NCCR- Mageuzi, PPT- Maendeleo: Uwanja wa ndege Mbeya usiitwe JK International Airport

GreenCity

JF-Expert Member
May 28, 2012
5,599
2,000
[h=3]NCCR WAUKALIA KOONI UWANJA WA NDEGE MBEYA KUITWA J.KIKWETE[/h]
NCCR WAPINGA UWANJA KUPEWA JINA LA KIKWETE
CHAMA cha NCCR-Mageuzi kimepinga uamuzi wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Mbeya kutaka Uwanja wa Ndege wa Songwe upewe jina la Rais Jakaya Kikwete. NCCR pamoja na PPT Maendeleo kimependekeza kuwa uwanja huo uitwe Mbeya International Airport. Uamuzi wa kutaka uwanja huo uitwe jina la Kikwete ulipitishwa katika kikao cha kamati hiyo kilichoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mjini, Dk. Norman Sigalla kwa niaba ya Mkuu Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro. Wakizumngumza na Tanzania Daima Jumapili baada ya kikao hicho, Katibu wa NCCR-Mageuzi Wilaya ya Mbeya Mjini, George Mbojela alisema licha ya yeye kuwapo kwenye kikao hicho, alishtushwa na uamuzi huo kwani tayari kuna miradi kadhaa ya maendeleo iliyopewa jina la Rais Kikwete.

“Ni vyema wananchi wa Mbeya wangeshirikishwa kwenye kupendekeza jina la uwanja huo kwani wanaopaswa kupewa kipaumbele katika kupendekeza jina la uwanja huo ni wakazi wa Mbeya na sio wakuu wa wilaya ambao ni watu wa kupita tu,” alisema katibu huyo wa NCCR-Mageuzi. Mwenyekiti wa PPT Maendeleo, Godfrey Devis aliungana na NCCR-Mageuzi kupinga hatua hiyo kwani inanyima fursa mkoa wao kujitangaza kimataifa. Ujenzi wa uwanja huo wa ndege wa Songwe ulianza kwenye uongozi wa Rais Benjamin Mkapa wakati huo Profesa Mark Mwandosya akiwa Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi.

Source: Ngelesi K. (March 2013). NCCR wapinga uwanja kupewa jina la Kikwete. Retrieved form Tanzania Daima
 
Biznocrats

JF-Expert Member
Apr 5, 2011
452
170
NCCR WAUKALIA KOONI UWANJA WA NDEGE MBEYA KUITWA J.KIKWETE

NCCR WAPINGA UWANJA KUPEWA JINA LA KIKWETE
CHAMA cha NCCR-Mageuzi kimepinga uamuzi wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Mbeya kutaka Uwanja wa Ndege wa Songwe upewe jina la Rais Jakaya Kikwete. NCCR pamoja na PPT Maendeleo kimependekeza kuwa uwanja huo uitwe Mbeya International Airport. Uamuzi wa kutaka uwanja huo uitwe jina la Kikwete ulipitishwa katika kikao cha kamati hiyo kilichoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mjini, Dk. Norman Sigalla kwa niaba ya Mkuu Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro. Wakizumngumza na Tanzania Daima Jumapili baada ya kikao hicho, Katibu wa NCCR-Mageuzi Wilaya ya Mbeya Mjini, George Mbojela alisema licha ya yeye kuwapo kwenye kikao hicho, alishtushwa na uamuzi huo kwani tayari kuna miradi kadhaa ya maendeleo iliyopewa jina la Rais Kikwete.

"Ni vyema wananchi wa Mbeya wangeshirikishwa kwenye kupendekeza jina la uwanja huo kwani wanaopaswa kupewa kipaumbele katika kupendekeza jina la uwanja huo ni wakazi wa Mbeya na sio wakuu wa wilaya ambao ni watu wa kupita tu," alisema katibu huyo wa NCCR-Mageuzi. Mwenyekiti wa PPT Maendeleo, Godfrey Devis aliungana na NCCR-Mageuzi kupinga hatua hiyo kwani inanyima fursa mkoa wao kujitangaza kimataifa. Ujenzi wa uwanja huo wa ndege wa Songwe ulianza kwenye uongozi wa Rais Benjamin Mkapa wakati huo Profesa Mark Mwandosya akiwa Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi.

Source: Ngelesi K. (March 2013). NCCR wapinga uwanja kupewa jina la Kikwete. Retrieved form Tanzania Daima

Tuna mambo mengi ya msingi kama Taifa tunatakiwa kuyajadili kwa maendeleo ya Taifa letu na sio upuuzi kama huu.
 
mazoo

JF-Expert Member
Mar 15, 2013
215
0
Hakuna uwanja wa Thatcher,Churchill,Blair au Cameroun nchini UK.
Bora wageuita uwanja wa Mwakyusa,Mwalongo,Ulimboka au so if their wish.
 
Chris Lukosi

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
4,581
2,000
Tanzania Daima sasa ni gazeti rasmi la udaku...
JK kafanya mengi sana kwa nchi yetu
Ni lazima ziwepo kumbu kumbu zake za kudumu kama hizi.
Mie bvinafsi nilikuwa Chadema , lakini niliporudi home na kukuta lami mpaka mlangoni kwetu kijijini kalenga ilibidi nirudi CCM
SALUTE JK
RAIS WA WATU
 
kinauche

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
7,681
2,000
Tuna mambo mengi ya msingi kama Taifa tunatakiwa kuyajadili kwa maendeleo ya Taifa letu na sio upuuzi kama huu.
What difference will it make? Ndege hazitatua na kuondoka? I agree. There are more important issues for discussion. What is in a name? Kama anaufungua yeye kwa nini usipewe jina lake? NCCR, jadilini mambo ya maana zaidi. Ukiitwa Kikwete au MBeya, bado utabaki Mbeya.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
punainen-red

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
1,732
0
Dhuluma ni mbaya sana.. Walishindwa kuupa uwanja wa michezo wa Dar jina la B. Mkapa, kwa wivu uliowajaa ikabidi wausilimishe uwanja wa Taifa kwa jina tofauti ili tu kupindisha mambo, sasa tena mradi ambao ulianzishwa wakati wa mzee wa utandawazi unapewaje jina la kikwete?! Hivi watu wa ccm hawana hata ile aibu ya kibinadamu tu?!
 
Inside10

JF-Expert Member
May 20, 2011
24,133
2,000
JK kafanya mengi sana kwa nchi yetu
Ni lazima ziwepo kumbu kumbu zake za kudumu kama hizi.
Mie bvinafsi nilikuwa Chadema , lakini niliporudi home na kukuta lami mpaka mlangoni kwetu kijijini kalenga ilibidi nirudi CCM
SALUTE JK
RAIS WA WATU

walewaleeeee..
 
MABAGHEE

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
686
250
Mbeya International Airport ingeuza jina la jiji la mbeya sehemu nyingi duniani. Lakini wakubwa wakiamua basi inakuwa. Wanapata kumfurahisha rais? Waache hizo.
 
Sikonge

JF-Expert Member
Jan 19, 2008
11,534
2,000
Wala mbwa bana?!?! Kasheshe kwelikweli.....

tumblr_m7876sckZj1rn4jfeo1_500.jpg

JK kafanya mengi sana kwa nchi yetu
Ni lazima ziwepo kumbu kumbu zake za kudumu kama hizi.
Mie bvinafsi nilikuwa Chadema , lakini niliporudi home na kukuta lami mpaka mlangoni kwetu kijijini kalenga ilibidi nirudi CCM
SALUTE JK
RAIS WA WATU
 
MPANDA Jr

JF-Expert Member
Nov 27, 2011
1,295
1,195
JK kafanya mengi sana kwa nchi yetu
Ni lazima ziwepo kumbu kumbu zake za kudumu kama hizi.
Mie bvinafsi nilikuwa Chadema , lakini niliporudi home na kukuta lami mpaka mlangoni kwetu kijijini kalenga ilibidi nirudi CCM
SALUTE JK
RAIS WA WATU

KWA UPUUZ WAKO ULIDHAN CHADEMA WANAGAWA TSHT Eeh? Utanywea chai hiyo lami. Mwenyewe unadhan umesaidiwaaa
 
JERUSALEMU

JF-Expert Member
Sep 19, 2012
3,012
2,000
Tuna mambo mengi ya msingi kama Taifa tunatakiwa kuyajadili kwa maendeleo ya Taifa letu na sio upuuzi kama huu.
mngekuwa makini kama unavyo jinasibu mbona tungekuwa mbali sana. watu wa ccm wameifikisha Nchi hapa tulipo. uwanja uitwe kikwete kwa kipi cha maana alicho wafanyia watanzania?
 
Consigliere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
12,004
2,000
JK kafanya mengi sana kwa nchi yetu
Ni lazima ziwepo kumbu kumbu zake za kudumu kama hizi.
Mie bvinafsi nilikuwa Chadema , lakini niliporudi home na kukuta lami mpaka mlangoni kwetu kijijini kalenga ilibidi nirudi CCM
SALUTE JK
RAIS WA WATU

kwa hiyo zile sababu ulizotoa awali ulizi stage ili kuchafua ila ukweli uliokurudisha ni lami mpaka mlangoni!
 
Baba V

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
19,487
2,000
JK kafanya mengi sana kwa nchi yetu
Ni lazima ziwepo kumbu kumbu zake za kudumu kama hizi.
Mie bvinafsi nilikuwa Chadema , lakini niliporudi home na kukuta lami mpaka mlangoni kwetu kijijini kalenga ilibidi nirudi CCM
SALUTE JK
RAIS WA WATU

Dah...! kazi ipo ..,
 
The Khoisan

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
13,687
2,000
JK kafanya mengi sana kwa nchi yetu
Ni lazima ziwepo kumbu kumbu zake za kudumu kama hizi.
Mie bvinafsi nilikuwa Chadema , lakini niliporudi home na kukuta lami mpaka mlangoni kwetu kijijini kalenga ilibidi nirudi CCM
SALUTE JK
RAIS WA WATU

Tubadilishe na jina la TZ na kuwa JK ili kumpa heshima inayostahili.
 
Ogah

JF-Expert Member
Mar 10, 2006
6,226
2,000
mijitu mingine kwa kujipendekeza aisee........yaani mijanaume mizima kazi kutwa kujipendekeza.........acheni Uitwe Mbeya International Airport.........au hata Uitwe Songwe International Airport
 
reandle

JF-Expert Member
May 6, 2009
11,202
2,000
mngekuwa makini kama unavyo jinasibu mbona tungekuwa mbali sana. watu wa ccm wameifikisha Nchi hapa tulipo. uwanja uitwe kikwete kwa kipi cha maana alicho wafanyia watanzania?
Tatizo sio CCM, tatizo ni Watanzania au labda niseme Waafrika, manake utafikiri ni kweli tumelaaniwa...tuache kujitia upofu!!! Na hakika hii nchi tutaendelea kuwa maskini maisha yetu yote kwavile bado hatutaki kujitazama kwa mapana yetu!! Sana sana naona CCM ni kama wakala tu umaskini wetu lakini tatizo la msingi ni sisi wenyewe.....!
 
Mvaa Tai

JF-Expert Member
Aug 11, 2009
6,161
2,000
Hakuna uwanja wa Thatcher,Churchill,Blair au Cameroun nchini UK.
Bora wageuita uwanja wa Mwakyusa,Mwalongo,Ulimboka au so if their wish.

Mkapa kajenga uwanja mkubwa wa soka Dar watu wakapendekeza uitwe Mkapa Stadium, inasemekana Kikwete alikataa, Mkapa akaanzisha ujenzi wa Chuo kikuu Dodoma, watu wakapendekeza kiitwe Benjamin Mkapa University, inasemekana Kikwete alikataza, Mkapa huyohuyo amefanya kazi kubwa kabisa kuhakikisha ujenzi wa uwanja wa ndege Songwe unafanyika leo hii watu wanaojipendkeza kwa huyu Kikwete wakitaka uwanja huo uitwe jina lake, jamani tuache tabia za kujipendekeza pendekeza hata ukifanyiwa kitu kikubwa, achilia mbali kupewa kitu kidogo kama ukuu wa wilaya, itaniuma sana uwanja wa Songwe ukiwa jina la Kikwete
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom