NCCR - Mageuzi, mguu sawa yajipanga tena baada ya miaka 30 ya Mageuzi

Dr Shekilango

Senior Member
Dec 30, 2013
192
117
Ni wazi chama cha NCCR-Mageuzi kinajipanga kufanya kazi kubwa katika siasa za Tanzania baada ya miaka 30 ya Mageuzi ya kisiasa Tanzania. NCCR-Mageuzi ni mwasisi wa siasa za vyama vingi na Mabadiliko ya katiba mpya, wao wanajita THE SUPER OLD PARTY (SOP)

Taarifa za ndani ya chama hicho zinadokeza chama hicho kinajiandaa na matukio mawili ya kukihuisha chama hicho moja linatarajiwa kufanyika mwezi huu katika Ukumbi wa Diamond Jubilee eneo kilipozaliwa miongo mitatu iliyopita na lingine litafanyika mwaka kesho, hii yote ni kuendelea kujiimalisha katika siasa za Mageuzi.

Baada ya uchaguzi chama hiki kilijifanyia baadhi ya mabadiliko kadhaa ikiwa ni pamoja na kuanzisha KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA TAARIFA, mwanzo hakikuwa mfumo huo. Mabadiliko mengi yamefanyika hasa baada ya uchaguzi, na sasa chama hicho kinajianda kufanya siasa za uongozi na kuwa mbadala au serikali kivuli. "Kuna mambo makubwa yanakuja kwenye chama chetu alisikika mmoja ya kiongozi kijana na mwenye ushawishi ndani ya chama hicho, tegeni masikio mwezi huu kila mtu atakubali upinzani kurudi kwenye asili yake".


THE SUPER OLD PARTY (SOP)


FB_IMG_1633544703528.jpg
 
Kuelekea uchaguzi Mkuu wa 2020 mlliwapamba kuwa watakuwa na wabunge wengi na mkafika sehemu mkawaambia kuna majimbo 20 ya free, naona mmerejea tena !
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom