NCCR Mageuzi: Lowassa ajieleze kama ataendelea kubaki CHADEMA akikatwa jina 2020

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
Kufuatia kauli ya aliyekuwa mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwavuli wa Ukawa, Edward Lowassa ya kugombea tena urais mwaka 2020, Mkuu wa Oganaizesheni wa NCCR-Mageuzi, Faustine Sungura amemhoji Lowassa kama atakuwa tayari kuendelea kutumikia Ukawa kama jina lake halitapendekezwa kugombea nafasi hiyo.

Sungura amesema kauli hiyo ya Lowassa kupambana tena katika kinyang’anyiro cha urais mwaka 2020 kunategemea maamuzi ya chama kupitisha jina lake.

“Nimemsikia Lowassa anasema kuwa anajiandaa kupambana na Rais John Magufuli mwaka 2020, lakini je, yuko tayari kuheshimu maamuzi ya chama kwa maslahi ya wakati huo?” Alihoji Sungura.

Sungura alisema mwaka jana jina la Lowassa lilipochujwa kwenye wagombea urais ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) alijiondoa na kuhamia Chadema.

“Je, atakuwa tayari kuheshimu maamuzi ya chama pale ambapo jina lake halitapitishwa kugombea urais Chadema au atahamia chama chake?” Alihoji Sungura.

Akizungumzia ushindi wa viti vya meya uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, Sungura alisema ushindi huo ambao wameshinda wagombea wa Chadema na CUF usitafsiriwe kuwa ni ushindi wa Ukawa, bali ni ushindi wa Chadema na CUF .

“Nasema hayo kwa sababu ukizungumzia Ukawa unazungumzia vyama vinne ambavyo ni Chadema, NCCR Mageuzi, NLD na CUF, lakini kilichofanyika kuna baadhi ya kata tulisimamisha wagombea lakini walituwekea kauzibe tusipate,” alisema Sungura.

Sungura alisema baadhi ya vyama ndani ya Ukawa wana ubinafsi kuwachanganya watanzania kwa neno Ukawa ambalo halina maana yoyote badala yake kuviua vyama vingine ndani ya umoja huo.
 
Sungura anaongea ongea naye aonekane

ili asajiliwe na ChichiM kwenye dirisha dogo la January. Ataambulia kupelekwa kwa mkopo a*t
 
We endelea kulalamika, mwenyekiti wako alipewa chake mapema akatulia, sahivi anafaidi mihela ya mmasai tu hana neno na mtu
 
Wakati wa Kampeni kuna watu walisema hivi hivi kuwa LOWASA endapo akishindwa ktika chaguzi ile ndio utakuwa mwisho wake atajiondoa tena CDM kwani amefuata cheo na siyo uanachama.

Na ndio maana hata mwandishi wa BBC alipomuuliza hili swali alimjibu kwua akishindwa ataenda kufuga ng'ombe kijijini kwake!!!!!!

Watu wakashabikia kichizi!!!!!!

lakini leo wanashangaa bado yupo fit ndani ya UKAWA, na wanaanza tena maneno ooohh!!! anataka kuwa chairman wa CDM na Sumaye katibu mkuu; na hii yote baada ya kuona maneno yao yameyeyuka.

Mtasema mengi sisi bado tupo ndani ya UKAWA na CCM mtazidi kupata homa kwa hili
 
Huyu RAT kwanza siku zote ni kibaraka wa CCM; sisi tunaelewa kuwa UKAWA ina vyama vinne, hivyo ushindi wa mgombea wa chama kimoja ni kwamba amepata kura za wajumbe wote.

Aelewe kuwa hata Mbatia kuwa mbunge ni kutokana na kura za wananchi wote wa UKAWA na siyo wana NCCR peke yao.

Aache tabia yake ya kibinafsi, hapa ni mabadiliko tu ndio wimbo wetu.

RAT alitamani muungano wa UKAWA usambaratike wakati wa kampeni lakini walishindwa.

Daima haturudi nyuma, akitaka aondoke yeye atuachie NCCR yetu wanachama tupo ngangari kinoma.
 
kumekucha

Sina Usingizi !!!!!!.jpg

Ukawa and CCM.jpg
 
TAMKO LA LOWASSA LA KUTAKA KUGOMBEA TENA MWAKA 2020 LAANZA KULETA MPASUKO MKUBWA UKAWA,NCCRA MAGEUZI WAMKATAA LIVEE
MUUNGWANA BLOG / 8 minutes ago

KUFUATIA kauli ya aliyekuwa mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwavuli wa Ukawa, Edward Lowassa ya kugombea tena urais mwaka 2020, Mkuu wa Oganaizesheni wa NCCR-Mageuzi, Faustine Sungura amemhoji Lowassa kama atakuwa tayari kuendelea kutumikia Ukawa kama jina lake halitapendekezwa kugombea nafasi hiyo.

Akizungumza na gazeti hili jana, Sungura ambaye alisema anazungumza siyo kwa niaba ya chama, bali kwa kauli yake mwenyewe, alisema kauli hiyo ya Lowassa kupambana tena katika kinyang’anyiro cha urais mwaka 2020 kunategemea maamuzi ya chama kupitisha jina lake.

“Nimemsikia Lowassa anasema kuwa anajiandaa kupambana na Rais John Magufuli mwaka 2020, lakini je, yuko tayari kuheshimu maamuzi ya chama kwa maslahi ya wakati huo?” Alihoji Sungura.

Sungura alisema mwaka jana jina la Lowassa lilipochujwa kwenye wagombea urais ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) alijiondoa na kuhamia Chadema.

“Je, atakuwa tayari kuheshimu maamuzi ya chama pale ambapo jina lake halitapitishwa kugombea urais Chadema au atahamia chama chake?” Alihoji Sungura.

Akizungumzia ushindi wa viti vya meya uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, Sungura alisema ushindi huo ambao wameshinda wagombea wa Chadema na CUF usitafsiriwe kuwa ni ushindi wa Ukawa, bali ni ushindi wa Chadema na CUF .

“Nasema hayo kwa sababu ukizungumzia Ukawa unazungumzia vyama vinne ambavyo ni Chadema, NCCR Mageuzi, NLD na CUF, lakini kilichofanyika kuna baadhi ya kata tulisimamisha wagombea lakini walituwekea kauzibe tusipate,” alisema Sungura.

Sungura alisema baadhi ya vyama ndani ya Ukawa wana ubinafsi kuwachanganya watanzania kwa neno Ukawa ambalo halina maana yoyote badala yake kuviua vyama vingine ndani ya umoja huo.
 
mmh..huyu sungura sio bure kuna namna,kamuuliza swali zuri lowassa lakini kuhusu ukawa katumwa na ccm...amulikwe huyu.
 
Anaweza akahamia TLP
kama akikatwa.
na lazima wamkate maana kazi yake imeisha.
He is totally useless
 
NLD wamepata mgao wa VITI MAALUMU au kauli mbiu ya MOTO..... MOTO.... MOTO... haikuchangia kura yoyote ndani ya UKAWA!
 
Back
Top Bottom