NCCR yahoji hotuba za mwezi za JK

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,794
287,947
Hongera NCCR! Hakuna ubaya wowote kuchukua points kutoka hapa ukumbini na kuzifanyia kazi

NCCR yahoji hotuba za mwezi za JK

na Mobini Sarya
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

CHAMA cha NCCR-Mageuzi kimemtaka Rais Jakaya Kikwete kutoa tamko la kupanda kwa bei ya mafuta akirejea ahadi zake za maisha bora kwa kila Mtanzania aliyowaahidi Watanzania.

Aidha kimehoji sababu ambazo zimemfanya Rais Kikwete aache kuhutubia taifa kupitia vyombo vya habari kama ilivyokuwa kawaida yake kila mwezi ambapo kwa miezi miwili sasa, hajalihutubia taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Idara ya Itikadi na Mafunzo, George Kahangwa, alisema chama hicho kinawapa pole Watanzania kwa ugumu wa maisha unaosababishwa na kupanda bei ya mafuta.

Alisema ni vema Rais Kikwete akatoa tamko la ufumbuzi wa tatizo hilo ili wananchi waweze kufikia ahadi iliyotolewa ya kupatiwa maisha bora.

Kahangwa alibainisha kuwa, malumbano yanayoendelea hivi sasa kuhusu sababu za kupanda kwa bei za mafuta, kunawachanganya wananchi, hivyo ni vema Rais Kikwete akaliweka wazi.

Alisena watu wengine wanadai hali hiyo inatokana na kushamiri kwa migogoro katika nchi zinazozalisha mafuta, hivyo kutokuwa na uwezo wa kuzalisha kwa kiwango kinachohitajika.

Aidha NCCR-Mageuzi imepinga vikali hatua ya serikali kubadili matumizi ya ardhi yenye rutuba kwa chakula na kuwapatia wawekezaji wapande mimea ya kuzalisha nishati mbadala ya dizeli.

“Serikali kupitia ubinafsishaji wake usio na hekima imekwishakujiingiza katika uuzaji wa ardhi ya rutuba ili wawekezaji waendeshe kilimo cha miwa na mibono kwa ajili ya nishati…hatua za namna hii zitasababisha taifa kuingia kwenye baa la njaa,” lilisema tamko la chama hicho.

Katika tamko hilo wametolea mfano mwekezaji aliyeuziwa bonde la Usangu wilayani mbarari ili aoteshe mibono baadala ya mpunga uliokuwa ukioteshwa katika bonde hilo ambapo asilimia 60 ya mchele unaouzwa nchini ulikuwa unatoka huko.
 
Naona vyama vya upinzani kuacha hili la kutumia kupanda kwa bei ya mafuta au vyakula kwani kwa wale ambao wanaishi nje ya Nchi nikikusudia maulaya wanajua hili tatizo la mfumko wa bei ,si Tanzania tu ni Dunia nzima ,hivyo watumie muda wao mwingi kujadili hatima ya mafisadi kwani tatizo la mfumko wa bei hili linawagusa vyama vyote kwa maana Chama chochote kitakachopata madaraka hakitaweza kupambana na suala hili ambalo hivi sasa katika ulimwengu ni jambo nyeti linalogusa maisha ya kila mtu.
Let them support CCM kwa hili kwa kukinga matokeo ya hapo baadae wapinzani wakifanikiwa kuitwaa nchi ,ziko ahadi zinaweza kuwekwa lakini sio hili la mfumko wa bei.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom