NCCR Mageuzi: Abadani hatutaruhusu nchi kurudi kwenye mfumo wa chama kimoja. Mbatia adai alifukuzwa UDSM akipigania mageuzi

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
34,099
2,000
1582185284731.png

Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi amesema wale vijana wadogo kwenye Siasa wanaodhani watairudisha nchi hii kwenye mfumo wa chama kimoja wanajidanganya na kuota ndoto za mchana.

Mbatia amesema alifukuzwa Chuo Kikuu pale UDSM tarehe 10/02/1992 siku ya Jumatatu kwa sababu ya harakati zake za kupigania mfumo wa vyama vingi. Anadai aliporwa haki yake ya elimu hali iliyomlazimu kupata elimu ughaibuni huko Uholanzi.

Naye Wakili Joshua amesema mfumo wa chama kimoja ni ugaidi kwani watu hutafuta haki zao kwa kutumia mapanga na marungu.

Source: ITV Habari

Maendeleo hayana vyama!
 

kalemauji

JF-Expert Member
Jun 24, 2014
1,016
2,000
Mhhhh! Wanasiasa hamna tofauti na Yuda eskalioti wengi wapo kwa ajili ya matumbo yao tu na si kingine mwanasiasa wa kibongo hana tofauti na ile jinsia nyingine yenye tamaa
 

ZENJIBARIA

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
574
1,000
msitupumbaze hii nchi haijawahi kuwa na vyama vingi,ni chi ya mfumo wa chama kimoja na nyie nyote ni watetezi wa chama kimoja.

katiba inatambua chama kimoja vyombo vyote vya dola vinatambua chama kimoja,acheni kufanya watu wajinga
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom