NCCR ni chama cha upinzani kilichotisha zaidi hapa Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NCCR ni chama cha upinzani kilichotisha zaidi hapa Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Annael, Jun 11, 2012.

 1. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #1
  Jun 11, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 13,202
  Likes Received: 10,153
  Trophy Points: 280
  Nimejaribu kufuatilia vyama mbalimbali vya upinzani hapa nchini kwetu, tangu mfumo wa vyama vingi uanzishwe mwaka 1992. Nimegundua katika vyama vyote NCCR Mageuzi ndicho chama kilicho tikisa nchi kuliko vyama vyote.

  Ninakumbuka mwaka 1995 nikiwa kijijini watu wote walijua Raisi wao ni Mrema.

  Tangu wakati ule hakijatokea chama kingine chenye nguvu kama kile. labda kwa sasa CHADEMA inafuata njia ileile miaka ya usoni huenda kikawa chama cha upinzani chenye nguvu.

  Hayo ni maoni yangu sawa wana jf?
   
 2. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2012
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  2005?
  Aidha ni chama pekee ambacho hakijashawishiwa na mabeberu wanaotumia migongo ya IMF na Benki ya Dunia
   
 3. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #3
  Jun 11, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Kinatisha sana baada ya M/kiti wake kuhushishwa na mambo ya cameroon!
   
 4. M

  Molemo JF-Expert Member

  #4
  Jun 11, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Pole sana hujui unachokisema
   
 5. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #5
  Jun 11, 2012
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Annael, ukitaka kujua rangi halisi ya mashabiki wa chama fulani ambacho ni bingwa wa matusi, taja chama ambacho si chao. Kitakachofuata ni kumwaga matusi (kana kwamba ndio sera yao kuu) kama unayoyaona hapa sasa.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. E

  EL MAGNIFICAL JF-Expert Member

  #6
  Jun 11, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 939
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  mkuu sasa hapo mbona umeweka neno "tetesi"
   
 7. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #7
  Jun 11, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 1,112
  Trophy Points: 280
  Kama ndiyo hivyo, nguvu zao ziliishia wapi? Kama waliishiwa nguvu, basi hata Chadema itakuwa hivyohivyo, watabaki na historia tu ya kuwahi kuwa chama cha upinzani kilichotishia Chama tawala(Ccm).
  The unseen is illustrated by the seen.
   
 8. George Kahangwa

  George Kahangwa Verified User

  #8
  Jun 11, 2012
  Joined: Oct 18, 2007
  Messages: 539
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Barnabas, kwa dhamira njema unataka majibu sahihi ya swali lako?
   
 9. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #9
  Jun 11, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,688
  Likes Received: 12,725
  Trophy Points: 280
  mwisho wako wa kufikiri.
   
 10. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #10
  Jun 11, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,688
  Likes Received: 12,725
  Trophy Points: 280
  Hapo zamani za kale palikuwa

  off..............date
   
 11. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #11
  Jun 11, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,493
  Likes Received: 1,050
  Trophy Points: 280
  Endelea kuota tu, mkono wa binadgmu haudondoki Mzee fisi! Utaranda na njia hadi uzeeke!
   
 12. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #12
  Jun 11, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  NCCR ilitisha ka moto wa mabua! ni kweli kabisa hujakosea!
  2005 Mrema hakuwa NCCR acha kukurupuka kijana
   
 13. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #13
  Jun 11, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 1,112
  Trophy Points: 280
  Yes, nahitaji jibu safi toka kwa mtu ambaye hana matusi kama mijichadema mingi ya humu.
  The unseen is illustrated by the seen.
   
 14. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #14
  Jun 11, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 1,112
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo.
  The unseen is illustrated by the seen.
   
 15. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #15
  Jun 11, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  kuna watu wamejiunga humu hata mwezi hawajamaliza lakini wameshaanza matusi.
  nccr mageuzi haijawahi kutikisa tanzania bali mrema ndiye aliyetikisa na kila kitu kilikuwa mrema na alipoondoka kwenda tlp nayo ikaonekana kama imetikisa.
  labda uiongelee cuf wakati ikiwa kigori kwa sababu haikupata nguvu ya kigogo yeyote kutoka ccm.
  chadema ni chama kinachokua kimkakati na kila mwaka kinaongeza mikakati ya kupanuka na kueleweka na watanzania.
  hata tajiri aliyeanza na mtaji mdogo na kuwa milionea ni vigumu kufilisika.

  MODS TUNAOMBA MREKEBISHE MASHART YA KUJIUNGA HUMU ILI MGENI AKIJA AKITOA MATUSI KABLA YA KUFIKISHA MWAKA ALE BAN YA MAISHA HATA KAMA KATUMIA ID YA BANDIA MTUMIE TEKNOLOJIA YA KUMFAHAMU KWA SABABU HILO NAJUA LINAWEZEKANA.
  TUNATAKA JF IWE MAHALA PA HESHIMA NA MAGT WAWEZE KUONEKANA.
   
 16. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #16
  Jun 11, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,814
  Trophy Points: 280
  Mkuu Ringo Edmund vyama karibu vyote viongozi wake kwa namna moja ama nyingine walitoka CCM ama kwenye serikali ya CCM. NCCR mwanzoni ilikuwa na viongozi ambao hawakuwa CCM mwanzoni lakini wengi wao walikuwa kwenye Serikali ya CCM. Kisha ndio Mrema akatinga pale NCCR na kuipa tafu. CUF ilibarikiwa kupata tafu ya Viongozi waanzilishi kama Maalim Seif, Shabaan Mloo, Hamad Rashid na wengine wengi ambao walikuwa wametimuliwa CCM huko nyuma. Nakumbuka UMD ndicho chama ambacho viongozi wake hawakuwa na historia na CCM bali TANU tena historia yenyewe mbaya tu. Kwa upande wa CDM na umaarufu wake ni kweli imekuwa ikipanda taratibu lakini pia kuna schools of thought mbili kubwa tofauti ambazo zinaelezea uhusiano wa umaarufu wa CDM na viongozi wake; kuna watu wanasema ni Mbowe amekiimarisha chama kwa uongozi wake uliotukuka lakini pia kuna wengine wanasema ni Dr. Slaa aliyekiimarisha Chama kutokana na kugombea URais 2010 na kuonekana anakubalika miongoni mwa Watanzania kutokana na makombora yake dhidi ya ufisadi. Hii misimamo miwili inaisumbua sana CDM. Hivyo huenda CDM nayo imeegemea mtu kama wanaoamini kuwa Dr. Slaa ndiye kaipaisha ni wakweli.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #17
  Jun 11, 2012
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hata UMD, Marehemu Mzee Fundikira mwanzilishi wake naye alitoka huko huko TANU/CCM. Hakika ukiandika historia za vyama kwa kigezo cha waanzilishi wote utakuta ni wale wale, japo sababu na mitizamo ni tofauti.
   
 18. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #18
  Jun 11, 2012
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Tafakari vizuri kabla ya kumshambulia unayedai kaleta matusi. Ni kweli Mrema alivuma, lakini ndani ya NCCR walikuwepo pia wakali wengine wakati huo ambao bahati mbaya nyota zao sasa ziko kivingine, hawa ni pamoja na Prof. Mwesiga Baregu (Sasa CHADEMA), Dr. Masumbuko Lamwai (sasa CCM), Marando, Mnyika, Selasini (Nao sasa CHADEMA) na wabunge 16 wa NCCR-Mageuzi wa wakati huo; matharani Ndimara Tegambwage, Makongoro Nyerere, Polisya Mwaiseje na wengine. Historia imeandikwa vizuri, wanaotaka kujua ukweli wataufahamu tu, hawatapotoshwa na ushabiki ambao unaelekea kukithiri sasa hapa JF
   
 19. B

  Bob G JF Bronze Member

  #19
  Jun 11, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  NCCR kama chama hakikua na nguvu bali Mrema ndiye alie kua na nguvu, But CHADEMA ni chama chenye nguvu kama chama sio mtu. na kilimfanya hata Nyerere akili kuwa ni chama chenye sera makini zaidi kuliko vyama vyote.
   
 20. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #20
  Jun 11, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  jitahidi kufuatilia na siyo kujaribu.
   
Loading...