Nazikataa rasmi takwimu hizi!

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
May 11, 2008
14,005
7,180
Kiwango cha wasio jua kusoma na kuandika nchini Tanzania kimeongezeka kwa asilimia mbili tangu mwaka 1992.

Kulingana na Takwimu zilizotolewa na mkurugenzi wa taasisi ya elimu ya watu wazima Lambertha Mahai zinaonesha kwamba asilimia 31 ya watanzania watu wazima hawajui kusoma na kuandika.
Amesema takwimu hizo zinaonesha kuondokana kabiza na elimu ya watu wazima ambayo ilikuwa inafanya vizuri miaka ya sabini wakati elimu ya watu wazima ilipewa umuhimu mkubwa.

SOURCE: EAR
 

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
May 11, 2008
14,005
7,180
Kuna tabia ya wafanyakazi wa vitengo fulani kutengeneza takwimu zinazoashiria kuwepo kwa tatizo lisilokuwepo ili mradi tu wapate sababu ya kuongezewa bajeti.Takwimu hizi ni ishara tosha kuwa waliofanya tathmini wanajaribu kutetea umuhimu wa kuwepo kwa mradi fulani!
 

Mkandara

JF-Expert Member
Mar 3, 2006
15,534
8,617
samahani wakuu mnachokataa hapa ni kipi haswa!..
Kuwa sii kweli asilimia hiyo ni KUBWA ama NDOGO!...
Ningewashauri zaidi kama mkizisoma takwimu zilizotangulia toka miaka ya 85 mtaona kwamba asilimia ya wanafunzi waliojiunga na shule za msingi zilishuka sana...
Sasa kama watu hawakwenda shule ya msingi mnategemea vipi leo hii baada ya miaka 20, hawa wtu watakuwa kundi gani!
Dawa ya kutokuwa na asilimia kama hii ni elimu ya msingi ambayo kwa ujinga wetu wenyewe tuliona elimu haina maana isipokuwa biashara...na ujinga huu wa Mdanganyika ndio chimbuko kubwa la kujenga taifa lenye machinga na wapiga debe.. hawa tunao graduates wengi kuliko hata wale wa elimu ya sekondari.
 

Mpita Njia

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
6,997
1,156
Nadhani kweli kuna tatizo kwenye takwimu. Niliwahi kuiona hiyo ripoti na kwa namba inasema watanzania takribani milioni tano hawajui kusoma na kuandika. ukichukulia kwa percentage, hii ni asilimia 13 ya watanzania takribani milioni 36 na si asilimia 31. nadhani walikosea wakati wa kuchapisha takwimu badala ya 13 wakaandika 31
 

Mkandara

JF-Expert Member
Mar 3, 2006
15,534
8,617
Mpita Njia,
Labda hukusoma vizuri takwimu zilizotolewa.
Wamesema:- Asilimia 31 ya watanzania WATU WAZIMA hawajui kusoma na kuandika..
Hii ikiwa na maana ni lazima kwanza ufahamu watu wazima wanatengeneza asilimia ngapi ya population ya nchi.
Hesabu uliyoitoa inahusiana na WATU wote hivyo kupungua kwa asilimia toka 31 kuja 13 kunatokana na kuwa kizazi kipya sasa hivi wengi wamepata elimu ya msingi.
Na hii bado haipotoshi heshima na takwimu ambazo zinaweza kutolewa wakilenga UJINGA...binafsi naamini kujua kusoma na kuandika sio kuondoa ujinga ila ni hatua ya kwanza ktk kuondoa ujinga.
 

Mpita Njia

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
6,997
1,156
OK. Kwa hesabu nilizopiga, kama wasiojua kusoma ni watu milioni tano, ndio kusema kuna watu wazima milioni takriban 16 tz. Is that the case wka mujibu wa data za sensa?
 

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
May 11, 2008
14,005
7,180
Katika uchaguzi wa rais wa mwaka 2005 kulikuwa na wapiga kura around milion 11. Hii ni kusema kulikuwa na almost asilimia 50 ya wapiga kura ambao hawajui kusoma na kuandika, that is to say we have a serious problem.
Kinachonifanya nikatae hizi takwimu ni kwamba asilimia 31 inamaanisha katika kila watu wazima watatu kuna mmoja asiyejua kusoma na kuandika. Sasa kwa vile utu uzima unaanzia miaka 18 then inamaana iwapo takwimu hizi zingekuwa sahihi basi Tanzania ingekuwa kila siku tunakutana na watu wasiojua kusoma na kuandika. Ukweli unaoonekana ni tofauti, just jiulize wewe lini umekutana na mtanzania asiyejua kusoma na kuandika!
 

Obe

JF-Expert Member
Dec 31, 2007
9,734
33,495
Labda naweza kuonekana kivingine, lakini jaribu kufanya utafiti wa kutaka kujua watu wanaohitaji msaada katika wilaya. Majibu utakayopatiwa utashangaa kwani karibu kila anayehojiwa atasema anhitaji msaada (nadhani hata na mhojaji)

Suala la kutengezeza takwimu ili bajeti iongezwe si geni hapa bongo


Ukijikataa hakuna atakayekukubali
 

Mpita Njia

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
6,997
1,156
Sasa hizi takwimu zinareflect reality au zimetengenezwa kwa ajili ya kuombea bajeti?
 

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,342
38,997
mbona hizi takwimu zinakubalika? hivi watu wazima wangapi wanajua kusoma na kuandika? Tulipoacha kutilia mkazo "kisomo cha watu wazima" tulitarajia watu wazima wajifunze wapi? Mwishoni mwa miaka ya sabini literacy level tanzania ilikuwa over 90 percent.. kilichotokea nini? Mimi nazikubali takwimu hizi kwa sababu they make sense!
 

Mkandara

JF-Expert Member
Mar 3, 2006
15,534
8,617
Nakukubali Mwanakijiji, sema tu tatizo la wengi hapa ni hili swala la kuanzisha upya elimu ya watu wazima!... hivyo takwimu hizi zinahusishwa na sera nzima ya elimu ya watu wazima ambao walisahauliwa na serikali hii miaka 20 iliyopita!... Kibaya zaidi ni kwamba nani ataweza kuacha kuuza maembe arudi shule kusoma na kuandika ambako hakuwezi kuweka mkate mezani?...
Hii ni nchi isiyokuwa na malengo wala vipaumbele hivyo upuuzi mtupu wa kufikiria kuweka elimu ya watu wazima baada ya matokeo ni nafasi ya kutafuta ulaji.
 

Fundi Mchundo

Platinum Member
Nov 9, 2007
7,791
4,853
Wakuu Mkandara na Mzee Mwanakijiji!
Matatizo ya wengi wetu ni kuwa tunapenda kudanganywa! Mbona hakuna anayepinga takwimu za kukua kwa uchumi? Katika social sector hali ni mbaya sana! Takwimu za vifo vya wakina mama wanaojifungua, watoto walio chini ya miaka mitano ni aibu tupu. hao wanaodhania kuwa hatua tuliyopiga kielimu chini ya sera za ujamaa bado zinaendelea wako ndotoni. Tuliacha kuwekeza kwenye elimu (ya watoto na watu wazima) na haya ndiyo matokeo yake. Badala ya kulalama, tujiulize tumefikaje vipi hapa na tufanye nini ili tutoke tulipo. Takwimu hazikusanywi Darisalama tu bali hata huko ambako bado wanadhani Nyerere ndiye mtawala wa nchi yetu. Tujikumbushe tulivyokuwa tunasema zamani" Aluta Continua........."

Amandla.......!
 

KOMBAJR

JF-Expert Member
Nov 15, 2011
5,829
1,267
Hii aitofautiani sana na zile Takwimu za Nape kuwa wanachama wa CCM ni 5mil.:wacko:
 

POMPO

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
6,690
2,397
Na itazidi kuporomoka sana tu Liwalo na Liwe anawaza kuwapeleka Waalimu mahakamani badala ya kutatua kero zao, tunategemea nini Kilimo kwanza kimemshinda, bora wa Elimu kwanza
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom