Nbc bank kuna wezi kuwa makini na account yako

Business integrity of this age is questionnable. Most people study and work to be rich in whatever means. It is a sign of wide and complex society problem that require multi-institutional approach.
 
Kuibiwa kwa fedha kwenye account za wateja wa benki za Tanzania kunasababishwa na mambo mawili makubwa:
1. UMBUMBU WA WATEJA: Wateja wengi wa benki za Tanzania ni wageni kwenye mambo ya technolojia za kibenki. Mfano kwenye matumizi ya Bank Cards, Credit Cards, ATM nk. Katika observation yangu nimegundua asilimia kubwa ya wateja ni malimbukeni wa kutumia hizo facilities. Na mbaya zaidi hata wale wenye kujua kuzitumia huwa hawachukui tahadhari na wanachukulia mambo kirahisirahisi.
2. WAFANYAKAZI WA BENKI KUKOSA UAMINIFU. Baadhi ya watu kama ma-programmer, ma-bank tellers nk hawaaminiki. Hili lipo benki zote kwani wengi wa Watanzania wana mindsets za wizi, hivyo wanashirikiana kwenye wizi.
 
Lakini ni kwa nini wamiliki wa mabenk hukataa kumrejeshea mlengwa pesa zake hata pale wanapokiri wizi kufanyika.!?
 
kwa ujumla hakuna faida ya kuweka pesa bank hapa tanzania kero zifuatazo..wizi,mtandao kuwa down,foleni,makato mengi
 
Mimi nilingundua salio kwenye account yangu ya NBC limepungua nikajaribu kuomba mini statement kwenye ATM haikuonyesha ndipo nikaenda ndani wakawa wakali nikaomba bank statement ikaonyesha loan arrears mkopo ambao nilishamaliza malipo yake mwaka uliopita. Baada ya kuwapa maelezo na vielelezo ikangundulika ni kweli sidaiwi nipo wakaniambia niandike barua ili niweze kunirudishia hela yangu hadi leo bado naidai bank. Ila kunadada pale counter kaniambia wateja wengi wanalamika hela zao zinapungu kwenye account bila kupatiwa maelezo ya kutosha toka utawala wa benk. Kwa hiyo siyo umbumbu wetu wateja ila kunawafanyakazi wa benki wanawaiba wateja kwa kutumia sababu mbalimbali. Kwa hiyo tuwe makini na account zetu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom