NCCR waanza kuteremsha bendera kupinga kutimuliwa kwa Kafulila na wenzake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NCCR waanza kuteremsha bendera kupinga kutimuliwa kwa Kafulila na wenzake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by johnmashilatu, Dec 21, 2011.

 1. j

  johnmashilatu JF-Expert Member

  #1
  Dec 21, 2011
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 538
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 80
  Baadhi ya wanachama wa chama ca NCCR mageuzi wameanza kujiondoa katika chama hicho wakipinga kitendo cha hivi karibuni cha halmashauri kuu ya chama NCCR mageuzi kuwafukuza uanachama na kuwavua nafasi za uongozi wanachama wake kadhaa

  Tukio la hivi karibuni limeshuhudiwa katika kata ya Nyamiaga wilayani Ngara ambako viongozi wa tawi jana wameteresha bendera ya chama hicho na kutangaza kujiunga na chama cha demokrasi ya maendeleo

  Mwenyekiti wao bw Patrick Geofrey amesema wanapinga hatua ya kufukuzwa uanachama kwa Bw David kafulila na wenzake watatu pamoja na kuwaondoa kwneye uongozi wanachama kadhaa ikiwa ni pamoja na james bazisa aliyekuwa mjumbe wa halmashauri kuuu ambaye pia ni mkazi wa wilaya ya Ngara

  Wamesema NCCR mageuzi imeonyesha kukosa mwelekeo kwa kutoa maamuzi ya kukomoa wanachama wenye mtazamo tofauti na viongozi
   
 2. w

  wabusara Member

  #2
  Dec 21, 2011
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kawaambie tena kuwa NCCR chini ya Mbatia ni watu makini kutokana na uamuzi walioufanya kwa kuwatimua viongozi wake walioonyesha utovu wa nidhamu, Watanzania inatubidi tuepuke tabia ya kuangalia matokeo ya tukio fulani tu kwa sababu siyo busara kudeal na matokeo ya uamuzi fulani bila kuangalia msingi au chanzo cha uamuzi au tatizo husika. Na hiki ndicho kinachojitokeza kwa baadhi ya watanzania ktk sakata la kumtimua David Kafulila na wenzake.

  Wengi wanadai kaonewa huku ukiwauliza kaonewa wapi na namna gani hawawezi kueleza. Sasa watueleze kinaga ubaga kafulila kaonewa namna gani? USHABIKI ni dhambi mbaya pale unapotumika vibaya, ni dhambi mbaya kumtetea muhalifu wa sheria zozote zile, Kwa hiyo hao wanaotaka kushusha bendera za nccr washushe tuuuuuuuuuuu, siyo tatizo sana kwani ni bora chama kubaki na watu wachache kuliko kubaki na lundo la wanachama wasiokuwa na faida kwa chama husika, hivi unakuwa na mwanachama kama Rungwe, Kafulila nk amabao wanatoka nje ya utaratibu wa chama na kwenda kukichafua chama tena kwa uongo halafu unaacha kuwachukulia hatua za kinidhamu kwa misngi gani? Huo utakuwa ni wendawazimu kwa chama husika, kwa hiyo nadhani hao wanaoshusha bendera washushe tu kwa sababu ni kenge katika mamba hawafai hata kidogo,

  Hongera nccr KWA MAAAMUZI MAGUMU LAKINI PIA MAZURI YA KUIGWA kwa kushughulikia nidhamu ndani ya chama,
   
 3. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #3
  Dec 21, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,980
  Likes Received: 6,626
  Trophy Points: 280
  ngara ndo jimbo la sam ruhuza analo pigania kulikomboa. hiyo inaashilia samwel ruhuza kakalia kuti kavu. mia
   
 4. F

  FUSO JF-Expert Member

  #4
  Dec 21, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,867
  Likes Received: 2,340
  Trophy Points: 280
  NCCR ilishakufa tangu siku ile walipozikunja kule Tanga hadi Mrema akajificha chini ya meza na Lamwai akatokea dirishani :lol:
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  Dec 21, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ni kweli Mkuu. Kirusi kiliingia wakati ule wameshindwa kukitoa mpaka leo
   
 6. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #6
  Dec 21, 2011
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kosa la Kafulila linafanana sana na lile kosa alilotenda akiwa CDM. Hivi kama taifa tuna tunu kweli tunazosimamia???? Mimi nashangaa Hamad Rashidi na Kafulila wanatamka hadharani wanataka kupindua Katibu na M/Kiti. Hivi kweli uvumiliwe kisa uchanga? Haya ndo maoni tofauti? Najua kabisa kule CDM kuna maoni tofauti na hata kwenye familia zetu tuna maoni tofauti. so ndo ukapayuke nataka nimtoe baba au mama fulani?

  Hivi hivi tumekaa na akina mafisadi eti wamekomaa wakikamatwa tutayumbisha uchumi, kila mtu akitaka kuficha upungufu wake anajificha kwenye siasa,. Mweh!

  Ninasema bora ujenge ushawishi kwenye vikao halali then utekeleze adhima yako, sio umesikika sana then unataka ufanye mapenzi yako wengine wafuate all the time. Namshangaa Kafulila aliulizwa "waht if ukafukuzwa uanachama?" akajibu anaungwa na hamashauri kuu, mweh, si ndo hao hao??? eti walinyoosha mikono badala ya kura ya siri. Umesahau watz kama hawajajengewa ujasiri ni wanafiki wa kutupwa? hajui kama asilimia kubwa walio kwenye siasa may be including himself ni wachumia tumbo? mweh.

  Shusheni bendera turudi kwa chama kimoja labda tutafahamu what we need which i believe in beyone our daily bread.
   
 7. minda

  minda JF-Expert Member

  #7
  Dec 21, 2011
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Mbatia ni kibaraka wa CCM na yuko hapo kwa special mission ambayo ni kama imeanza kuwa accomplished.

  Time will tell.
   
 8. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #8
  Dec 21, 2011
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  kama ni kweli the we need serious people to attack him. sio move za kijinga za Kafulila

   
 9. Escobar

  Escobar JF-Expert Member

  #9
  Dec 21, 2011
  Joined: Sep 16, 2011
  Messages: 576
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 60
  Si hukumu but jamaa hana sifa!
   
 10. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #10
  Dec 21, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Wambie hao wana-ngara waache unafiki wao mbona hawakupata mbunge wa NCCR or CDM kama kweli wapambanaji?
  wote wanaomtetea Kafulila ni virus tu... so hata CDM msiwapoke... mwisho wamshauri Kfulila atafute kazi nyingine siasa apumzike
  ama aanzishe chama cha wanafiki CCW, Yeye kafulila, Zitto na Hamad Rashi CCW itawafaa sana, sababu wote wanatamma ya madaraka na msajili aruhusu wote mapacha watatu. KAZIHA wawe wenyeviti! teh chama kimoja wenyeviti watatu. CCW
   
 11. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #11
  Dec 21, 2011
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hivi, CHADEMA na vyama vingine, akitokea mwanchama wenu akaenda katika vyombo vya habari akasema CHADEMA ni photocopy ya CCM, akaonywa juu ya matamshi yake hayo akaleta dharau, akaambiwa athibitishe anachokisema akashindwa, mtamwacha aendelee kuwachafua?
   
 12. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #12
  Dec 21, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Wabusara Mshauri Mbatia atoe barua za kufukuzwa akina Kafulila na wenzake , kumbuka Mzee Rungwe ameshamwandikia Barua kutaka Mbatia atoe barua hizo!!!


  Hatutaki Mawazo ya Kidikiteta na kwa Suala hili Mbatia atajua na kupima je anaweza kusababisha Ufisadi wa kurudia Uchaguzi Kigoma KUsini??? Maana gharama zi zaidi ya 30bils kwa vyama vyote !!!

  Ni kweli NCCR ni chama makini lakini mwadhilishi wake Marando amekimbilia Chadema baada ya Mbatia kuingia mkataba na CCM??


  Mimi namushauli kafulilia asiombe msamaha wala asirudi NCCR kwani Mbatia hawezi kuacha kuitumikia CCM?? Hoja hapa Kafulila atumukia CDM
   
 13. FKM

  FKM Member

  #13
  Dec 21, 2011
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  mmmh kuwafukuza uwanachama ndo kuwachukulia hatua za kinidhamu?
   
 14. Chilipamwao

  Chilipamwao JF-Expert Member

  #14
  Dec 21, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 514
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  HUwezi tetea chama kilichojifia. Kinaongozwa na kipofu mbatia na vipofu wenzake wanaelekea shimoni. kwanza ni aibu kwa mwenyekiti wa chama kugombea na kukosa ubunge. Aone wenzie kama Mbowe na mrema wanadumisha haadhi za nafasi zao kwa vitendo.

  Shame on you Mbatia!
   
 15. Chilipamwao

  Chilipamwao JF-Expert Member

  #15
  Dec 21, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 514
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Na kamwe hawataweza kurudi. remember by that time NCCR = MREMA. It was a one man party.
   
 16. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #16
  Dec 21, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Hiyo ndo safari ya chama kujifia.
   
 17. 2mbaku

  2mbaku JF-Expert Member

  #17
  Dec 21, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 317
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Palipo na ukweli, uongo hujitenga!!!
  Matendo huhukumu.
   
 18. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #18
  Dec 21, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  nccr ilishakufa siku tangu mrema alipoikimbia,
   
 19. J

  JokaKuu Platinum Member

  #19
  Dec 21, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,098
  Trophy Points: 280
  ..wakati wote nilikuwa nadhani Kafulila ana support ya kumuondoa Mbatia NCCR.

  ..what was Kafulila thinking when he was making all that noise while campaigning for the removal of James Mbatia?

  ..hivi ina maana Kafulila alikuwa anazungumza tu kwenye vyombo vya habari bila kuhakikisha ana kura za wajumbe wa kutekeleza azma yake?

  ..halafu nawashangaa Mzee Tendwa na Nape Nnauye. hivi Nape anapozunguka nchi nzima akidai mafisadi wafukuzwe CCM hajui kwamba tutalazimika kuingia gharama za uchaguzi mdogo?
   
 20. M

  Morinyo JF-Expert Member

  #20
  Dec 21, 2011
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 2,486
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180

  Huyu jamaa uchaguzi uliopita aliacha rekodi ya pekee katika historia ya vyama vingi. Katika uchaguzi huo aliyekua mpinzani wake(Mh. D. A. Ntukamazina) alilazwa India takriban asilimia tisini na tisa(99%) ya muda wa kampeni bado Ntukamazina akashida kwa kishindo. Wananchi wa Jimbo la Ngara syo kwamba hawataki mabadiliko ila hawamwamini Ruhuza hata kidogo ndio maana waliamua kumpa mtu aliyekua amelazwa India mda wote wa kampeni kuliko kumpa Ruhuza.
   
Loading...