Elections 2010 NCCR na CUF wamezuia Tarime Kupata Mbunge Mpiganaji

Jobo

JF-Expert Member
May 15, 2008
586
43
Uchaguzi umekwisha na matokeo ya Tarime yanasikitisha. Chadema imezidiwa kura chini ya 1000 na CCM... hii inaweza kuwa ni kweli au vinginevyo. Lakini lililo dhahiri ni kwamba ushindi wa Chadema ungekuwa dhahiri kama si kujitosa katika uchaguzi kwa CUF na NCCR huku wakijua kabisa kuwa kuingia kwao kutawanufaisha zaidi CCM. Hawa wawili wana kura karibia 18000 ambazo zingetosha kabisa kuibwaga CCM. Kwa maoni yangu hawa ndio wamewapora wananchi wa Tarime, mbunge wao mahiri.... ni wazo tu!!!!!
 
hilo mbona halina ubishi kaka.
Mwera njaa sana.Amekosa yote na amewasaliti wanatarime.
 
Mimi mara nyingi nimekuwa nikiwaza sana jmabo hilo,kuna sehemu unakuta kuna wagombea wengine hata kwa kuwatazama tu unaona hawashindi,nafikiria kwa nini wasiunganisha nguvu kwani mara nyingi ukijumuisha nguvu za wapinzani wote zinakuwa nyingi kuliko hata ccm wanazoweza kuiba,hata kenya waliitoa KANU madarakani kwa mtindo huo kupitia rainbow coalition.Pia kwa upande mwingine kuna shaka pale mpinzani wa kweli kujiunga na mpinzani uchuro baadae anawavurugia wenzie mipango mpaka wengine imesadikiwa ni makada wa chama cha wezi wanaingia upinzani ili kuwadhoofisha.Ila bado naamini watu wakiwa makini na waelewa,uchu wa madaraka ukawekwa pembeni wakaangalia sehemu fulani nguvu ikiunganishwa kwamba ushindi utapatikana ni vyema kufanya hivyo wakiwa na tahadhari pia ya mamluki.Pole pole tutafika
 
hivi wenye uhalali wa kuachiwa majimbo ni CHADEMA tu sio vyama vingine nauliza jamani?
 
Tyson Wassira aliwaambia Tarime kuipa CHADEMA itekeleze sera za CCM ni sawa na kumpa Shetani atangaze injili takatifu (Tarime 2010 wakaafiki)..Hongera Chacha Nyambari Nyangwine, mbunge kijana (34) wa chama cha mapinduzi, Chadema imerudisha maendeleo yetu Tarime, nafuu na halmashauri ya wilaya imerudi CCM..
 
Nadhani matokeo hayo wasilaumiwe NCCR wala CUF, hayo ndio matokeo ya demokrasia, Chadema kwa bahati mbaya haikujipanga vyema katika kulitetea jimbo hili ambalo kwa muda mrefu limekuwa strong hold ya Chadema. Migogoro ya ndani ya chama jimbo la Tarime ilipelekea Mwera kuondoka na ndipo tatizo lilipoanza, kimsingi Mwera hakuwa anazifahamu hata sera za CUF na alikuwa anajinadi kwenye kampeni zake kwa kutumia sera za Chadema, Tarime ni pigo kwa Chadema
 
Cha kushangaza, Mwela aligombea Ubunge na Udiwani, kapata udiwani...... sijui kama amewatendea haki chadema
 
Nadhani matokeo hayo wasilaumiwe NCCR wala CUF, hayo ndio matokeo ya demokrasia, Chadema kwa bahati mbaya haikujipanga vyema katika kulitetea jimbo hili ambalo kwa muda mrefu limekuwa strong hold ya Chadema. Migogoro ya ndani ya chama jimbo la Tarime ilipelekea Mwera kuondoka na ndipo tatizo lilipoanza, kimsingi Mwera hakuwa anazifahamu hata sera za CUF na alikuwa anajinadi kwenye kampeni zake kwa kutumia sera za Chadema, Tarime ni pigo kwa Chadema

Suala la Mwera kuhama chadema na kujiunga cuf limechangia kwa kiasi kikubwa jimbo la tarime kuangukia mikononi mwa ccm. Mwera aliondoka na wanachama wengi tu na wananchi wengine waliokuwa wanamuunga mkono kwahiyo kuidhoofisha chadema. Inabidi chadema wajifunze kutokana na makosa yao, waangalie njia bora zaidi za kusuluhisha migogoro na matatizo yao ya ndani. Kama chadema wangekuwa makini sana hata jimbo la kigoma kusini lingekuwa lao kama wasingemfukuza kafulila, na hapa simaanishi kwamba nccr kushinda ni makosa ila najaribu kutafakari ni kwa namna gani chadema walishindwa kumaliza matatizo yao ya ndani pasipo kufukuzana. Juzi nimemsikia zitto kupitia ITV akisema kwamba wote walioshinda nafasi za ubunge kwa tiketi ya nccr mageuzi mkoani kigoma walikuwa wanachama wa chadema lakini kutokana na mambo fulani fulani yaliyotokea ndipo wakaamua kuhamia nccr mageuzi. Nadhani chadema wana kazi ya kutafakari kwa kina namna bora ya uendeshaji wa chama na kutatua migogoro yao bila kuathiri ustawi wao.
 
Cha kushangaza, Mwela aligombea Ubunge na Udiwani, kapata udiwani...... sijui kama amewatendea haki chadema

Hata mimi nilishangazwa kidogo kwamba aligombea na udiwani na akashinda.

Kumbe angeweza kubakia chadema na akagombea udiwani, na kwahiyo angeweza kukisaidia chama chake kupata viti vingi vya udiwani na hatimaye kuendelea kuongoza halamashauri na bila shaka angeweza kuchaguliwa kuendelea kuwa mwenyekiti wa halamashaurilakini kwa kuwa alitaka mbili kwa mpigo ndio matokeo yake hayo.
 
umoja ni silaha kuu........ vyama vikiungana hata kama ni leo......nijulisheni ili niwe mwanachama rasmi wa chama hicho cha siasa kilichosheni mseto maalumu......! lakini kwa kutengana kwao huku...waacheni wawe wanagalagazwa kila siku na vilio vya kuibiwa kura huku wangeungana tu jimbo lingekuwa lao na mfano tumeuona..... ULIZENI WILAYA YA NYAMAGANA
 
Nyahende hapa kuilaumu Chadema sidhani kuwa ni sahihi! MwerA alipaswa kuelewa kuwa kushindwa kwake kura za maoni ndiyo demokrasia. Ikumbukwe kwamba ni Chadema kilimpigania hadi kuupata ubunge tena kwa gharama kubwa! Kweli shukrani ya punda!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom