NBC na TRA waibiwa zaidi ya Tsh 15bn/- | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NBC na TRA waibiwa zaidi ya Tsh 15bn/-

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwenda_Pole, Jul 28, 2009.

 1. Mwenda_Pole

  Mwenda_Pole JF-Expert Member

  #1
  Jul 28, 2009
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 260
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  AUTHORITIES are investigating alleged fraud within the National Bank of Commerce (NBC) that has led to the disappearance of at least 20bn/- from the accounts of some of the bank’s key corporate customers, including the Tanzania Revenue Authority (TRA) and Tanzania Telecommunications Company Limited (TTCL).

  According to latest THISDAY findings, some NBC officials at various branches in Dar es Salaam are suspected to have colluded in the facilitation of fraudulent transactions with local businessmen.

  In one incident of fraud so far detected by bank officials, around 15bn/- was stolen through the use of fake companies and manipulation of electronic payment systems.

  Informed sources say another incident involved the embezzlement of 5bn/- earlier this year through use of the name of one particular construction company.

  A co-owner of a local magazine along with a number of NBC employees are believed to be under investigation following the discovery of over 4.5bn/- in vanished monies from bank accounts owned by TRA and TTCL, both state-owned enterprises.

  ’’The fraud was done through the use of fake names and identities. In some cases, the photos of deceased individuals were also used to facilitate the scam, ’’ said an informed source in the banking industry.

  NBC officials confirmed that a formal investigation has been launched into the matter, but declined to give details on precisely how much money has so far been stolen.

  ’’The management of the National Bank of Commerce (NBC) Ltd is not at liberty to comment on the alleged fraud incidents, while the matter is under investigation,’’ said a brief statement issued by the bank in the wake of queries from THISDAY.

  Police in Dar es Salaam are understood to be handling the investigation of the reported theft, with several NBC bank employees already subjected to questioning.

  The Director of Criminal Investigations (DCI), Commissioner of Police Robert Manumba, said he personally was not aware of the alleged fraudulent incidents at the bank.

  Manumba said Dar es Salaam police were probably better placed to offer details on the ongoing investigation.

  Investigating officers are believed to have last week questioned several suspects as part of the ongoing probe.

  There are reports of the probable involvement of various influential people, thus posing a more difficult challenge to the investigators.

  The formerly state-owned NBC Bank was privatised in 2000 to South Africa’s financial services giant ABSA Group Limited. Its shareholders are ABSA Group (55 per cent), the Tanzanian government (30 per cent), and the International Finance Corporation (15 per cent).

  Incidents of fraud in commercial banks and other financial services institutions have been on a rampant rise in the country over the past few years.

  A number of suspects are already facing criminal charges in Dar es Salaam in relation to such cases involving banks based in the city.

  Source: ThisDay 27th July, 2009

  My Take: hivi ni lini mali ya umma itakuja heshimika kama ni mali ya umma na sio mali ya wale waliopewa nafasi ya kusimamia?

  Namkumbuka sana Baba wa Taifa Mwl J.K. Nyerere
   
  Last edited: Jul 28, 2009
 2. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  And that's whay i did concur with Prof Kapuya on this matter. Watanzania walio wengi wanapoomba kazi, ishu si ile kazi but is what sorrounds ile kazi. Hili ni tatizo la kitaifa na inabidi ufumbuzi wa kudumu utafutwe!!!!!!!

  Mtu anakuja kwenye kampuni yako kuomba kazi yeyote lakini akiwa amelenga kufanya wizi ili eti atoke......... Na mbaya zaidi tz kuibia kampuni au serikali inaonekana si wizi. I guess tumetoka nayo kule kwenye mambo ya ujamaa. Ni aibu and it is eveywhere to every age group.
   
 3. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #3
  Jul 28, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,896
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  This kind of thing inanikera sana. Yaani sana. Hivi systems za hii nchi zimekaaje jamani?
   
 4. b

  bnhai JF-Expert Member

  #4
  Jul 28, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,207
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Sie Watanzania ndio wa wanza kulalamika wakati ndio tunaofanya uhalifu mwingi kwenye systems zetu. Nadhani iwe kama kampeni ya HIV tulaunch awareness kutokomeza hali hii. Generally inasikitisha saana
   
 5. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #5
  Jul 28, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Jamii yetu imeharibika tangu enzi za Rais Mwinyi (watu walipokuwa wanaenda kazini Long Room na kurudi nyumbani na box la hela.!!), sasa wezi na wahujumu uchumi wanaonekana wajanja. Wale waofanya kazi kwa uadilifu wanaonekana wajinga. Tumefika pabaya sana kugeuka kutoka hapa ni kazi ngumu kweli kweli kwa sababu yote haya yanahusu hela. Sehemu kuwa ya Watanzania nao wao wanataka kulipwa BIG iwe kihalali au vinginevyo...I guess hiyo ndio ungly side ya ubepari.

  My fav rapper once rap

   
 6. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #6
  Jul 28, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Hatari kubwa. sasa hivi ni nani mwaminifu huko Tanzania?
   
 7. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #7
  Jul 28, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 160
  Niliwahi kuandika kwenye hii topic (tarehe 23 Julai 2009):

  Bank ya NBC mitambo yake ina kwikwi

  Hivi:

  Na wengi nadhani hamkujua kama nilimaanisha hili!
   
 8. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #8
  Jul 28, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  wizi kama huu ni easily traceable lakini jinsi baadhi ya waTanzania tulivyo, hao wataopewa kazi ya ku-trace, wakikatiwa na hao walioiba, basi mambo ndio yataishia hapo hapo.
   
 9. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #9
  Jul 28, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  ...nadhani sio hatua moja tu mkuu ni zaidi ya hapo.
   
 10. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #10
  Jul 28, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Watanzania wengi huwa hatupendi kuambiwa kuwa hatujui, hili ni tatizo namba moja, wenzetu wa ulaya wanakitu wanakiita FEEDBACK, yaani mtu anakupa nafasi ya kumkosoa na akikosolewa yale uliyompa anayaita Changamoto (Challenges) alafu anayafanyia kazi, akiyafanyia kazi anakuja kukuuliza tena feedback. (how do you see now? do you think we have improved? are you happY?)

  Sisi tumekalia ubishani kama ule wa simba na yanga kwenye vijiwe vya kariakoo, hata kama tunajua beki wetu wa kutegemea kaumia ni majeruhi, tutabaki kusema tupo fit. Wataalam wetu hawapo tayari kusema hapo tumeshindwa, hawapo tayari kusema tunaomba msaada, ukizingatia matop wao (madingi wa 47) wapo nyuma sana kwenye teknolojia kwa hiyo wasipowashauri hao madirector wa kibongo wanaona sawa tu.

  Hii kasumba ipo kila mahali, ukienda kununua nguo, unakuta muuza nguo hakwambii kuwa zip haifungi, ukiingia mgahawani chakula kina pilipili utasikia chakula kitamu sana, kwenye dala dala ndio kabisa wanakwambia ulisikia wapi gari inajaa, inajaa ndoo ya maji.

  Watanzania tu wabishi mpaka ubishi usio kuwa na faida ule wa Abunuasi. Tubadirike sasa, maneno mingi haitusadii, hizo pesa sasa hivi zimeshatambaa zipo viwanja vya mbali kwa walio endelea. Huu ni ujinga wa hali ya juu, tunaiba kwetu (choka mbaya) tunapeleka zinakotengenezwa, wakati huo huo na wao wanaiba madini, meno ya tembo, miti yetu na mbao. Bado tunaiba hata tupesa kwenye benki ya wa lala hoi kama NBC na kutuvusha bahari kwenda Ng'ambo. INAUMA sana ukifikiria kwa makini, Unajiona mimi na wenzangu wadanganyika tu-Mabwege
   
 11. Kabuche1977

  Kabuche1977 JF-Expert Member

  #11
  Jul 28, 2009
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mimi nafikiri Mbogela you are right, Watanzanaia tuna matatizo sana, tunaiba hata dawa ya mswaki nyumbani kwetu, yaani mtu ameweka hela kwa ajiliaya chakula nyumbani wakati wa kwenda kazini anakwapua zile hela na kujiona yeye mjanja, jioni akirudi nyumbani anaanza kudai chakula, akiambiwa hela ilipotea anakuwa mkali, yaani ndo watanzania tulivo sasa, sasa wewe imagine mtu anaenda kuiibia benki cha kusikitish naye ni mmoja wa wateja wa ile benki, just imagine, ikifika wakati wa kuchukua pesa akiambiwa hakuna basi anakasirika.

  AKILI IMDUMAA KWA KWELI.
   
 12. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #12
  Jul 28, 2009
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,400
  Likes Received: 432
  Trophy Points: 180
  Watanzania tu wabishi mpaka ubishi usio kuwa na faida ule wa
  Abunuasi.

  Siyo Wabishi, bali ni Washamba na wajinga wajinga tu!!
   
 13. Alwatan

  Alwatan JF-Expert Member

  #13
  Jul 28, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 409
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Mi nafikiri kikwete lazima abebe lawama kwa jinsi nchi inavyoenda shagala bagala. Hakuna heshima kabisa kwa mali ya umma. Na hii inatokana na kesi za mafisadi kuonekana kiini macho mbele ya jamii. JK angekua mkali si kwa kuonekana bali kwa vitendo, watafuna nchi bila kunawa wangepungua sana as wabongo waoga sana kunyea debe gerezani wakaacha wake zao mjini.

  Hili tatizo la mabenki lipo muda mrefu kama mwaka wa pili huu, na lilipofikia sasa limekua ni fashion ya mfanyakazi wa benki, usipowapiga(kama wenyewe wanavyoita wizi) wewe **** na hufai. kama kuna kijana hasa wa kwenye branches za nje ya makao makuu kwa Dar, au mikoani hasa morogoro, dodoma, shinyanga(ambako hii mihela ya wizi wanaenda kuichomolea) ambaye hataki kushiriki huu wizi wanamwita majina ya kishenzi na kumtishia kumng'oa kwenye hizo sehemu. Sababu kubwa ni washiriki wa huu wizi, wapo pia mabosi wachache wanohusika moja kwa moja na wizi. Wengine wamekua ni perrenial wapigaji na wakiwekwa ndani wiki kuua noma ndio kesi imeisha hivyo, anaenda kutumbua na anarudi kazini kwa position ileile. Kesi ndo imekufa tena!

  Hivi sasa si Stanbic, NBC, Standard chattered, Barclays na mpaka Citibank(wenyewe wapigaji wanakiita kigingi hiki), koote kumeoza na huu wizi wa kuhamisha pesa toka kwenye corporate accounts za mashirika ya umma kwenda kwa watu wenye accounts zilizo active(zenye mzunguko mkubwa) ili zikachomolewe mbele ndio the rule of the day na mwenye hio active account anaachiwa chake kwa kufacilitate pesa kupitia kwake.

  Kuna baadhi ya investors wameshaanza kuraise concern na wanatishia kulifikisha magogoni, na ubaya zaidi, wale ambao utadhani wanakuja kusaidia uchunguzi(Vijana wa Saidi Mwema) ndio wameoza kuliko hao waliochora huo wizi wa ndani. Yani hao vijana wa Mwema wanachotaka kujua ni pesa imeliwa kiasi gani?(ili wajue wataenda kula ngapi).... kwa mbinu ipi?( ili wajue wataharibu vipi ushahidi n.k), wataalam wao signature ndio usiseme, akishajua signature imefojiwa anatangaza dau kwa hao wezi ili awalinde kwa kusema signature ni halali. Halafu eti hiyo ya TRA, unaambiwa computer zinasema hela ya kodi ya TTCL imepokelewa lakini vijana wa Utouh walipoenda TRA wakakuta hesabu hazibalance...yani huu uozo wa taifa wa kumlaumu si mwingine, yupo mtu mmoja tu aliyepewa madaraka makubwa sana kikatiba kuweza kuweka displine kote huku within 100days kama akiamua...narudia KAMA!

  Kifupi nchi imeoza mno, JK amezidi mno kuchekacheka... Watu wanamtetea wee mpaka makoo yanakauka lakini wapi, yeye anachekacheka tu,...hajui kuwa anawachekea nyani kwenye shamba la mahindi, TUTAISHIA KUVUNA MABUA KWA MWENDO HUU...
   
 14. Sura-ya-Kwanza

  Sura-ya-Kwanza JF-Expert Member

  #14
  Jul 28, 2009
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 561
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hakuna jipya hapa!

  Lakini kuna ulazima wa kufiki ukomo.
   
 15. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #15
  Jul 28, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kuna mtu yeyote mwenye more info about those unnamed hapo juu. Ni vyema jamii ikaelewa kuwa ni nani yuko under suspicious and investigation. Nchi inaliwa na kutafunwa watanzania wanazidi kumenyeka na maisha magumu.
   
 16. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #16
  Jul 28, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 160
  Mimi sizunguki mkuu, ni Exel Magazine... Mmiliki wake si mnamjua? Walio karibu naye wanaweza kuongea zaidi!
   
 17. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #17
  Jul 29, 2009
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  WanaJamii,

  Hapa baadhi yenu mtadhani mimi ni "conspiracy theorist", lakini ngoja niwafafanulie kwa nini kiasi kikubwa kama hiki kimeweza kuibiwa, kwa njia rahisi mpaka inawachanganya wadau.

  1) Wizi wa aina hii hauwezi kufanyika bila ya kushirikishwa kwa watendaji waliomo ndani ya mfumo wa kibenki, hususan wale wanaohusika na idara ya ama mawasiliano ya kimataifa (international remittances) au uendeshaji (operations).

  2) Kumbukeni kwamba NBC "ilipobinafsishwa" kulikuwa na madai kwamba taratibu zilizofanyika ziliruhusu benki hiyo ambayo ilikuwa "mhimili mkubwa wa kiuchumi" hapa nchini iliuzwa kwa bei chee.

  3) Watendaji wazalendo waliomo ndani ya NBC ambao ndio wanaojua siri za utata huo, walikuwa wanatafuta muda wa "kuusoma vizuri zaidi" mfumo mpya wa kibenki, chini ya wawekezaji, kwanza kutoka ABSA na sasa Barclays, lakini bado haieleweki haswa "operations" ya benki hii ni ya Barclays South Africa au Barclays UK. Hili halijakaa vizuri.

  4) Mimi nawaita "wazalendo" lakini kwa upande fulani wamekosea. Kama ilikuwa ni suala la "kuchukua chao mapema" bora hata wangeiba (ingawa siridhiki na wala sishabikii wizi..., msinielewe vibaya.... wizi ni wizi) kutoka kwenye kampuni za "wawekezaji" ambao mimi nawaona ni wezi tu! Basi! Lakini kuchukua fedha kutoka TRA, TTCL na kwingineko, kampuni za serikali, hii inauma...

  5) Kwa kuwa hii ilikuwa "inside job", basi, kugundua nani aliyehusika ni rahisi, kwani, ukianza kufanya "audit trail" utagundua mfumo mzima wa nani anayehusika, katika uhamishaji wa pesa, kutoka akaunti moja kwenda nyingine, kwa njia ya elektroniki. Kama ziliundwa kampuni hewa, na yakatumika majina hewa ya wakurugenzi wa kampuni hizo, hakuna ambaye aliyeweza kujua siri hiyo kuliko mtu wa "ndani".

  Sasa, mtauliza. Imejulikana kwa namna gani?

  Kwenye "mpango kamambe" kama huu, ambao msimamizi wake mkuu (haonekani, lakini yumo...) ni Iblis..., lazima kuna mtu ambaye "atadhulumiwa" mgao wake. Huyu ndiye anayebumburusha "zali" lote na kuharibu kila kitu. Lakini hii ndiyo hali halisi ya "mipango yote ya kishetani", kwani Shetani hawezi kuruhusu fedha zinazoibiwa kwenye benki zitumike kuwanufaisha wanaozichukua. Hata siku moja. Lazima ahakikishe pesa hizo zinawaumiza wao wenyewe, zinaishia kwenye maasi zaidi, kuliko heri. Watazitumia kwa pombe, anasa, starehe za kila aina, lakini hawatanufaika nazo. Huu ndio utendaji wa Shetani. Mnakumbuka yaliyomtokea .... nani yule... nimeshasahau jina lake.... wizi wa zile pesa zilizoibiwa kwenye armored cash-in-transit vehicle, jirani na Dar es Salaam International Airport. Kwani zilitumikaje? Si aligawana na "maafande" na zilipokwisa wakamweka ndani? Kesi yake imeisha? Ah, nimkumbuka! KASUNGURA!

  Hawa hawatafika mbali, na kwa kuwa NBC imekata bima, fedha zimelindwa...

  Naishia hapa.

  ./Mwana wa Haki

  P.S. Mojawapo ya sababu ya pesa kuchukuliwa ni kisasi, cha wanyonge dhidi ya wakubwa, kwani mpaka leo pesa za wanyonge wanachama wa DECI (original) hawajalipwa fedha zao. Wanyonge hawa hawajatendewa haki, basi, kwa kuwa huu ni ushetani wa aina yake, kuwanyima haki yao, basi, Serikali nayo italazimika kupigwa mapanga mengi mpaka pesa zile zirudi, kwa wanachama wanyonge wale.... Nimesikia fununu ati zinangojewa kwenye kampeni 2010... ni kweli hayo?
   
 18. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #18
  Jul 29, 2009
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Invisibo, mtaje mmiliki wa Excel Magazine.... sisi wengine hatumjui.... LOL
   
Loading...