NCCR Mageuzi: Hatukubaliani na kikao cha TCD kilichoitishwa Dodoma

Mwenyekiti wa chama cha Nccr Mageuzi James Mbatia kwenye video hii amenukuliwa akisema kwamba kwenye swala zima la kudai katiba mpya na uhuru wa vyama vya siasa wamemshitukia Zito Kabwe kuwa ni dalali wa serikali anayelenga kukwamisha jitihada za kupata katiba mpya kabla ya mwaka 2025.

Kitendo cha Zito kuwemo kwenye kamati iliyopendekeza katiba ipatikane baada ya uchaguzi mkuu wa 2025 kimewasikitisha sana.

View attachment 2175517

AYATOLLAH ZITTO ZUBERI KABWE
 
Mbatia hana lolote bali chawa tu wa chadema. Lazima awe upande wa chadema kwa Kila jambo. Kwasababu anategemea kuachiwa Jimbo la vunjo. Anaogopa kuwakera chadema cos anajua kama chadema wakisimamisha mgombea vunjo mbatia hatoboi.
Tofauti na Zitto katika majimbo ya kigoma mjini na kigoma kaskazini hata kama chadema wataweka wagombea Zitto anatoboa kwa asilimia nyingi tu.
 
Nakukumbusha

1) Mchakato wa Katiba mpya ukianzishwa na 'Mvaa Kobaz'

2) Nakukumbusha nyinyi 'msiovaa kobaz' kupitia Mzee Edwin Mtei mliipinga Tume ya Warioba kwa kuwa mvaa kobas alijaza Wavaa kobaz wenzie…hadi mkamshinikiza Hayati Prof Mwesiga Baregu ajitoe akakataa kwa hoja ikibidi kuchagua Chama au Taifa atachagua Taifa

Mkiwa Wajinga sio lazima muwe pia wasahaulifu

Nchi hii nzuri sana …mkianzisha Siasa za Udini mnufaika mara zote huwa ni CCM kwa kuwa Raia wenye misimano ya ubaguzi wa kidini dini huwa ni wachache sana na Raia wengi sana huwapuuza …ukibisha rejea uchaguzi wa 2010
Bwana nyepesi ni ndugu yake hangaya katika Imani

Zam za wavaa kobaz hiz

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Mwenyekiti wa chama cha Nccr Mageuzi James Mbatia kwenye video hii amenukuliwa akisema kwamba kwenye swala zima la kudai katiba mpya na uhuru wa vyama vya siasa wamemshitukia Zito Kabwe kuwa ni dalali wa serikali anayelenga kukwamisha jitihada za kupata katiba mpya kabla ya mwaka 2025.

Kitendo cha Zito kuwemo kwenye kamati iliyopendekeza katiba ipatikane baada ya uchaguzi mkuu wa 2025 kimewasikitisha sana.

View attachment 2175517
huyu ni mamluki ndo maana alifukuzwa chadema.
 
Zitto ntu ya dili..... ila wanasiasa wote ni kopo na mfuniko. Huyo Mbatia mwenyewe enzi za Mwendazake alikua toy ya jiwe katika kufanikisha mipango yake kisiasa kupitia upinzani
Mapinzani ya Tanzania ni matakataka tu!
 
  • Thanks
Reactions: PhD
Inaonekana Zitto ni turufu Muhimu sana kwenye Mchakato wa Katiba ndio maana anatajwa tajwa sana kukwamisha Mchakato wa Katiba mpya.

Kwanini NCCR na Chadema wasiendelee tu na michakato yao kuishinikiza Serikali wakaachana na Zitto, mbona Zitto anaendelea na michakato yake ya 'kukwamisha katiba mpya' bila ya kumtaja Mbatia kuwa anataka kukwamisha harakati zake za kukwamisha Katiba mpya?

Nahisi kuna kamchezo ndani ya NCCR na Chadema kwa kujua au bila ya kujua kumuongezea thamani Zitto kwny macho ya Watawala.
Labda kwa watanzania wendawazimu, Zito ameongezewa umaarufu.

Zito ni kibaraka hatari. Anatumika na CCM kwenda kinyume na matakwa ya wapinzani na watanzania wengi wenye uelewa ili makundi haya yakisusia uchaguzi, yeye Zito atumike na CCM kama chama cha upinzani, agawiwe wabunge, na kisha ahesabike kama kambi rasmi ya upinzani.

Lakini kamwe hatafanikiwa.
 
Hapo chacha, vyuma vimeumana
wasichokijua CHADEMA na NCCR ni kwamba waende wasiende CCM na Dola watafanya walitakalo. Miaka 6 iliyopita Magufuli hakutoa hata dakika moja kwa chama kukutana, leo inatokea fursa mnahamisha goli sababu eti ZZK yupo. Vyama vingi hapa nchini ni uhuni.
 
Ayatollah Zitto Zubeir Kabwe ni Mrema aliyechangamka ✈️
 
Ndio Denokrasia

Kila mtu ana haki ya kufanya siasa anazohisi zinafaa

Wewe una haki ya kuona ianze katiba mpya…mwingine ianze tume huru…mwingine ikarabatiwe iliyopo…mwingine tuvute subira kwanza…ndia siasa hizo na kila aliekinyume na maoni yako ukiona ni msaliti itakuwa unajitesa sana

Mbona nyie mliikataa Tume ya Warioba mara tu baada ya kuundwa mkamtaka Baregu ajitoe…lakin baadae mkaikubali kazi ya hiyo Tume na Mh.Jakaya hakuwazodoa?

Back
Top Bottom