NCCR Mageuzi, tunaomba Mh. Kafulila asamehewe! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NCCR Mageuzi, tunaomba Mh. Kafulila asamehewe!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by anney, Dec 21, 2011.

 1. a

  anney Senior Member

  #1
  Dec 21, 2011
  Joined: Jul 9, 2010
  Messages: 156
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu nimekuwa nikifuatilia sakata la Mh. Kafulila jinsi iliyokuwa na hukumu iliyotolewa kuwa amefukuzwa uanachama. Mimi binafsi nawapongeza NCCR kwa kuchukua ule uamuzi ili kujenga nidhamu. Chadema wameifanya kwa madiwani wake. Hivi vyama vimeonyesha kuwa vinaweza kufanya maamuzi. Mimi nimeamua kuandika hili jamiiforum kwa sababu ni watu wengi wanaosoma maoni humu mtandaoni na pia ujumbe unafika mapema. Kwanini tunahitaji kumsamehe Mh Kafulila:
  1. Ameshaomba msamaha na kujuta, ndiyo maana alilia machozi.
  2. Tangu apate hili kasheshe amekuwa na nidhamu ya kuongea na vyombo vya habari, hii inaonyesha kuwa amejifunza.
  3. Ana mchango muhimu kwenye bunge,NCCR na taifa, kwa hiyo tusiupoteze.
  4. Wananchi jimbo la Kigoma kusini walifanya maamuzi magumu sana ya kuweza kumchagua kijana mdogo kama yeye na kuipa fursa taifa kuwa na mbunge kijana kama yeye. Hivyo tuwaonee huruma wananchi wa kigoma kusini. Tusiwapelekee vurugu kama za Igunga.
  5. Uchaguzi mdogo ni gharama kwa taifa na hatujui matokeo yake maana yapo mengi yanayoweza kufanyika ili kutuondoa kwenye mchakato wa Katiba mpya ambayo tunapaswa kuelekeza fikra za vyama vyote. huko
  6. Kwa NCCR hivi sasa nidhamu imerudi ndani ya chama, hivyo hakuna sababu wa kushikilia msimamo ambao kwa misingi yake umeogeza vuguvugu la chama kukua. Mjiandae kujenga umoja ili mjenge upinzani.
  7. Tunapaswa kujifunza kusamehe kwa kosa ambalo linasameheka. NCCR naomba muwe kama yule mzazi wa kwenye biblia ambaye alimfanyia kijana mpotevu sherehe baada ya kurudi. Hivyo tutumie pia imani zetu kusamahe maana hiyo ni sehemu ya maisha.
  Mimi sio mwanachama wa NCCR, kuna tuhuma nyingi zinatolewa dhidi ya Mbatia kuwa anaisaidia CCM, hizi ni tuhuma, hakuna mwenye uhakika, hii tabia yetu ya kuhukumu kuwa huyu ni ccm bila kuwa na 'data' si jambo jema katika kujenga mstakabali wa taifa. Nafahamu Mbatia amefungua kesi ya kupinga ubunge wa Mh Halima Mdee, Mimi binafsi ile kesi siipendi, ila kwa kuwa tunaamini mfumo wa utawala bora na kila mtu yupo huru kufikiri na kuamua anavyataka!mbatia hana hatia kwa kuamua kufungua kesi. Ndivyo ilivyo kwa wewe mwanajamii humu unavyokuwa huru kutoa maoni yako na wengine pia wako huru kufanya hivyo. Hatupaswi wote kufikiri kwa kufanana. Ila namshauri naye angaiacha ile kesi kwa kumsamehe, najua ni changamoto kwake na familia yake!maana ukitoka kwenye uchaguzi kunama chungu mengi.
  Nafahamu wengine Mtasema/watasema kuwa mbona hujawaombea Madiwani chadema msamaha! Sijafanya hivyo kwa sababu wale madiwani hata baada ya kuombwa na chama hawakuonyesha nia njema ya kuheshimu maamuzi ya chama. Ingawa wakati mwanzo niliwahi kumwambia kiongozi moja chadema mkae mmalize kimyakimya mgogoro wenu, kwa bahati mbaya haikuwezekana.
  Pia kwa kujenga mstakabali wa upinzani NCCR iwasamehe wale wote iliowafukuza pamoja na Kafulila. Pia nawashauri wanasiasa ambao wapo kwenye vyama wajenge busara ya kuheshimu utaritibu wa vyama vyao kwa kusubiri wakati wa uchaguzi kufanya mabadiliko tunayohitaji. Tuna historia ndefu ya vurugu ya upinzani Tangu enzi za Mzee Mapalala CUF, Mrema na Mabere NCCR, TLP nk.
  Asanteni
   
 2. u

  utantambua JF-Expert Member

  #2
  Dec 21, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,373
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mbatia akagombee mwenyewe Kigoma Kusini
   
 3. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #3
  Dec 21, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,276
  Trophy Points: 280
  Sijakuelewa nini unamaanisha !!Kichwa cha habari na maneno vinasigana!!hapohapo unasema wewe siyo NCCR!!kichwa cha habari kimejitangaza wewe NCCR unaomba.......
  [h=2]Re: Nccr mageuzi tunaomba mh. Kafulila asamehewe![/h]
   
 4. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #4
  Dec 21, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,973
  Likes Received: 2,967
  Trophy Points: 280
  Hizi thread za Kafulila zimezidi. Mods unganisheni hizi mambo.
   
 5. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #5
  Dec 21, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Msamehe wewe na Zitto wako. mshauri atafute kazi nyingine! kwani lazima awe mbunge? aende zake huko mnafiki analia kinafiki na bado huyo kaka yake mroho wa madaraka!
   
Loading...