NBC: This is not fair!

dorin

JF-Expert Member
Jan 29, 2010
267
285
Wakuu!
Nilibahatika kufungua Account Na NBC Hapa Dar. Tangu 2002. Mpaka sasa naitumia hii account.
Hivi majuzi nimeingia Mkoani nilikua na shida ya pesa ambazo singeweza kuzitoa kwenye ATM ikabidi niingie Ndani Kwa teller!! Huku nikiwa na statement niliyo itoa kwenye ATM kama Kidhibitisho kuwa mimi ndio mwenye Account.
Niliambiwa wanatakiwa kutoa kitambulisho changu cha Benki Copy wakitume Dar Es Salaam Kwenye Branch Yangu Ndio Niweze kuruhusiwa kuchukua Pesa(Tshs 1,200,000) Ambazo Mtu anaweza kuzitoa kwenye ATM kwa siku Mbili.
Wadau nilikaa pale Benki Kwa zaidi ya masaa matano nasubiri Repply ya Fax Kutoka Dar. Ikabidi nianze kufoka Hapo Ndipo wakaamua kutumia Njia Nyingine ya kuniuliza maswali yanayo husiana na ile account yangu Nikajibu vizuri ndipo wakanipa hela.
Kwa hasira niliyopata, Nikirudi Dar I will Take all my Money From That Account and I will never ever do Business with You Guys!!
Hayo maswali waliyoniuliza baada ya kukaa masaa matano Mbona wasingeniuliza mwanzoni wakanipa changu nikatimua!!
Am Really fed up with you otherwide mjirekebishe.
 
NBC ni benki kimeo sana, system yao haiko reliable,mtu ukitaka kuchukua pesa ndani lazima uende kwenye ATM uchukue statement ndiyo upate pesa,...

Kibaya zaidi kwenye ATM kuna que as well as kwa teller..

Unaweza kutumia more than 7 hours to get your own cash....
 
NBC ni benki kimeo sana, system yao haiko reliable,mtu ukitaka kuchukua pesa ndani lazima uende kwenye ATM uchukue statement ndiyo upate pesa,...

Kibaya zaidi kwenye ATM kuna que as well as kwa teller..

Unaweza kutumia more than 7 hours to get your own cash....

Bora ungeenda na hiyo statement ukapewa pesa!! uliza kinachfuata baada ya kwenda na hiyo statement kama hapo benki hufahamiki......
 
Hata CRDB wanalo hilo tatizo. Lakini ata least wao inaweza kuchukua some few mninutes kama 'ukiwafokea'. Sidhani kama wanaitumia vya kutosha technolojia ilivyopo. So sad.
 
Kwa kweli sijawahi Bank na hizi benki za kizawa, sijaonja joto ya jiwe ila wife yupo NMB(kwa kweli sometimes mpaka unatamani unekuwa na KALASHNIKOV (AK-47) uwachape wote risasi maana utawaona wale ma teller wapo pale physially tu lkn mentally hawapo kabisaa, foleni imejikunja km mara nne hivi wao utawaona wanapiga story tuuu ndani mle
 
Dah pole sana lakini afadhali ya wewe ulihudumiwa wengine huwa tunatolewa mikono mitupu mi huko nimebakiza 50,000/= ya kulinda account yangu endapo wataboresha huduma zao. Maana inachosha na kusikitisha account yako kadi yako na kwenye ATM kadi kuna picha yako alafu jamaa wanaanza kukuzingua wkt pesa zako.
 
Jamani ni Bank gani ni nzuri kihuduma. hili swala limekuja wakati nataka kufungua acount na NBC ilikuwa mojawapo, nilitafuta na bank nyingine just to compare.their services, currently niko CRDB , ningependa kuwa na separate bank accounts for some reasons. natafuta bank ambayo haina ubabaishaji na ni nzuri kwa mfanya biashara.
wataalamu nisaidieni.
 
Hapo umenena mkuu! Kwa heshima na mimi naoma niendeleze ka-mchango kangu dhidi ya benki hii ya makaburu.

Kuna mambokadhaa niliyo-note ambayo mimi binafsi sikuvutiwa nayo. Moja ni juu ya kuchukua pesa pale unapokuwa mbali na tawi ulilofungua akaunti yako. Hawa jamaa walianza kwa awamu. Awamu ya kwanza ilikuwa ni ni kuchukua salio kwenye ATM kabla ya kuingia ndani. Ukishakuwa na salio basi unapata pesa yako. Awamu ya pili wakaja na suala la kuchukua salio linalotosha kwa siku yaani laki sita (600,000/-) kupitia ATM na zinazobaki ndo unazichukua kwenye teller ndani.
Walipomaliza na hiyo awamu ya pili wamekuja na kimeo zaidi, kwanza uchukue laki sita kwenye ATM na zinazozidi hapo uende ndani wakatume fax kwenye tawi lako mpaka utakapojibiwa ndo upewe hela yako. Na kitu kinacho-udhi zaidi ni paleunapoambiwa nendapale ukatume fax wakikujibu ndo utapewa pesa yako.
Kuna siku siku nilihitaji 2m nikachota laki sita kwenye ATM baada ya foleni hiyo nikapanga foleni nyingine ya ndani nkiwa na receipt nilizochukulia pesa kkt ATM. Baada ya kufika kwa teller, akanielekeza ofisi nyingine. Nikafika hapo nikakuta mama mmoja asiyejua customer care, akanieleza nenda pale ukatume fax wakikujibu nitakupa pesa yako. Nikamuuliza maswali ya kutaka kujua kwa nini wanasababisha usumbufu kwa wateja kana kwamba hawana kazi nyigine? Akanijuibu hawajakataa kunipa pesa. Nifate taratibu hizo nitapewa hela yangu. Baada ya hapo ikaonekana kuwa fax haziendi na nikawa bored nikaondoka mpaka benki nyingine kungua akaunti mpya. Kwa sasa sehemu kubwa ya pesa yngu iko kwenye akaunti mpya ambapo kwa safari zangu nakula good time kwani nikihitaji pesa napata kwa wakti.
Jambo jingine lililoniudhi juu ya hao NBC - kaburu Ltd ni pale nilipotaka kufungua akaunti za wanangu. Nilienda pale nikiwa na vitambulisho vyangu na picha za watoto na nikiwa nao na kadi zao za kuzaliwa. Kilichonishangaza ni pale waliponitaka nijaze fomu na pia niende kwa mjumbe zikaidhinishwe kwamba ninakaa mtaa huo na pia niende na salary slip yangu. Sasa nikajiuliza hivi hawa jamaani wazima ama wameoza? Inawezekanaje utake maelezo yote hayo kwa mtu ambaye tayari ana akaunti mbili kwenye benki yenu? Je, km ni mshahara si unapitia hapo hapo kwao? Je, hizo akaunti za baba hazitoshi kuwadhamini watoto?

Wizi mtupu!!!

Kwaherini NBC na wizi wenu kupitia ATM. Kwa sasa nimebakiza kidole nachenyewe muda wowote nitakiondoa maana JUMBO akaunti nimepata bila mizengwe.
 
Pole ndugu yetu Dorin.La kusikitikitisha kuliko yote wanaoyafanya haya ni ndugu zetu tunaokaa nao uswahilini na sio makaburu.Baadhi ya haya mambo wanayoyafanya ni kwa usalama wa pesa zetu-sawa(watu wametumia sana loop hole hiyo kuiba sana pale NBC),uzembe wa wafanyakazi wao-hawa wazeee waliowarithi kutoka NBC ya kikoloni,hujiona wao ni miungu watu na wamejawa na red minds.Hayo yote ukiyachanganya matokeo ndio hayo,la kusikitisha ni pale unapomueleza m TZ mwenzako kuwa umekuja pale umetoka kazini, sasa ni zaidi ya masaa 7 akusaidie urudi kazini anasema nenda urudi kesho kama huwezi kusubiri, ungejua una haraka ungekuja jana.Lakini hawa hawa wakiburuzwa wanabadilika sijui mwokozi atoke wapi!
 
Hata CRDB wanalo hilo tatizo. Lakini ata least wao inaweza kuchukua some few mninutes kama 'ukiwafokea'. Sidhani kama wanaitumia vya kutosha technolojia ilivyopo. So sad.

for that case benki zote zilizo angalau na matawi hata mikoani ziko hivyo, I mean NBC, CRDB na NMB. sasa ukifunga ya NBC where do you go?

Damn!!!!!!!!!
 
The problem kubwa kwa Bank zetu customer care is big problem. The same to NMB kuna sikunilikuwa Arusha natakiwa nimwekee mtu pesa ambaye akaunti yake ipo NMB Wami Branch Morogoro. Huwezi amini kwa two days ilishindikana kwanihakukuwa na network tena Branch zao mbili za Ngarenaro na Clock tower, Tena imenifanya niwachukue pale wanapojitangaza kwa kutoa hela kwenye mipira. kwanini wasiimarishe IT Department?
 
The problem kubwa kwa Bank zetu customer care is big problem. The same to NMB kuna sikunilikuwa Arusha natakiwa nimwekee mtu pesa ambaye akaunti yake ipo NMB Wami Branch Morogoro. Huwezi amini kwa two days ilishindikana kwanihakukuwa na network tena Branch zao mbili za Ngarenaro na Clock tower, Tena imenifanya niwachukue pale wanapojitangaza kwa kutoa hela kwenye mipira. kwanini wasiimarishe IT Department?

Hiyo kitu NMB hata mimi siwaelewi kabisa inapokuja kufadhili mashindano ya mpira wakati IT ni kimeo kupindukia. Priority iko ktk kujitangaza tu?
 
Am sorry Geoff. wewe bado mdogo katika maswala ya ndoa!!! siku nyingine ukifika kwenye signature yangu funga Macho. Pole sana mdogo wangu
im out of topic,did u get that husband you were looking for?
 
NBC wazinguaji sana, mimi mara kadhaa nimeahirisha zoezi la kuchukua pesa kwa sababu ya ususmbufu wao, watakwambia tumeshatuma faksi tunasubiri majibu na hiyo ndio inakuwa imetoka. shiiiiiiiiit
 
Kwa ujumla...customer service bongo ni UZEMBE! Benki shida, madukani shida, serikalini shida...how do we expect to develop? Yani it's shocking kwa kuwa na service mbovu hivi! The private sector has to take charge. Lakini in bongo...it's the opposite!
 
Dorin hivyo vitu vipo sana NBC . wanaboa sana Pesa yako mwenyewe inakutesa imeshanitokea pia .
 
Pole sana Dorin, Mimi siku moja ilisha nikuta niko mlimani city NBC Jumapili nataka nihamishe pesa zangu kutoka A/C yangu ya NBC kwenda kwenye A/C yangu nyingine ya NBC na pesa nilikua nahamisha ni zaida ya laki sita na baadae nilikua nataka kufanya transaction nyingine kwenye ATM so ilinilazimu niiingie ndani ya benk, yule teller aliniambia kitu cha ajabu kwamba hawezi kuaccess account yangu kwa vile brach niliyo fungulia A/C yangu imefungwa na wakati huo huo nime deposit pesa kwa huyo huyo teller kwa A/C yangu, Nikambishia nikamwambia kama umeweza kudeposit kwa nini ushindwe kutoa hiyo pesa?, Nikamwambia nini maana ya ku centralize information za wateja na hiyo kitu inafanyika kwa benki yenu?, akutulia baada ya muda kidogo akanza kuniuliza maswali yao ya kizushi kama walio kuuliza na ndio akakubali kufanya hiyo Transaction. Sasa hiyo tutasema ni ufahamu mdogo wa wafanyakazi wa Benki hiyo au ni Taratibu za NBC? This is real Dam Shit
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom