NCCR yakosoa Wahariri kwa kukurupukia Maandamano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NCCR yakosoa Wahariri kwa kukurupukia Maandamano

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Habarindiyohiyo, Oct 29, 2008.

 1. H

  Habarindiyohiyo JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2008
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wakati huo huo, mwandishi wetu Hilary Komba, anaripoti kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Oganaizesheni, Kampeni na Uchaguzi ya NCCR-Mageuzi, Bw. Faustin Sungura, alisema wahariri hawakupaswa kuandamana bila kwanza kujiridhisha iwapo habari iliyosababisha gazeti kufungiwa ilifuata maadili ya kitaaluma na kwamba ilikuwa ya kweli.

  "Maandamano ya wahariri hayakutakiwa kufanyika kabla ya kufanyika uchunguzi wa kina, kwa sababu kwa sasa kuna baadhi ya watu wamejitokeza wanataka kulishitaki gazeti hilo sasa kama litaonekana lina hatia mahakamani basi wahariri watajiweka katika nafasi mbaya," alisema Bw Sungura.

  Kwa maoni yake, alisema wahariri wameharakisha kuandamana kabla hata ya kufanya uchunguzi kwani inaweza kuwashushia hadhi yao, ambayo ni muhimu katika Taifa ambalo linawahitaji kwa kazi zao.

  Alisema wahariri wana haki ya kuandamana kama haki zao zikiwa zimekiukwa kama kufungiwa magazeti, lakini wanapaswa kufahamu kuwa jambo wanalodai lazima liwe limefanyiwa kazi kwanza.

  Aliongeza kuwa iwapo ingebainishwa kwanza ukweli wa habari hiyo, hata chama chake kingekuwa tayari kushirikiana kwa karibu zaidi kupinga hatua iliyochukuliwa ya kulifungia gazeti la MwanaHALISI.

  Nacho Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kiliunga mkono maandamano hayo katika ilichokiita salamu zake za mshikamano kwa wanahabari nchini zilizotolewa jana na Mkurugenzi wa Vijana wa Chama hicho, Bw. John Mnyika.

  "Tunawapongeza wahariri kwa mshikamano wenu katika kipindi hiki cha majaribu; endeleeni kusimama pamoja, ni umoja wenu ndio utakaokuwa kinga ya pamoja dhidi ya mtu au chombo chochote kinachoingilia uhuru wenu.

  "Mshikamano wenu ni ishara ya kushindwa kwa mkakati wa ‘wagawe uwatawale’ na imani kwamba umoja ni nguvu. Wahariri wote hawapaswi kukaa kimya kuhusu kufungiwa kwa MwanaHALISI, kwa kuwa leo ni kwa gazeti hilo, kesho itakuwa kwa gazeti lingine; hivyo ni vyema kuungana kulinda uhuru, taaluma na sekta ya habari," alisema.

  Chama hicho kililaumu jinsi hatua hizo zilivyochukuliwa kwa kusema ni sawa na Serikali kuamua kesi ambayo yenyewe ndiyo ilikuwa imelalamika.

  "Hatua ya Waziri mwenye dhamana na sekta ya habari kugeuka mlalamikaji, mwendesha mashitaka na mfungaji ni mwelekeo mbovu wa kupuuza taasisi za kusimamia uwajibikaji na haki.
  "Uamuzi uliofanywa na Serikali hauna tofauti na unaofanywa na raia wanaojichukulia sheria mikononi(mob justice).

  "Kwa Serikali inayoheshimu misingi ya asili ya haki, tulitarajia chombo chochote cha habari, kikivunja sheria ama kukiuka maadili dhidi ya serikali, viongozi wake ama watu binafsi mashitaka au malalamiko yangepelekwa kwa taasisi zinazohusika mathalani Baraza la Habari (MCT) au Mahakama," aliongeza.

  Chanzo: Udokozi toka MAJIRA
   
 2. P

  Paparazi Muwazi JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2008
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kahangwa

  Huu ndio msimamo wa chama chenu au ni maoni binafsi tu ya Bwana Sungura? Nini maoni yako kuhusu kufungiwa kwa gazeti la MwanaHALISI?

  PM
   
 3. George Kahangwa

  George Kahangwa Verified User

  #3
  Oct 29, 2008
  Joined: Oct 18, 2007
  Messages: 539
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Mkuu PM,
  Kwanza kabisa naomba utimize ahadi yako ya jana tafadhali, pengine kwa kufanya hivyo tutapata fursa ya kutafakari kwa pamoja suala la kufungiwa kwa MwanaHALISI. Ninachoweza kukueleza kwa ufupi kuhusu kufungiwa huku, ni kwamba hilo limekuwa sehemu ya kilele cha kuandamwa kwa muda mrefu kwa chombo hiki na waandishi wake, nadhani makala moja tu ya kutaja njama za kumzuia Kikwete 2010 sio sababu pakee ya kufungiwa huku, kuna mengi nyuma ya pazia.

  Sijaongea na Sungura kujua ni nini hasa alichokisema na kwa nini alisema hivyo, kwa idhini ya chama au nafsi yake. Binafsi sikubaliani naye, lakini natambua anayo haki ya kutoa maoni binafsi . Ukitaka kujua kama huo ni msimamo wa chama au la, tafadhali wasiliana na Katibu Mkuu.
   
 4. P

  Paparazi Muwazi JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2008
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35

  Nashukuru kwa ufafanuzi. Niko Dodoma kikazi, nitarejea baada ya kipindi cha Bunge na kupita UDSM kukuona.

  Naomba namba ya Katibu Mkuu nifanye nae mahojiano kwa simu kupata msimamo wa NCCR

  PM
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  Oct 29, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Bwana Sungura alitakiwa kusoma tamko la wahariri. Walichosema (kama nimewaelewa sawasawa) waliandamana kupinga gazeti kufungiwa, si kuitetea habari iliyoandikwa na gazeti. Wanasema kuna uwezekano kuwa habari hiyo haikuwa sahihi lakini kuna adhabu nyingine ambazo zingeweza kutolewa bila kuathiri uhuru wa gazeti hilo kutoa habari
   
 6. George Kahangwa

  George Kahangwa Verified User

  #6
  Oct 29, 2008
  Joined: Oct 18, 2007
  Messages: 539
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Call Dr Mvungi, Kama huna namba yake niandikie kahangwagl@udsm.ac.tz nitakupatia
   
 7. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #7
  Oct 29, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kahangwa na Paparazi Muwazi,

  Tumieni feature ya "ujumbe wa faragha" au barua pepe za hotmail, gmail, yahoo, na nyingine nyingi tu zinazotolewa bure, zikiwemo paparazi_muwazi@jamiiforums.com, likewise for Kahangwa.

  Lakini kama nia ni kuonyesha kwamba mko mbioni kuwapigia simu wahusika wakuu fulani na mna contact zao basi wapigieni simu kwanza ndio mje kuleta habari hapa.

  Wengi huahidi "nitampigia simu Kamanda wa polisi" halafu hawarudi. Sijui huwa wanataka kuonyesha nini hasa. Ile enzi ya kuheshimiana based on patronage, elitism, privilege and connection is long gone!!!
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Oct 29, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  sasa kwa nini wewe hukuwatumia huu ujumbe kwenye PM kuonesha kuwa siyo elite, au una kind of privilege kiasi cha kuwaambia watu wafanye nini kana kwamba hawajui kuna feature ya PM hapa JF?
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Oct 29, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Hubba hubba hubba hubbaaaaa......sometimes you are so good at this....
   
 10. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #10
  Oct 29, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  ...kama wewe ulivyoahidi kuleta matokeo ya "investigation" yako halafu ukaingia mitini na uliporudi ukaendelea kuuchuna. Sijui ulikuwa unataka kuonyesha nini hasa....
   
 11. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #11
  Oct 29, 2008
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Ohhooo! yangu macho bana, naona miamba inapambana, sisi wadogo tutakwepa kuhakikisha hatuumii!
   
 12. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #12
  Oct 29, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Nimekuwa nikifuatilia hii NCCR-Mageuzi naona kama kuna kaharufu flani ka kuwatetea au wapo bega kwa bega na CCM indirect kwani siku zote wamekuwa wapondaji fatilia ishu ya Tarime waliponda wakaambulia vikula hata buku havikufika.
  Angalia sasa chama hicho hata nguvu hakina kabisa kinapoteza mwelekeo hawa viongozi wamesha kiua chama.
   
Loading...