Nbc bank kuna wezi kuwa makini na account yako | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nbc bank kuna wezi kuwa makini na account yako

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by watambi, May 8, 2012.

 1. w

  watambi Senior Member

  #1
  May 8, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 178
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Kuna wafanyakazi wa kampuni moja. Wapo zaidi ya kumi wamejikuta hela zao zimetoweka katika mazingira ya kutatanisha katika akaunti zao Za NBC. Na kila mmoja kwa wakati wake alijaribu kufuatilia bila mafanikio.Ila walioibiwa wote ni wale wenye kadi mpya Za NBC.Je kuna mwanajamvi yeyote naye keshalizwa? Nawakilisha
   
 2. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #2
  May 8, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Itabidi sasa tuache kupeleka pesa Benki, kla siku ni hadithi za wizi, wizi, wizi tu!
   
 3. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #3
  May 8, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Unajua nilidhani ni izi local banks zetu tuu yaani mpaka Stanbic jamaa yangu walikwangua ela yake.
  Banks needs to be serious bse the cry is from all over acheni wizi
   
 4. kussy

  kussy JF-Expert Member

  #4
  May 8, 2012
  Joined: Jun 15, 2010
  Messages: 346
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Aisee sio NBC tu! Wiki iliyopita nami niliibiwa kwenye Account yangu ya CRDB mpaka leo bado nafuatilia, kuna watu walikuwa wanatoa hela toka kwenye Account yangu kwa kutumia EXIM bank, mpaka leo nafuatilia
   
 5. m

  msitaki Member

  #5
  May 8, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 69
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 15
  stanbic ndo hakufai kabisa..kuna shida kubwa kwenye benki zetu za tanzania..hakuna maadili na wala hawajali wateja kabisa..
   
 6. M

  Mabelana JF-Expert Member

  #6
  May 9, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 441
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 60
  Kiukweli hii habari inasikitisha sana wengi wameibiwa sana na siyo hapa nchini tu, vilio hivi vipo sana sehemu nyingi na sisi wenyewe wateja inatubidi tuwe makini unamkuta mtu anachomeka ATM card kuomba kudraw fedha na anaomba apatiwe list baada ya huduma ile list anaitupa kwenye kapu la taka, sasa wenzio watatumia hivyo vilist vyetu kuweza kusaidi kuingilia kwenye account yako. Jamani ukiomba list ondoka nayo kama huitaki bora usiombe kabisa.
   
 7. C

  Cool Member

  #7
  May 9, 2012
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 98
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Jamani hata mie nimeibiwa kamshahara ka mwezi huu. Nimekuta vipesa kiduchu. Hadi sasa nahaha namna ya kuishi, ndo naanza kufuatilia
   
 8. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #8
  May 9, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,088
  Likes Received: 6,554
  Trophy Points: 280
  Wizi wa mabenk umeanza zamani sana
  hata kabla ya teknolojia mpya
  kuna teller pale mbeya alikuwa akikuhesabia hela anadondosha chini kwenye
  miguu yake hasa anapoona una haraka huwezi kucounter check.

  sasa ndo wanaiba kwa kwenda mbele
  ila mchongo unakuwa wa wafanyakazi wa humo humo ndani ya benki.
   
 9. g

  guta Senior Member

  #9
  May 9, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 179
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Fuatilia ujue ni ATM gani pesa zako zimetolewa, ukishajua nenda exim uwaombe wakuangalizie picha. mimi niliibwa namna hiyo kujakufuatilia nikakuta ni mtu wangu karibu ndo kaniibia kadi yangu. nilishawahi kumtuma akanichukulie pesa nikampa namba ya siri.
   
 10. ze encyclopedia

  ze encyclopedia JF-Expert Member

  #10
  May 9, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 271
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  mSiogope jaman. kwa usalama wa pesa zako. na kujua kila kinachoendelea ktk akaunt yako 24/7 na teknolojia ya kibenk ya hali ya juu. tembelea FNB BANK. popote tanzania na upate kaunt yako leo. kwan una uwezo wa ku trace akaunt yako popote na wakat wowote.
  mi binafsi nimewakubali sana hawa jamaa yaani hata ikitoka shs 10 ktk ak.unt yako unapata sms na email notificatiom.
   
 11. MUREFU

  MUREFU JF-Expert Member

  #11
  May 9, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,230
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  kwa uelewa wangu mimi sio watu wanaibiwa isipokuwa sisi wnyewe tunajiipia kiukweli watu wengi sasa hivi wanapenda kununua vitu online. Na ndio sababu ya wao kuibiwa unapokuwa umeona kitu kwenye internet alafu ukataka kununua kwa kutoa VISA,MASTER CARD au NYNGNE YOYOTE inayoweza kukuruhusu wewe kununua hicho kitu. swali ni kwamba unauhakika gani na huyo unaempa bank account yako online tena password? watu wengi wanaibiwa na kukombwa pesa zao kwenye accont alafu mwisho wa siku wanawasingizia bank fulani wamemuibia pesa hiyo kitu haipo bank wapo kwa ajili ya kutrust wewe wapo kwa ajili yako so ndugu zangu UNAJIIBIA MWENYEWE
   
 12. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #12
  May 9, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Kuna kitengo ndani ya bank kinaitwa "Risk Management" hao ndio wezi balaa hao watu,yani wanapitia kila accoount wanacholopoa mia hadi buku 2000 sasa wakifanya hvyo kwa wateja 500,000? Ni sh ngapi wanaingiza kwa mwezi kwa wizi? BOT mmelala tu na mmekalia politiki wenzenu wanatuibia!! Ukitaka kujua mabenk wanaiba we ulizia bank statement ya mwezi tu halafu angalia makato yako yani utakuta kwa mwezi kalipia elfu 7 hadi kumi haionekani ilipo!!
   
 13. M

  MTUMISHI WA WATU New Member

  #13
  May 9, 2012
  Joined: May 8, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani tusiwalaumu sana wafanyakazi, ukitoa taariza za account yako kwenye internet, ikiwemo pamoja na kadi namba yako, unaweza kuibiwa na watu wanaojiita 'hookers'. zaidi unaponunua vitu online ni hatari pia, swapping of your master card on the point sales, be careful do not leave receipts behind, if does not print cancel the transaction.
   
 14. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #14
  May 9, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  na hao walioibiwa wanaweza ku-trace account zao mahali popote na ndio maana wamegundua kuwa wameibiwa mkuu.

  Katika suala la maendeleo ya teknolojia hakuna wa kupona kwani hata hao waiozigundua wanaweza kuibiwa na wakagundua wakati pesa zilishaliwa!
   
 15. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #15
  May 9, 2012
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Risiti (au Receipt) mkuu
   
 16. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #16
  May 9, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,316
  Likes Received: 2,278
  Trophy Points: 280
  Mimi nimempa bibi pesa zangu anitunzie sitaki kujua anaziweka wapi..........Kwake hakuna riba,wizi, foleni ya ATM wala network down , ni kiasi cha kumwambia nahitaji 20,000.Unasubiria kibarazani anakuletea cash.

  Ila kuna service charge kama kg 1 ya sukari angalau kwa mwezi!
   
 17. yaser

  yaser JF-Expert Member

  #17
  May 9, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 1,373
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  advertisement...watakulipa?
   
 18. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #18
  May 9, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,273
  Trophy Points: 280
  Ushamba na ulimbukeni unakusumbuwa wewe.
   
 19. Ennie

  Ennie JF-Expert Member

  #19
  May 9, 2012
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 7,145
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  Bora niweke chini ya godoro tu maana bank shida,simu pesa tabu aaargh!
   
 20. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #20
  May 9, 2012
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160

  Kwa kweli sijakuelewa - labda ndio ushamba wangu wenyewe!
   
Loading...