NCCR wamwonya JK mchakato wa Katiba; Mbatia asema NCCR walikuwa wa kwanza na hawajaitwa

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=2]28 NOVEMBER 2011[/h][h=3]Na Peter Mwenda[/h]
CHAMA cha NCCR-Mageuzi kimetoa tamko rasmi kuhusu muswada wa sheria ya kuundwa kwa Tume ya kukusanya maoni ya wananchi kuhusu katiba Mpya na kumshauri Rais Jakaya Kikwete, kutosaini muswada huo kuepusha taifa kuingia kwenye malumbano.

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Taifa Bw. James Mbatia, wakati akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya chama hicho Jijini Dar es Salaam.

Alikumbushia historia ya kupigania mabadiliko nchini na kusema kuwa NCCR Mageuzi ilikuwa ya kwanza kuwasilisha mapendekezo ya Katiba Mpya ya Tanzania kwa Rais Kikwete mwezi Aprili mwaka huu lakini cha kushangaza mpaka sasa hajaitwa wala kujibiwa.

Bw. Mbatia aliweka wazi kuwa chama chake inaona giza likikumba Taifa kutokana na ukweli kwamba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haipo kisheria wala kihalisia kutoka na kitendo cha Tanzania Zanzibar kubadili katiba yao na kusema kuwa eneo hilo ni nchi.

"Wanzanzibari hawatataliwa na kura ya maoni ya sheria ya muungano kwa kuwa wanayo sheria yao ya kura ya maoni, katiba ya Zanzibar haibadilishwi bila kura ya maoni iliyopigwa kwa mujibu wa sheria na Zanzibar kuridhia," alisema Bw, Mbatia.

Alisema kabla ya Rais Kikwete kukubali hoja ya kuwa na mchakato wa kuandika upya katiba kumekuwa na viashiria vinavyoonesha kuwa kumekuwepo na utayari na dhamira ya kweli ya CCM na serikali yake kukataa dhana nzima ya katiba mpya.

Alisema CCM hakioni umuhimu wa kuandika katiba mpya ndiyo maana hawataki kubainisha kwenye ilani yao ya uchaguzi na kwamba hata baada ya rais kukubali bado inaonekana CCM na serikali yake kuhakikisha mchakato mzima unakuwa mikononi mwa dola.

Mwenyekiti huyo alisema mwaka 1992 wakati mfumo wa vyama vingi unaanzishwa nchini NCCR Mageuzi ni miongoni mwa vyama vilivyoanzishwa kuhoji uhalali wa Katiba ya Tanzania kwa nguvu nyingi na kubainisha madhaifu makubwa.

Alisema NCCR Mageuzi ndiyo waasisi wa kudai Katiba ya Tanzania na kwamba wanayo imani kubwa kuwa watanzania wanao uwezo wa kujipatia katiba wanayoitaka kwa kuandikwa katiba mpya.

Bw. Mbatia alitaja baadhi ya kasoro katika muswada huo kuwa ni pamoja na vifungu vya 28 na 29 cha sheria mpya kuonesha kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ndiyo chombo kinachosimamia kura ya maoni huku wengi wakikosa imani na tume hiyo kwa sasa kutokana na kutokuwa huru.

Alisema kifungu cha 26 kinaonesha kuwa Rais atakuwa na mamlaka ya kuhakikisha Bunge la katiba linakuwa chini yake na kuongeza kuwa NCCR-Mageuzi inapendekleza Bunge la Katiba kuwa huru ili kufanya kazi yake bila shinikizo na mtu au kikundi chochote.

Alisema kifungu cha 20 cha sheria mpya kinabainisha kuwa Rais atakuwa na mamlaka ya kuteua wajumbe 116 kutoka Asasi zisizokuwa za kiserikali, asasi za kidini, vyama vya siasa vilivyo na usajili wa kudumu, taasisi za elimu ya juu na kwamba chama chake kinapendekeza kuwa wawakilishi hao wateuliwe na taasisi husika badala ya ya Rais.

Bw. Mbatia alisema NCCR Mageuzi inafahamu kuwa msingi wa umasikini unaokabili watanzania ni mfumo mbovu wa utawala hivyo katiba ya nchi ndiyo silaha ya kuhakikisha kunafanyika mapinduzi ya kisasa.



 
Oops, hata mimi nimepost hii. Hope MOD atatusaidia kuunganisha
 
Mbatia unataka kwenda peke yako IKULU? Jadili na Wabunge wa NCCR Mageuzi bungeni kama wako pamoja na wewe

Tulisikia wanataka mabadiliko ya Kiongozi yaani kukuondoa...
 
"Hatukutoka nje ya bunge ili tutafute nafasi ya kuonana na CCM Ikulu. Hatuna haja wala hatuhitaji kuonana na Kikwete kuhusu katiba".....David Kafulila, MP
 
haaaaa mbatia bana..eti nilikuwa wa kwanza..tiiiiteeeehhh teeehhh
 
wingi wa mashabiki wa chama fulani humu unaleta shida, jadilini hoja alizotoa, mnashupalia tu mtu ati kwa sababu hayumo kwenye chama chenu
 
Kwa nini watu mnapenda kuishi kwa historia??. This is too low. Utasikia, mara oh..sisi cuf ndiyo tulikuwa wa kwanza kutaka katiba mpya, serikali tatu etc. Na sasa nccr..! Mimi nauliza, mlikuwa wapi mpaka hizo hoja zikalala usingizi??. Mlihongwa???. Au ndiyo wivu wa kike kuona mwenzenu (CDM) anatumia kila opportunity iliyopo??.
 
Kwa nini watu mnapenda kuishi kwa historia??. This is too low. Utasikia, mara oh..sisi cuf ndiyo tulikuwa wa kwanza kutaka katiba mpya, serikali tatu etc. Na sasa nccr..! Mimi nauliza, mlikuwa wapi mpaka hizo hoja zikalala usingizi??. Mlihongwa???. Au ndiyo wivu wa kike kuona mwenzenu (CDM) anatumia kila opportunity iliyopo??.

The funny thing ni kwamba yeye Mbatia alikuwa akisubiri kuitwa, alipeleka mapendekezo akawa amekaa kimya anasubiri kuitwa, wakati CDM wao waliomba audience na raisi, ofcourse jibu lilitegemewa kuwa yes or no na watu wana move-on. Sasa cha kushangaza yeye Mbatia inaonekana kinachomsumbua ndiyo yale yale ya CC ya CCM.
 
Mhe. Kikwete mfanyie hisani Bw. Mbatia ukutane naye, mpige picha maana hizo ndizo siasa anazotaka yeye na Kamati kuu ya chama chako!! Ila hoja ya madai ya katiba mpya msiichakachue na kuifanyia siasa! Naamini Mhe. Kikwete utajiweka katika upande mzuri wa historia ukienda sambamba na upande wa Wananchi wanao kuambia ukweli bila kukuogopa au kujipendekeza kwako.

Taifa letu linahitaji katiba mpya sasa, kuliko kipindi kingine chochote kilicho wahi kutokea!

Hata kama suala la katiba mpya haikuwa ktk Ilani ya chama chako, lakini hili ni suala muhimu sana ili kuepusha migongano ya katiba ya JMT na ile ya ZNZ pia kumaliza kabisa mnachokiita kero za Muungano!
 
J ambo la msingi kuangalia tulipo fika kama ni pazuri tusonge mbele na kama ni pabaya tutafute namna ya kurekebisha ili tusonge mbele kirahisi
 
Nlisema jana Mh. Rais hakuwa na sababu zozote za msingi za kukutana na Chademu..sasa a can of worms imeshafunguliwa..kila mtu atakuja na ku-demand na yeye asikizwe na Mh. Rais. Nafikiri suala la katiba liachwe kama alivyopendekeza rais, watu wapeleke maoni yao kwa tume na bunge la katiba litaja yachambua..si rahisi kumridhisha kila mtu. Ni lazma tukuliane ktkk mambo ya msingi, lakini si lazma tukubaliane ktk YOTE. Wao Chademu / NCCR/CUF kaa wanaona wao ndo wanawakilisha maoni ya walio wengi basi wasubiri kushinda 2015 halafu waweke wao hiyo katiba wanayotaka wao. Wasitupotezee muda na nishati.
 
mbona kafulila alisema hawako tayari kukutana na kikwete au ulikuwa msimamo binafsi
 
Ama kweli Panya wengi wakichimba shimo haliwezi kwenda mbali, ina maana Mbatia hujaridhika na kilichowasilishwa na ujumbe wa CHADEMA? Au ni wivu wa kisiasa? Ninaamini ungekuwa na nia njema na mchakato wa katiba mpya ungeitisha press kuunga mkono kilicho wasilishwa na ujumbe wa CHADEMA, kuliko hatua uliyochukua ya kujitafutia umaarufu kivyakovyako Mkuu!
 
Tatizo la vyama vya siasa ni ubinafsi. Cdm wakifanikiwa kila mtu atafaidi ikiwa ni pamoja na nccr mageuzi. Pia cdm wameomba na wengine wasikilizwe ikiwa ni pamoja na nccr.
Drive ya kikwete na ccm yake ni kuogopa nguvu ya umma waliyonayo cdm. Unajua mpaka sasa hivi ni vimaadamano vya hapa na pale tu wakiamua kufanya kweli hapatakalika. Wapenzi wa cdm siyo wa kadi, wako kibao jeshini serikalini, usalama wa taifa. Hawahitaji kumlipa mtu awafuate kama ccm! Hilo ni jambo la kuogopa sana. Afanyeye kwa moyo ni bora kuliko kibarua wa siku.
 
Back
Top Bottom