Uchaguzi umekwisha na matokeo ya Tarime yanasikitisha. Chadema imezidiwa kura chini ya 1000 na CCM... hii inaweza kuwa ni kweli au vinginevyo. Lakini lililo dhahiri ni kwamba ushindi wa Chadema ungekuwa dhahiri kama si kujitosa katika uchaguzi kwa CUF na NCCR huku wakijua kabisa kuwa kuingia kwao kutawanufaisha zaidi CCM. Hawa wawili wana kura karibia 18000 ambazo zingetosha kabisa kuibwaga CCM. Kwa maoni yangu hawa ndio wamewapora wananchi wa Tarime, mbunge wao mahiri.... ni wazo tu!!!!!