Elections 2010 NCCR-Mageuzi wajipanga kupinga ushindi wa Mdee mahakamani

ndio democracy, naamini kwa kawe hata uchaguzi ukirudiwa mara 5 chadema itachukua, mdee atachukua anatumia vibaya inavyoonekana na malengo binafsi
 
werevu tulishajua. nia ya mbatia kugombea kawe haikuwa kushinda ila kuisadia CCM kushinda.
 
Hapa ndio nachoka na siasa za bongo!


(Source Mwananchi)

hahaaa unajua Mbatia unataka kutia hasira watu humu wakutusi wapewe BAN..we haya tu ...we hupendwi kwa nini huelewi?hata ugombee uenyekiti wa mtaa hutapata? hivi wewe ukoje lakini
 
Waache waende wanadhani huko kuna kuchakachua? Wameliwa hao wao watafute njia mbadala kuiboresha NCCR siyo kwa mgongo wa CHADEMA. Wenzao wameuza sera je wao? Mahakamani? Kweli wao maslahi kwanza.
 
Dawa ya Mbatia huko NCCR- mageuzi iko jikoni, yeye kakosa ubunge Kawe lakini wenzie kule Kigoma wamefanya kweli na huo ndio utakuwa mwanzo wa wakina Kafulila kutaka kumuondoa kwenye uenyekiti kwani wao ndio wanaoipa NCCR ruzuku !! Huku kwenda mahakamani ni geresha tu!!
 
Dawa ya Mbatia huko NCCR- mageuzi iko jikoni, yeye kakosa ubunge Kawe lakini wenzie kule Kigoma wamefanya kweli na huo ndio utakuwa mwanzo wa wakina Kafulila kutaka kumuondoa kwenye uenyekiti kwani wao ndio wanaoipa NCCR ruzuku !! Huku kwenda mahakamani ni geresha tu!!

tena kuna jimbo dogo wa miaka 24 kashinda bana?daaah yule dogo kanipa raha sana ..sasa ale nondo ili awe anachangia mambo ya maana bungeni
 
Mbatia fanya kazi za kujinge chama acha na mambo ya ubunge kawe. Wananchi wa kawe walimchagua halima mdee kwa kura za tsunami. Hivyo hata uchaguzi ukirudiwa leo bado wananchi watamchagua tu.
 
Mbatia kama anazo sababu za msingi na ana amini haki yake imegandamizwa ruksa kwenda mahakamani.
 
Kesi nyingine ni ya Jimbo la Kawe ambapo wanaamini kuwa maneno ya Nkya kwamba mgombea wa chama hicho, James Mbatia ananyanyasa wanawake yalisababisha wanawake na wasichana kuwapigia kuwa wanawake wenzao.

Aliwataja wanawake hao kuwa ni Mdee aliyeshinda na Angela Kizigha wa CCM aliyeshika nafasi ya pili.

Alisema sheria ya uchaguzi ya mwaka 1985, inakataza kushawishi kupiga kura kwa kufuata jinsia, na shauri lingine linamtaka Mdee kuthibitisha kauli yake kwamba Mbatia kapewa milioni 80 na CCM kutokana na kutokuwepo na hesabu za kupokea kiasi hicho cha fedha
katika vitabu vya hesabu vya vyama hivyo.

"Kwa misingi hii, Halima Mdee alijua kuwa anasema uongo, basi alikusudia kupotosha
wapigakura na kama aliyasema yana ukweli atakuwa amevisaidia vyama hivyo juu ya ufujaji mkubwa wa mali za vyama na njia ya kujua kweli ni kufika mahakamani," alisema.

Alisisitiza kuwa kesi ya Mdee na Nkya ni ya uchaguzi lakini wanaweza kufunguliwa kesi
nyingine na Mbatia kudai bilioni moja kwa kumdhalilisha kutokana na kutoomba msamaha katika siku walizopewa.

Hata hivyo, Nkya alishasema kuwa alinukuliwa vibaya na gazeti (si Habarileo) wakati Mdee alikanusha kuwa hajawahi kusema mambo hayo

Huyu jamaa kwan ni wa jinsia gani? Mbona ana mabifu na wanawake? Kwanini asimshataki na huyo wa CCM?
 
Tatizo la NCCR-Mageuzi lipo kwa watu wawili. Yule jamaa aliyekalia kiti na mwingine ni yule mwenye jina la ka-mnyama.
 
Huyu Mbatia anatafuta aibu zaidi kwani yataibuka mambo huko mahakamani ambayo atatamani dunia ipasuke ajifiche, shauri yake. Angewekeza nguvu ya kukijenga chama baada ya kuanza kuonyesha uhai kwa kupata wabunge wanne.
 
mmmh,haya ngoja tuone zitakavokuwa busy mahakama,najua hukumu zitatoka 2014
 
Kesi nyingine ni ya Jimbo la Kawe ambapo wanaamini kuwa maneno ya Nkya kwamba mgombea wa chama hicho, James Mbatia ananyanyasa wanawake yalisababisha wanawake na wasichana kuwapigia kuwa wanawake wenzao.

Akili mbofumbfu ndiyo matatizo yake! kwa namna hii Mbatia huwezi kutuwakilisha wana Kawe hata siku moja,achilia mbali ubunge hata uenyekiti serikali ya mtaa wako huwezi kupata maana wanaoishi mtaa wako ni wenye upeo mkubwa wa uelewa.Angalia hata matokeo ya mtaani kwako. Kama maneno ya Nkya yalikuathiri kwa nini Angela hakushinda na ni mwanamke?
Kwa taarifa yako Mbatia huna uwezo wa kuwawakilisha wana Kawe. Habari ndiyo hiyo.
 
Back
Top Bottom