NCCR-Mageuzi wafanyiwa vurugu Babati

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,571
[h=2][/h]
VIONGOZI wa Chama cha NCCR-Mageuzi, jana walifanyiwa vurugu na baadhi ya wakazi wa mji wa Babati, mkoani Manyara, kutokana na matumizi ya eneo la uwanja. Hali hiyo ilijitokeza juzi baada ya uwanja uliokuwa umeandaliwa, kwa ajili ya mkutano wa hadhara, kutumiwa na vijana wa mji huo ambao walikuwa katika mchezo wa soka wa Ligi Daraja la Nne ngazi ya wilaya.

Viongozi Danda Juju na Hemed Msabaha, ambao ni wajumbe wa halmashauri kuu ya chama hicho, walipofika katika Uwanja wa Kwaraa na kukuta mchezo wa soka ukiendelea.

Kabla ya vurugu hizo, viongozi kadhaa wa chama hicho, walitangaza, eneo hilo lilipaswa kutumika kwa ajili ya mkutano wa hadhara kwa kuwa taarifa ilitolewa tangu mapema.

Baada ya matangazo hayo, ilipotimia saa 10 jioni, Juju, Msabaha na viongozi wengine wa chama hicho, walifika uwanjani hapo kwa ajili ya mkutano wa hadhara na kukuta mchezo wa mpira ukiendelea.

Tukio hilo, lilionekana kuwashangaza viongozi hao na hivyo kulazimika kulalamika, huku mashabiki wa timu hizo nao wakionesha kutokuwa tayari kupisha kwa madai kuwa wao ndiyo wenye kibali.

Mvutano huo, ulidumu kwa dakika kadhaa na kusababisha vurugu kidogo kati ya wafuasi wa chama hicho na mashabiki hao wa mpira.

Hata hivyo, vurugu hizo zilimfanya Ofisa Michezo, Wilaya ya Babati, Fabian Manda, kufika uwanjani hapo na kutangaza wenye kibali kwa wakati huo walikuwa ni viongozi wa chama hicho.

Hata hivyo viongozi hao kwa nyakati tofauti, walipinga kitendo hicho na kusema kwamba, hawawezi kuendelea na mkutano katika mazingira yenye utata.

Juju alililaumu Jeshi la Polisi Wilaya ya Babati, kwa kile alichosema kuwa limeshindwa kutimiza wajibu wake na kusababisha vurugu zisizokuwa na sababu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom