Kayemba
JF-Expert Member
- Jul 5, 2013
- 221
- 175
Naomba huu ujumbe uwafikie menejimenti ya Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi , NBAA.
Yahusu ucheleweshwaji wa matokeo ya mtihani wa Novemba 2017.
Kwanza kabisa hajawahi tokea kwa bodi kichelewesha matokeo ya mitihani kwa kipindi kirefu kama ambavyo mmefanya kipindi hiki. Kumekuwa na sababu lukuki mara hii mara ile zote ambazo sio rasmi. Ikumbukwe kuwa hakuna hata moja ya hizo sababu imetoewa na kurugenzi wala memenjimenti ya bodi, pia ikumbukwe mpaka leo ni miezi zaidi ya mitatu watahiniwa tuliotumia muda mwingi kwenye maandalizi, tumetumia pesa nyingi kulipia, tumeacha mambo mengi yamesimama ili tufanye hii mitihani, sasa bodi haijatoa matokeo ili watu tujue mustakabali wetu na bodi ipo kimya kana kwamba sisi sio kitu, kana kwamba mnaweza kutufanyia chohchote mtakacho.
Kumbukeni sisi sio watoto wa shule ya msingi. Ni watu wazima wenye taaluma zao. Sisi ni moja ya wanaochangia kwenye pato la taifa ila mnatuchukulia poa tu, kana kwamba hatuna lolote la maana. Tambueni ukimya wenu ni dharau kubwa sana kwetu.
NBAA MMETUDHARAU SANA WAHASIBU.