NCCR Mageuzi wanaitaji pongezi kwa kuonyesha uzalendo wao bungeni kupinga ufisadi

Mshume Kiyate

JF-Expert Member
Feb 27, 2011
6,766
894
Wana JF.
Mwenyekiti wa chama hicho James Mbatia katoa taarifa za uhakika zimeonyesha kuwa mgao wa umeme unaoonekana ukiendelea nchini una mkono wa baadhi ya wabunge na watendaji wa Tanesco, ambao wasingependa wananyang'anywe ulaji wao.

Katika hatua nyingine Mbatia alionyesha kushangazwa na watu wanaobeza hatua iliyochukuliwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi kuipa zabuni Puma Energy ya kusambaza mafuta ya uzalishaji umeme kwa Tanesco na IPTL na kuziacha kampuni nyingine zilizokuwa na bei kubwa, akisema hawana uzalendo.

Mbatia anasema hawa ndiyo majambazi na wanahujumu uchumi tunaowasema, kwa nini upinge uamuzi ambao unalifanya taifa liokoe Sh3 bilioni kila juma fedha ambayo siku zote ilikuwa inaingia kwenye mikono ya wajanja...Mbatia aliyeongozana na wabunge wengine, Moses Machali, David Kafulila, Felix Mkosamali na Agripina Buyogela.

SOURCE; MWANANCHI JUL 27 2012
 
Mbatia kakopi na kupaste kutoka CDM.Angalia hotuba ya Mnyika leo bungeni utajua maana yake.
 
Mbatia kakopi na kupaste kutoka CDM.Angalia hotuba ya Mnyika leo bungeni utajua maana yake.

nilikuwa mpenzi wa hoja za zito na ni moja ya vijana walionivutia kwa hoja zao cdm ukiongeza na mie kutoipenda ccm. Kwa kauli zake kwenye suala la umeme na nishati,zito amepotoka na fedha anazohongwa na hao wajanja wanaochota pesa kupitia sakata la umeme. Wameruhusu maji ya ruaha yahamishiwe kapunga,mto umepungua,mabwawa hayana maji na wao wanavuna sasa. Jk tunajua ulileta iptl, umekula vya kutosha. Tuachie tupumue kidogo!!!
 
Sasa hapo mbatia katoa ufisadi gani, hilo mbona liko kwenye Mwanahalisi au raia mwema la jumatano, sasa yeye katoa jana
 
Mbatia kakopi na kupaste kutoka CDM.Angalia hotuba ya Mnyika leo bungeni utajua maana yake.

Mkuu Molemo,
Samahani nina maswali kuhusiana na mchango wako katika hili.
Una uhakika hujaongozwa na ushabiki?
Waweza kuweka tamko la Mbatia na Hotuba ya Mnyika pamoja ili kuthibitisha hiki unachokisema? Mbatia aliongea lini, na hotuba ya Mnyika imetolewa lini?
Je, kuna mgogoro wowote kama wawili hawa kwa nyakati tofauti wanaongelea suala hilo hilo moja kwa maslahi ya umma?
 
naona ss umefika wakati wakati wa uchaguzi ni kuwachagua wale maskini huku mkila hela za mafisadi
 
Mbatia kakopi na kupaste kutoka CDM.Angalia hotuba ya Mnyika leo bungeni utajua maana yake.

Mkuu wakati mwingine tujaribu kuweka mapenzi mbali hajaona wala kusikia Mbatia alivyokuwa anaongea na waandishi wa habari unataka kutuambia Mnyika alimpa Mbatia hotuba yake kabla kuisoma bungeni? Yeyote ambaye anapambana kuitetea nchi yetu akifanya vizuri tunaitaji kumpongeza.
 
Back
Top Bottom