazi wameamua kumuondoa Mbunge huyo katika nafasi yake iliaweze kupewa mtu ambae atafanya kazi hiyo kwa muda wote wa kazi.
“Kama unavyo fahamu Kafulila ni Mbunge na anamajukumu mengi katika jimbo lake sasa hatuwezi kuendelea na nafasi hiyo ambayo inahitaji mtu wa kufanya katika muda wote wakazi ndio mana tumeamua kumpumzisha,” alisema Hata hivyo Katibu Mkuu huyo alisema suala la Kafulila sasa limekwisha na haipaswi tena kulizungumzia kwa sababu tayari chama kimeshatekeleza majukumu yake kwa kufuata Katiba ya chama hicho
 
that's why i hate party politics..... Yaani kila ufanyalo liendane na maslahi ya chama.. Hapa ndo tunapokwa ia
 
Jemus mbatia unatuonyesha ni kwa jinsi gani wewe ni CCM..hv kuna kazi gani unafanya apart frm Politics
 
Jemus mbatia unatuonyesha ni kwa jinsi gani wewe ni CCM..hv kuna kazi gani unafanya apart frm Politics
Hana kazi yeyote huyo anawategemea dada zake waliopo ulaya wamtumie pesa na pia wife wake ana kazi nzuri pale nssf!
 
Kitakachoumaliza upinzani nchi hii ni hii tabia ya viongozi wote ndani ya vyama hivi kuwa na "SHARUBU" kama kambale. Angalau viongozi wa vyama wangekuwa wanaapa kuzilinda na kuzitetea KATIBA za vyama vyao. Chama ni VIKAO. Maamuzi yote yafanywe na vikao. Kauli, maoni, matamshi yote yatolewe ndani ya vikao vya ngazi husika. Baadhi ya viongozi au wanachama wanapodhani wao ni maarufu kuliko vyama hivi ndipo taabu inapoanzia.
 
hata mimi naanza kuwa na doubt na kaka Kafulila, kila sehemu anapoelekea yanatokea ya kutokea! jipange kaka karibu tena chadema
 
Cha msingi ni kwamba wakishamvua, basi jimbo la Kafulila linarudi CHADEMA. Peoples power
 
kazi yake ni Uenyekiti wa NCCR-Mageuzi, ndio maana kakaa pale zaidi ya miaka kumi na moja na hataki kuondoka. analipwa na CCM kwa jitihada za kuudhoofisha upinzani ili CCM iendelee kuwa madarakani. Project yake ya sasa ni kuhakikisha jimbo la Kawe na Kigoma kusini yanarudi CCM kwa kumuondoa Mh. Mdee kwa kesi na Kafulila kwa kumnyang'anya kadi ya uanachama wa NCCR-Mageuzi. Pia inasemekana alimpa Mkosamali wakili aliyefremu kesi yake vibaya, hivyo yaelekea Mkosamali akashindwa kesi ya kupinga ushindi wake mahakamani iliyofunguliwa dhidi yake na aliyekuwa mgombea wa CCM, ndio maana kuna wakati alikuwa akitishia kuwa atahamia CHADEMA. Hivyo hayo ndio madili na kazi za James mwana wa Mbatia, Injinia ambaye hajawahi practice kazi alosomea na dependant na mvivu wa kufanya kazi bali anaishi kwa fitina za siasa.

From what I know James Mbatia HAKUIHITIMU chuo kikuu. Kwahiyo labda kama kasomea ukubwani miaka ya karibuni. Kama nimekosea nisahihishwe
 
HASHIMU RUNGWE AMESEMA JEMUS MBATIA NI KIBARAKA WA CCM NA NI DIKITETA Mgombea wa Urais Mwaka 2010 Hashimu Rungwe amesema Jemus Mbatia ni Kibaraka wa CCM, kwa kuwa wakati wa Uchaguzi alimwambia yeye kama mgombea wa Urais asimushambulie sana Mgombea wa CCM Jakaya Mrisho Kikwete bali afanye hivyo kwa Mgombea wa Chadema Dr. Wilbroad Slaa. Kauli hiyo ya Mbatia ilimusababisha Rungwe ambaye ni Mwanasheria Kitaluma Kumwamwandia barua Mbatia Kutaka Ufafanuzi Zaidi, Lakini Mbatia Huyohuyo amepanga kumufukuza Uanachama. Tayari Rungwe amesha tangaza nia ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti Taifa NCCR kumutoa Mbatia!!! Rungwe anasema Mbatia anaendesha NCCR kidikiteta kwa Maongozo ya CCM na hataki Mawazo ya Upinzani kujenga Chama kwa maslahi ya Taifa. Anasema Mbatia ni injinia wa maji kitaluma lakini hataki kufanya kazi ya taluma yake kama yeye anavyofanya kazi ya uwakili na kuchangia NCCR . Anasema akina Prof. Lipumba ni Wanataluma , akina Tundu lisu ni wanataluma, Akina Mabere Marando ni Wanataluma, lakini wote pamoja na kutumikia vyama vyao wanafanya shughulin za taaluma zao na kujipatia fedha zinazo inua vyama vyao. Sasa tatizo la Mbatia hajawahi kufanya shughuli yoyote ya taluma yake tangia apate nafasio ya uenyekiti lakini amekuwa na matumizi makubwa katika chaguzi mbalimbali ambazo wakati wote wa kampeni amekuwa akiwataka Wana NCCR kutowasema vibaya CCM na viongozi wake ambao ni wafadhili wake!!! .Tatizo la Mbatia ni kukaa kijiweni makao makuu na kutaka anyenyekewe kama mungu mtu na hata anapohitaji pesa kutaka kwa wabunge anafanya hivyo kwa udikiteta na wanapo mhoji anawajengea Chuki na kupanga njama za Kuwavua uongozi kabla ya kunyang'anya kadi za uanachama. Yupo Mbunge ambaye amemkopesha pesa zaidi ya 80m ambaye kwasasa ndiye silaha yake!!!. Mbatia ni Mshamba anadai yeye ni Mhandisi wa Maji Mbona hatumuoni akifanya kazi ya Uhandisi Wa Maji??. Hashimu Rungwe amemtaka Mbatia kujipanga na kunandaa Ushahidi kwenye kikao cha feb,2012 na sio kuendesha udikiteta na mbinu za kitoto za kuwafukuza wanao daui haki ya kugombea NCCR






 
From what I know James Mbatia HAKUIHITIMU chuo kikuu. Kwahiyo labda kama kasomea ukubwani miaka ya karibuni. Kama nimekosea nisahihishwe
Mbatia alifukuzwa UDSM na baada ya kukubali kuwatumikia CCM alikwenda kusoma nje ya nchi!!!
 
Kama habari hii ni ya kweli, si habari njema kwa mustakabali wa upinzani endelevu unaojiandaa kushika dola 2015. Kafulila naye ni muhimu atafute jinsi ya kuchukuliana na viongozi wake, hata kama wanaonesha aina fulani ya udhaifu kiuongozi - kama kweli upo.

Pamoja na mapungufu ya Mbatia, lakini naona kama Kafulila ana matatizo zaidi. Kiongozi mzuri anajua jinsi ya kuzicheza karata zake, ili kufikia malengo yake. Lakini huyu anaonekana kuzibwaga tu, then watu wanamuona mwehu...
 
that's why i hate party politics..... Yaani kila ufanyalo liendane na maslahi ya chama.. Hapa ndo tunapokwa ia
never trust ANY politician. Don't ever put your trust in a man! All you will get is disappointments!
 
Back
Top Bottom