Elections 2010 NCCR Mageuzi waungana na CHADEMA - Uchaguzi Ulikuwa mbovu, umevurugwa sana!

Not_Yet_Uhuru

JF-Expert Member
Oct 11, 2010
1,304
431
Ukweli unasambaa, Uongo unazidi kujitenga...!

Kulingana na Taarifa Ya Habari, Redio Tumaini - saa 9:00 alasiri hii, Chama cha NCCR Mageuzi kimetoa tamko kuwa Uchaguzi wa Tanzania ulikuwa mbovu, umevurugwa na Kura nyingi zimeibiwa kwa kiwango kikubwa, jambo amabalo limeharibu na kuvuruga haki karibu nchi nzima.

Pia Taasisi ya Wanasheria ambayo ilikuwa ikishirikiana na taasisi nyingine kadhaa kusimamia uchaguzi zimetoa Tamko kuwa Uchaguzi haukuwa huru na haki Maana Tume haiko huru, imeteuliwa na Rais ambaye naye alikuwa Mgombea, ndio maana kumekuwa na ukiukwaji na ucheleweshwaji wa makusudi wa matokeo has kule ambako vyama vya Upinzani vilionekana kuishinda; Mfano Arusha, Mwanza, Dar, Mbeya nk...


Source: Taarifa Habari; Radio Tumaini saa 9:00 alasiri.
 
Kama kweli wanauhakika na wanachokisema wadai haki kwa kuwa haki hailetwi kama maji ya mto inapiganiwa haye.
 
watu walisema nccr ni mapandikizi ya ccm imekuwaje tena?
Nakumbuka kusema mbatia ni political prostitute na pandikizi la ccm... sijisahihishi

haya turudi kwenye mada.... kama nimeelewa vizuri, nccr haijaungana na chadema kama vyama, bali nccr nayo imesema uchaguzi ulivurugwa

au wewe una uelewa gani? labda tuanzie hapo
 
Pia Taasisi ya Wanasheria ambayo ilikuwa ikishirikiana na taasisi nyingine kadhaa kusimamia uchaguzi zimetoa Tamko kuwa Uchaguzi haukuwa huru na haki Maana Tume haiko huru, imeteuliwa na Rais ambaye naye alikuwa Mgombea, ndio maana kumekuwa na ukiukwaji na ucheleweshwaji wa makusudi wa matokeo has kule ambako vyama vya Upinzani vilionekana kuishinda; Mfano Arusha, Mwanza, Dar, Mbeya nk...
[/COLOR][/SIZE][/FONT]

Source: Taarifa Habari; Radio Tumaini saa 9:00 alasiri.
[/COLOR]

tunaomba ripoti hiyo ya wanasheria itundikwe
 
ni kweli whata DW-swahili mchana huu walikuwa wanamhoji DR MVUNGI kadai kuwa uchguzi umechakachuliwa
 
tunaomba ripoti hiyo ya wanasheria itundikwe

A quick quote is here:
LHRC, Sweden, ponder on General Elections


The LHRC was on November 4th, 2010 honored with a visit from the Swedish Embassy in the country. Margareta Brisman, Counselor charged with Political Affairs, Trade and Jacob Strom, Deputy Director, Ministry for Foreign Affairs; came to the LHRC to find out more on the just ended polls in the country. The LHRC Executive Director Francis Kiwanga held a meeting with the team and highlighted a number of flaws that his organization had noticed during the just ended General Elections with one being delay to announce results, violence, and fraud among other things.
Harold Sungusia, Director of Advocacy and Reform at the LHRC also told the guests that they had received more than 6 thousand reports ever since they began using ICT. According to Sungusia, the LHRC will compile a comprehensive report on the just ended general elections.
Sweden has always maintained close ties with the LHRC. Last year, the Swedish embassy in the country funded the LHRC making it possible for the later to train on civic and voters education before deploying 95 monitors to overseer the local government elections. This year, The Swedish Embassy has once again funded the LHRC making it possible for the later to monitor the General Elections.

Found on here: Legal And Human Rights Center
 
Back
Top Bottom