NCCR-Mageuzi: Wananchi wanataka kujua mahali aliko Rais wao kipenzi

Trust None

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
1,260
2,000
CHAMA cha upinzani nchini Tanzania – NCCR-Mageuzi – kimekoleza moto katika mjadala unaohusu mahali alipo Rais John Pombe Magufuli. Anaripoti Matrida Peter Dar es Salaam … (endelea).

Martha Chiomba, katibu mkuu wa chama hicho, amewaambia waandishi wa habari, leo Jumapili, tarehe 14 Machi 2021, makao makuu ya NCCR- Mageuzi, Ilala, jijini Dar es Salaam, kwamba wananchi wanataka kujua, “mahali aliko rais wao kipenzi.”

Kwa niaba ya wanachama wa NCCR- Mageuzi na wananchi wengine, Matha amesema, “wananchi wanataja Rais Magufuli ajitokeze hadharani, ili kumaliza shauku yao, kuhusu mahali aliko rais wao.”


Akisitiza hoja yake, Matha ametumia Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, inayozungumzia uhuru wa maoni na haki kwa wananchi kupewa taarifa, wakati wote kuhusu matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli zao.

Amesema, “viongozi tulionao ni zao la Katiba, na mamlaka yao yanatoka kwa wananchi kwa mujibu wa Ibara ya 8 ya Katiba ya Tanzania. Katiba hii, inaeleza, wananchi ndio msingi wa mamlaka yote na serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi.”

Anaongeza: “…NCCR- Mageuzi, inaitaka serikali kutoa taarifa sahihi juu ya hali ya kiafya ya rais, ili kumaliza minong’ono na kuondoa taharuki.”

Kwa mujibu wa Matha, chama chake, kimetaka kuelezwa mahali aliko Rais Magufuli, ili kusaidia umma kuondokana na uvumi unaosambaa kwenye mitandao ya kijamii, ukidai kuwa “Rais ni mgonjwa.”

Hatua ya chama hicho ambacho ndio mwasisi wa mfumo wa vyama vingi nchini, kutaka maelezo ya mahali aliko Rais Magufuli, imekuja siku tatu baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kufanya hivyo.

Akizungumza na waandishi wa habari, tarehe 12 Machi mwaka huu, katibu mkuu wa Chadema, John Manyika, aliomba serikali kueleza umma, “rais yupo wapi; na hali yake yake ya kiafya ikoje?”

Akizungumza kwa kujiamini, Matha amesema, “wananchi wana haki ya kupata habari sahihi na kwa wakati kuhusu masuala mbalimbali yanayowahusu na hasa ya kuhusu viongozi wao.”

Amesema, “wananchi wanapotaka kujua hali au mahali aliko rais wao, siyo kosa hata kidogo. Kosa ni pale wenye wajibu wa kutoa taarifa, kushindwa kutekeleza takwa hilo la kikatiba.”

Amesema, maelezo yaliyotolewa na Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, kwamba Rais Magufuli yupo na anaendelea na shughuli zake, haijeleza kama rais ni mzima.

“Wala waziri mkuu, hajaeleza rais yuko wapi. Hajaeleza anafanya shughuli gani mzito ambayo inamzuia kutoka hadharani. Taarifa yake inapaswa ifafanue yupo wapi na hili ni wajibu wetu Kikatiba la kupewa taarifa iliyojitosheleza,” amesisitiza mwanasiasa huyo.

Akizungumza baada ya sala ya Ijumaa, mjini Njombe, tarehe 12 Machi 2021, waziri mkuu Majaliwa aliwataka wananchi, kuwapuuza watu kutoka nje wanaoeneza uzushi kuwa rais ni mgonjwa.

Alisema, watu hao, wakiwamo Watanzania wanaoishi nje ya nchi, wanafanya hivyo, ili kuleta taharuki zisizokuwa na tija kwa taifa, kwa kuwa ni maadui wa maendeleo ya nchi.

Majaliwa alisema, “kiongozi huyo mkuu wa nchi, anaendelea vizuri na anachapa kazi zake kama kawaida.”

Alisema, “…tuwapuuze baadhi ya Watanzania ambao wamejawa na chuki tu, wamejawa na husda tu na wanatamani kuwachonganisha na kutaka kushuhudua taifa hili likiporomoka.

“Tulieni, uongozi wenu upo imara na mafanikio tunayaona. Kumzushia rais ugonjwa ni chuki. Wanasema atoke, aende wapi? Ulishamkuta siku moja anazurura Kariakoo? Rais ana mpango wake wa kazi si mtu wa kuzurura!”

Lakini Martha anasema, kauli ya waziri mkuu Majaliwa, haijitoshelezi na hivyo, wanataka rais mwenyewe ajitokeze hadharani, ili kumaliza shauku ya wananchi wake ya kumuona kiongozi wao.

Naye Mkuu wa Idara ndani ya chama hicho, Joackiam Mahega amesema, “Rais ni taasisi; na wananchi waliomchagua wanataka kumwona rais wao.”

Amehoji: “Kama tumefikishwa hapa, ugumu uko wapi? Kipi kigumu kinachomzuia raia kutoka hadharani?”

Chanzo: mwanahalisionline.com
 

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
9,682
2,000
Huyu mama lengo lake ni kutaka watu wajue tu kuwa Chama chao bado kipo. Maana watu tulishasahau kama kuna Chama hapa nchini kiitwacho NCCR Mageuzi!!
 

Maneno Meier

JF-Expert Member
May 12, 2013
2,401
2,000
Inauma sana. Sielewi kwa nini anawatendea wananchi wake hivyo. Kweli huyu Rais ana moyo wa upendo kwa wanachi wake kama yeye mwenyewe anyvo jipa? Au anatuona sisi wote ni maadui zake tusio mtakia mema? Inashangaza sana.
 

kawombe

JF-Expert Member
Mar 26, 2015
5,385
2,000
fd1362e0-7cad-4466-b99c-a10708ed5ccc.jpg
 

Deceiver

JF-Expert Member
Apr 19, 2018
8,812
2,000
Kwanza kabisa rekebisha usemi wakO
NCCR MAGEUZI CHINI YA MBATIA SIO CHAMA CHA UPINZANI.
1. Hiyo Ni CCM B Ila NCCR hawakujua kwamba shetani Hana dini.
2. NCCR Ni CCM B hata kiongozi wake alishawahi kupewa ubunge ma wakubwa wa CCM.

I rest my case
 

Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
46,503
2,000
Ina uma sana. Sielewi kwa nini anawatendea wananchi wake hivyo. Kweli huyu Rais ana moyo wa upendo kwa wanachi wake kama yeye mwenyewe anyvo jipa? Au anatuona sisi wote ni maadui zake tusio mtakia mema? Inashangaza sana.

Ni jizi la kura.
 
  • Love
Reactions: BAK

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom