NCCR-Mageuzi: Wananchi wanataka kujua mahali aliko Rais wao kipenzi

Kihava

JF-Expert Member
May 23, 2016
4,823
2,000
Kwa mujibu wa Majaliwa huyu anayeuliziwa akitoka hadharani atakuwa anazurura. Je, ina maana hatutamwona tena hadharani? Na akija kuonekana hadharani tujue ni mzuriraji? Yaani atakuwa anazurura?
 
Kihava

JF-Expert Member
May 23, 2016
4,823
2,000
Majaliwa alisema, “kiongozi huyo mkuu wa nchi, anaendelea vizuri na anachapa kazi zake kama kawaida.”. Kwa wale waliofika angalau darasa la Saba wanaielewaje kauli hii ya huyu kiongozi wetu?
 
Phillemon Mikael

JF-Expert Member
Nov 5, 2006
10,228
2,000
Hajafa kafungua macho alfajirii baada ya kuwa amekata kauli toka tarehe 4/3 ina maana zaidi ya siku kumi kuwa kwenye machine hajitambui, haonekani kuwa timamu ....japo watalazimisha aanze kutoa maagizo ,kwenye nchi inayofuata katiba angehitaji miezi kadhaa ya kuangalia afya yake ....
 
chikambabatu

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
1,256
2,000
Mbatia ana namba ya mkuu, ampigie waongee, toka mwanzo hutuma sms za kumtia moyo, waziri amesema tumwache anachapa kazi!
 
Juma1967

JF-Expert Member
Jun 27, 2012
19,181
2,000
CHAMA cha upinzani nchini Tanzania – NCCR-Mageuzi – kimekoleza moto katika mjadala unaohusu mahali alipo Rais John Pombe Magufuli. Anaripoti Matrida Peter Dar es Salaam … (endelea).

Martha Chiomba, katibu mkuu wa chama hicho, amewaambia waandishi wa habari, leo Jumapili, tarehe 14 Machi 2021, makao makuu ya NCCR- Mageuzi, Ilala, jijini Dar es Salaam, kwamba wananchi wanataka kujua, “mahali aliko rais wao kipenzi.”

Kwa niaba ya wanachama wa NCCR- Mageuzi na wananchi wengine, Matha amesema, “wananchi wanataja Rais Magufuli ajitokeze hadharani, ili kumaliza shauku yao, kuhusu mahali aliko rais wao.”

Akisitiza hoja yake, Matha ametumia Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, inayozungumzia uhuru wa maoni na haki kwa wananchi kupewa taarifa, wakati wote kuhusu matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli zao.

Amesema, “viongozi tulionao ni zao la Katiba, na mamlaka yao yanatoka kwa wananchi kwa mujibu wa Ibara ya 8 ya Katiba ya Tanzania. Katiba hii, inaeleza, wananchi ndio msingi wa mamlaka yote na serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi.”

Anaongeza: “…NCCR- Mageuzi, inaitaka serikali kutoa taarifa sahihi juu ya hali ya kiafya ya rais, ili kumaliza minong’ono na kuondoa taharuki.”

Kwa mujibu wa Matha, chama chake, kimetaka kuelezwa mahali aliko Rais Magufuli, ili kusaidia umma kuondokana na uvumi unaosambaa kwenye mitandao ya kijamii, ukidai kuwa “Rais ni mgonjwa.”

Hatua ya chama hicho ambacho ndio mwasisi wa mfumo wa vyama vingi nchini, kutaka maelezo ya mahali aliko Rais Magufuli, imekuja siku tatu baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kufanya hivyo.

Akizungumza na waandishi wa habari, tarehe 12 Machi mwaka huu, katibu mkuu wa Chadema, John Manyika, aliomba serikali kueleza umma, “rais yupo wapi; na hali yake yake ya kiafya ikoje?”

Akizungumza kwa kujiamini, Matha amesema, “wananchi wana haki ya kupata habari sahihi na kwa wakati kuhusu masuala mbalimbali yanayowahusu na hasa ya kuhusu viongozi wao.”

Amesema, “wananchi wanapotaka kujua hali au mahali aliko rais wao, siyo kosa hata kidogo. Kosa ni pale wenye wajibu wa kutoa taarifa, kushindwa kutekeleza takwa hilo la kikatiba.”

Amesema, maelezo yaliyotolewa na Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, kwamba Rais Magufuli yupo na anaendelea na shughuli zake, haijeleza kama rais ni mzima.

“Wala waziri mkuu, hajaeleza rais yuko wapi. Hajaeleza anafanya shughuli gani mzito ambayo inamzuia kutoka hadharani. Taarifa yake inapaswa ifafanue yupo wapi na hili ni wajibu wetu Kikatiba la kupewa taarifa iliyojitosheleza,” amesisitiza mwanasiasa huyo.

Akizungumza baada ya sala ya Ijumaa, mjini Njombe, tarehe 12 Machi 2021, waziri mkuu Majaliwa aliwataka wananchi, kuwapuuza watu kutoka nje wanaoeneza uzushi kuwa rais ni mgonjwa.

Alisema, watu hao, wakiwamo Watanzania wanaoishi nje ya nchi, wanafanya hivyo, ili kuleta taharuki zisizokuwa na tija kwa taifa, kwa kuwa ni maadui wa maendeleo ya nchi.

Majaliwa alisema, “kiongozi huyo mkuu wa nchi, anaendelea vizuri na anachapa kazi zake kama kawaida.”

Alisema, “…tuwapuuze baadhi ya Watanzania ambao wamejawa na chuki tu, wamejawa na husda tu na wanatamani kuwachonganisha na kutaka kushuhudua taifa hili likiporomoka.

“Tulieni, uongozi wenu upo imara na mafanikio tunayaona. Kumzushia rais ugonjwa ni chuki. Wanasema atoke, aende wapi? Ulishamkuta siku moja anazurura Kariakoo? Rais ana mpango wake wa kazi si mtu wa kuzurura!”

Lakini Martha anasema, kauli ya waziri mkuu Majaliwa, haijitoshelezi na hivyo, wanataka rais mwenyewe ajitokeze hadharani, ili kumaliza shauku ya wananchi wake ya kumuona kiongozi wao.

Naye Mkuu wa Idara ndani ya chama hicho, Joackiam Mahega amesema, “Rais ni taasisi; na wananchi waliomchagua wanataka kumwona rais wao.”

Amehoji: “Kama tumefikishwa hapa, ugumu uko wapi? Kipi kigumu kinachomzuia raia kutoka hadharani?”

Chanzo: mwanahalisionline.com
So what?
 
Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,908

Huu uzi umefufuliwa upya, kulikoni??
 
  • Haha
Reactions: BAK

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom