Nccr: Fomu na ilani kutolewa april 2010

Charuka

Member
Oct 20, 2009
56
18
CHAMA cha NCCR-Mageuzi kimetangaza kuanza kutoa fomu za wagombea urais, ubunge na madiwani kuanzia mwezi Aprili, kwa ajili ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.

Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia alitoa kauli hiyo alipozungumza katika kipindi cha Jambo kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha Taifa TBC 1.

Mbatia alisema kwa sasa, chama chake kipo katika maandalizi ya kutengeneza Ilani mpya kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujaona kwamba kazi hiyo inaendelea vizuri.

Alisema ilani itakamilika kabla ya Machi ambapo sasa chama kitaanza kutoa kutoa fomu kwa wanachama wake kwa ajili ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea nafasi mbalimbali mwanzoni mwa mwezi Aprili.

"Kila kitu kitakuwa wazi kuhusu wagombea wetu wa nafasi ya Urais, Ubunge na Udiwani mwanzoni mwa Aprili. Na hapo ndipo itajulikana kama na mimi nitagombea au la," alisema Mbatia.

Akizungumzia malumbano ya kisiasa yanayoendelea nchini kwa baadhi ya wanasaisa, Mbatia aliwalaani wanasiasa wanaomini kuwa maoni yao ndio bora na yenye haki zaidi kuliko ya wengine.

Alishauri mwaka 2010 uwe mwaka wa kupambana kwa hoja, ili zisaidie kupanua na kuongeza wigo wa uelewa wa Watanzania katika masuala mbalimbali na nyeti ya kitaifa na kimataifa.

"Nalaani wanasiasa wanaojiona kuwa maoni yao ndio yenye haki na bora na kupuuza maoni ya wengine. Mwaka 2010 tuutumie kwa kushindana kwa hoja ili tuwaelimishe zaidi Watanzania masuala nyeti yatakayosaidia kuchochea ukuaji wa uchumi na maendeleo,"alisema Mbatia.

Hata hivyo Mbatia alisema wakati umefika kwa Watanzania wa kada zote kuacha tabia ya kulalamika na badala yake waelekeze nguvu katika kujenga na kuibua hoja mbalimbali zitakazosaidia kukuza uelewa na kuchochea maendeleo katika nyanja zote.

"Hatuwezi kuwa ni watu wa taifa la kulalamika tu bali tunatakiwa tuwe ni taifa lenye watu wenye uwezo wa kujenga au kuibua hoja zitakazosaidia kutujenga kifikra, na kutuletea maendeleo," alisema Mbatia
Mwanasiasa huyo kijana alisema malumbano yanayoendelea sasa ya mtu na mtu au kundi moja na lingine hayana faida yoyote, lakini yanahatarisha usalama na amani ya nchi.
Source; Mwananchi 10th Jan
 
Back
Top Bottom