Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,565
- 19,440
1. Ndicho kilichoanza harakati za vyama vingi- kwa kiwewe changu hata mimi nilisukuma gari la Mrema mwaka 1995, halafu siku moja pale Uhuru nilipaki gari langu sehemu ya Breweries ambayo almanusra nivunjiwe kioo cha gari kwa watu kuegemea gari hilo sehemu ambayo nilidhani ni mbali na mkutano pale shule ya Uhuru kabla mkutano haujaanza, lakini baada ya mkutano kuanza gari langu likawa limezingirwa na umati. NCCR kilipotea step baada ya 1995 lakini nadhani wanaweza kuwa wanalijua hilo sasa.
2. Kama CCM hakina mmiliki, yaani ni cha wanachama wote kwa vile walioko leo wamekikuta. CHADEMA ni cha Mbowe kwa vile alikirithi kwa Mtei, na ACT ni cha Zitto aliyekianzisha. CUF ni cha Lipumba ambaye amekuwa ni mwenyekiti na mgombea pekee wa uraisi kwa takriban miaka 25 sasa. Kuna vingine vingi vidogovidogo ambavyo vina wamiliki wake. Mbatia asiendelee kuwa mwenyekiti wa NCCR, kwa sababu naye anaweza kuwa perceived kama mmiliki wa NCCR.